Dk Slaa: Ufisadi umekuwa ni kielelezo cha taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Ufisadi umekuwa ni kielelezo cha taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, May 26, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot] KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Wilbrod Slaa amesema vitendo vya ufisadi, ubinafsi, kutowajibika na kukosa uzalendo vimekuwa ni kielelezo cha taifa machoni pa watanzania na wageni wanaokuja kutembelea nchini.

  Slaa alisema kuwa inashangaza kuona mashirika muhimu ya umma katika taifa yenye dhamana ya kutoa huduma kwa jamii yakiwa katika hali mbaya kiutendaji na kushindwa kutoa huduma hizo kwa ufanisi jambo ambalo hutoa sifa mbaya kwa taifa.

  Alieleza hayo akichangia mada kwenye mtandao wa Twitter juzi iliyosema kuwa ‘Utajuaje kama upo Tanzania’ iliyolenga kuwapa fursa watu mbalimbali kubainisha vielelezo vizuri kwa maana ya mafanikio na vibaya kwa maana ya kasoro vinavyomfanya mtu ajue yupo Tanzania.

  Akitolea mfano vielelezo cha madudu nchini Slaa alisema kuwa “kielelezo cha kuwa upo Tanzania ni pale unapoona Shirika la Mawasiliano, TTCL likiwa katika hali mbaya na kushindwa kuonyesha ufanisi wake, huwezi kujua limekufa, linaumwa au liko hai”.

  Slaa alisema mbali na TTCL, kielelezo cha madudu nchini pia ni kuona wanasiasa wakichochea udini na ukabila majukwaani wakati misingi ya nchi inahimiza watu kuishi kwa amani na upendo bila kuulizana wala kubaguana kidini, kikabila wala rangi.

  Katika maoni yake alishangaa kuona Rais wa nchi anashindwa kujua kwanini nchi yake ni masikini huku akisikitishwa na kuona wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika wakifaulu kuingia sekondari.

  Aliwaponda watu wanaotumia muda mwingi kushangilia na kutamba mitaani baada ya timu za ligi za ulaya kushinda katika mechi zake wakishindwa kushangilia timu za nyumbani na hata kujali maendeleo ya nchi yao.

  “Utajua kuwa upo Tanzania endapo utaona Serikali inawaita wezi ‘wajanja wachache’ wanaoliibia taifa au wanasiasa wachache wakitumia muda mwingi mahakamani badala ya kuwatumikia wapiga kura wao,” alisema Slaa.

  Alisema mbali na changamoto hizo pia hapendezwi na askari wa usalama barabarani wanaoongea na simu katika vituo vyao vya kazi huku magari yakiwa yamekwama kwenye foleni jambo ambalo ni kielelezo tosha kinachoweza kumfanya mtu yeyote hata kama ni mgeni atambue kuwa yupo Tanzania aliyoiita ya ‘wajanja’.

  Mada hiyo ilichangiwa na watu wengi wakiwemo wanamuziki, wananchi na watu maarufu ambao kila mmoja alitoa dukuduku lake moyoni juu ya vielelezo vya Tanzania machoni pa watanzania wenyewe na wageni.[/FONT]
   
 2. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Kaazi kweli kweli
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkuu. Magazeti ya jana yameripoti kwamba China (nchi ambayo magamba wanapenda sana kujinasibu nayo ukiondoa adhabu ya kunyongwa ambayo wanajua 80% yao watakula vitanzi ikiwa introduced nchini), wamepitisha sheria ya viwango vya usafi katika VYOO VYA UMMA.

  Kwa sheria hii, ni marufuku choo cha umma kuwa na/kuonenkana nzi zaidi ya wawili (2) kwa wakati mmoja na msimamizi wa ofisi husika atawajibishwa endapo atashindwa kusimamia hili! Wenzetu wamefikia hatua kama hizi za uwajibikaji sisi majizi yanayouza nchi tunacheka nayo. AIBU.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Eti wanasema sasa hivi tumeendelea kuliko miaka 30 iliyopita maana karibu kila kiongozi wa umma ana biashara inayotokana na kazi yake.
   
 5. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dr. Vp CCBRT?! Maana nishasikia harufu ya Ufisadi pia.
   
 6. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Moja wapo ya kauli ambayo muandishi wa hiyo makala hapo juu ameicha na ambayo ni muhimu sana iliyotolewa na Dr Slaa kwenye huo mjadala kama jinsi zilivyokuwa muhimu hizo kauli nyingine alisema "You can still a pair of shoes and get stoned to death but rob the nation and walk free".

  Hapa unaweza kuvuta kiasi cha hisia ulizo kuwa nazo na kukumbuka wale wezi wa EPA walivyoambiwa warudishe fedha halafu hatukuambiwa kuwa ni nani na nani waliozirusisha na wamerudisha kiasi gani na hatua gani zimechukuliwa baada ya kubainika kuwa wao ndio wameiba?! Halafu vuta tena kiasi cha hisia kwa kukumbuka idadi ya vifo vya vibaka walio uwawa kwa kupigwa baada ya kuiba simu au ndala za kuogea.

  Wa'methubutu, wa'meweza na bado wanasonga mbele, kwa ari zadi, nguvu zaidi, na kasi zaidi tena mara hii kwa utii wa sheria pasipo shuruti. Tanzania bila Marelia inawezekana.
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye red ni STEAL na sio STILL! halafu ni MALARIA na sio MARELIA
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi ni mdau mzuri tu pale, ninayo furaha kukueleza kwamba CCBRT is one of the best performer wa health care nchini kwa kila indicator... hata za finances

  cha maana ni kupunguza nguvu tu za wale wazungu kwenye pesa

  Naskia muhimbili wanajitahidi kweli kwenye kuzuia ufisadi na wameshaifikia 30% ya performance
   
Loading...