Dk. Slaa: Safu Mpya ya CCM imejaa Taswira ya Ufisadi

Ungekua na ka-umri kidogo kujua niko upande gani, basi ungeweka makalio chini
Huo upande ni upi zaidi ya kuwa gamba,njaa kali na mchumia tumbo...mafisadi wakubwa mkitembea mnajam...ba hovyo hovyo tu shauri ya viposho vya lumumba....
 
Willibrod-Slaa.jpg

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia Dr Slaa

• Adai wateule wapya wana taswira ya ufisadi

na Mwandishi wetu


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameichambua safu mpya ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoundwa hivi karibuni mjini Dodoma, akisema wana taswira ya ufisadi.
Amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi yao kuhusika kwenye matukio kadhaa ya kifisadi moja kwa moja.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusu mtazamo wake kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu uliomalizika juzi, Dk. Slaa alisema haoni jambo jipya.
“Nadhani hakuna jambo jipya, kipya ni kwamba wameteuliwa jana, lakini wote ni wazoefu wachafu,” alisema.
Katika safu hiyo, Kikwete anasaidiwa na makamu wawili, Philip Mangula wa bara na Dk. Ali Mohamed Shein wa visiwani na pia alimteua kada mkongwe, Abdullahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM.
Wengine wanaounda Sekretarieti ni Zakhia Meghji, Mwigulu Nchemba, Asha-rose Migiro, Vuai Ali Vuai, Nape Nnauye na Mohamed Seif Khatib.
Akimchambua mmoja baada ya mwingine, Dk. Slaa alimtuhumu Mangula kuwa ni mmoja wa watu waliohusika na ufisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.
“Makamu Mwenyekiti Mangula anahusika na EPA, vimemo vingi vya kutaka fedha za EPA vimetokea kwake…sioni leo atajisafishaje kuleta tumaini jipya kwa Watanzania,” alisema.
Kuhusu Meghji, Dk. Slaa alisema huyo ndiye aliyeandika barua na kudanganya kuwa fedha hizo za EPA zimetoka kwa ajili ya Usalama wa Taifa.
“Sasa mtu kama huyo aliyedanganya, leo hii ukamweka kwenye fedha maana yake ni ku-‘recycle material’ ile ile,” alisema Dk. Slaa.
Akimchambua Katibu Mkuu, Kinana, alisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli na kwamba hajakanusha mpaka sasa.
Dk. Slaa alisema Kinana ambaye alikuwa meneja kampeni wa mgombea urais wa CCM mwaka 2010, katika chaguzi hizo CCM imeshutumiwa kwa kuiba kura, hivyo uteuzi wake ni kukubali kuzika demokrasia nchini.
Alisema timu hiyo imeundwa mahsusi kwa ajili ya kujiandaa kuiba kura mwaka 2015.
Dk. Slaa aliongeza kuwa baada ya uchaguzi, CCM walitumia fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti wa kukijenga upya chama chao, ambao uliozaa kauli mbiu ya ‘Kujivua Gamba’, kwamba pamoja na kazi ya kitaalamu wameshindwa kuvuana magamba.
Alifafanua kuwa hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba walioitwa magamba sasa wamo kwenye safu mpya ya uongozi wa CCM.
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kumjibu Rais Kikwete hasa kutokana na kauli yake kuwa wapinzani wanafanya kazi ya kueneza uongo na kuwataka makada wa CCM kujibu mapigo, Dk. Slaa alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.
Dk. Slaa alisema kuwa Rais Kikwete huenda hasomi, anadanganywa au anapenda lugha rahisi za kusema wenzake waongo.
“Mawaziri wameutumia Mkutano Mkuu kwa mbwembwe kueleza uongo…katika ripoti ya Juni 2012, hali ya uchumi wa taifa, iliyoandikwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Mipango, na kelele zote zilizopigwa kuhusu maendeleo yaliyopatikana kwenye barabara.
“Kwenye ripoti hiyo imeandikwa kuwa mwaka 2011 barabara zilizokuwa katika hali nzuri ni kilomita 5,976 sawa na asilimia 30.4 ya barabara zote za mikoa,” alisema.
Ukilinganisha na mwaka 2010, barabara zilizokuwa na hali nzuri ni kilomita 11,012, maana yake ni kuwa nusu ya barabara zilizokuwa nzuri mwaka 2010 leo mwaka mmoja baadaye ni mbaya.
Aliongeza kuwa wakizitumia takwimu hizo ambazo zimeandikwa na Ofisi ya Rais, bado wanaambiwa ni waongo.
Alisema itakumbukwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga wakati alipotoa orodha ya mafisadi, Rais Kikwete alimjibu kuwa kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala lakini leo amekiri ufisadi upo CCM.
Mwanasiasa huyo machachari, alisema kuwa Rais Kikwete amesikika mara kadhaa akilalamika kuhusu ufisadi ndani ya chama chake na kuhoji kati yake yeye na Kikwete nani muongo?
“Aidha Rais sio makini; anapenda maneno rahisi…tunamwambia aweke hadharani takwimu asilete propaganda,” alisema.
Slaa alikumbusha pia jinsi ambavyo Rais Kikwete na CCM walivyowaita ni waongo wakati CHADEMA walipokuja na sera ya matumaini kwa Watanzania mwaka 2010, wakisema nyumba za tembe na nyasi sasa basi na kueleza mikakati yao ya kushusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.
Katika hilo Dk. Slaa alisema kuwa alifurahi juzi kusikia CCM katika maazimio ya Mkutano Mkuu wao wakisema kuwa watashusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.
“Sasa CCM na CHADEMA nani waongo? Mimi nasema hakuna kitu kinachotushangaza katika uongozi wa sasa, timu ni ile ile ya mafisadi,” alisema
Aliwataka Watanzania kuwa makini akidai kuwa waliowekwa kwenye safu ya uongozi CCM ni mafundi wa ufisadi na kutoa wito kuwa wajiandae kulinda kura.
Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza, alisema wao kama chama wanawapongeza CCM lakini kwa jicho la siasa hawaoni kipya na kwamba viongozi wapya ni wachovu wale wale.
“Hawana jambo jipya kwa sababu CCM imechoka sana haina watu wapya ni walewale, sasa hivi tulitegemea vijana wapya lakini hilo halijatokea,” alisema Ruhuza.
JK awasuta wabaya CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewashambulia wanachama wa chama hicho waliokuwa na ndoto za kuona mkutano mkuu wao ukimalizika kwa mpasuko, akisema kuwa wameshindwa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya kuiteua sekretarieti ya chama hicho, itakayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdullahman Kinana.
Akiwatambulisha rasmi wateule hao, Rais Kikwete alisema anawashangaa baadhi ya wanachama ambao wanaifahamu vizuri CCM lakini walikuwa wakiombea mabaya ili mkutano umalizike vibaya waweze kujivunia kile walichokikusudia.
“Namshukuru sana Mungu tumemaliza salama; kuna watu walikuwa wakitambika usiku na mchana CCM imalize vibaya mkutano wake na walitamani itoke na vipande lakini wameshindwa na sijui watamdai nani gharama zao?” alihoji.
Alisema watu hao wamepoteza muda wao bure na CCM imara imeweza kumaliza mkutano wake vizuri na kupanga safu ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuingia Ikulu mwaka 2015.
“Nimesikia mambo mengi na kuna watu kabisa walikuwa wakinijia wakiniambia kuwa kuna jambo hili na hilo, lakini nilikuwa nawaambia kuwa watulie kwani kuna watu wana ndoto za mchana wanatumia nguvu nyingi, wanatumia muda wao bure na wanapoteza wakati wao,” alisema.
Rais Kikwete alitamba kuyatekeleza maazimio yote waliyoazimia moja baada ya lingine ili kuhakikisha wanayatimiza kwa wakati na kwa muda mfupi ili Watanzania kuendelea kujenga imani na chama hicho.
Alisema wajumbe wa NEC wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kuifanya kazi ya chama ili kuweza kukijenga chama hicho kwa kiwango kikubwa.


h.sep3.gif


juu
blank.gif
 
Huo upande ni upi zaidi ya kuwa gamba,njaa kali na mchumia tumbo...mafisadi wakubwa mkitembea mnajam...ba hovyo hovyo tu shauri ya viposho vya lumumba....

una kadi ya chadema? maana mimi ninayo mkuu.... If you want to learn, then accept criticism, Slaa need to up his game to match Mbowe, Mnyika, Zitto, nk. we cant depend on one single year in year out

Hayo mengine ongea na mamako, anajua zaidi kwanini mimi ni anko wako

senzy
 
una kadi ya chadema? maana mimi ninayo mkuu.... If you want to learn, then accept criticism, Slaa need to up his game to match Mbowe, Mnyika, Zitto, nk. we cant depend on one single year in year out

Hayo mengine ongea na mamako, anajua zaidi kwanini mimi ni anko wako

senzy
Huwezi kuwa mwana Chadema mwehu hivi...nakuuliza tena ndo mlivyofundishwa na kikwete muwajibu wapinzani hivi???
 
Bwana mkubwa , kwanza kabisa ni lazima uelewe mazingira ya kitanzania yalivyo, wanasiasa wenyewe, na kule tunakoelekea.

Sijaona mwanasiasa, ndani na nje ya CCM asiyeganga njaa katika mihangaiko ya kisiasa.
Au niwe direct, nipe jina la mwana CDM ambaye kwake ana maono ya kisiasa kama Mwalimu.

Hakuna!

Nipe jina la mwanasiasa mmoja(mmoja tu) msafi katika vyama vya upinzani. Na dossier yake itatawala hapa jamvini.
Kwa hiyo msilete utetezi wa wizi, wizi upo CCM, upo CDM, upo CUF na vyama vyote.
Vyama vyote hivyo kiongozi atakayepewa nchi atataka ajinufaishe kwanza kabla ya kuachia madaraka.

Tumeona ufisadi wa kula ruzuku na hata kwenye halmashauri zilizokamatwa na CDM.
Hivyo ni kujidanganya kubaya unapoahidiwa neema na kiongozi ambaye kwao ana nyumba ya nyasi!

CCM inawazidi kete kiuongozi.
Makosa ya viongozi yanaonekana wazi, na uongozi ingalau uko wazi, umangi meza hata kama upo utapata ukomo wake.
Scenario ya vyama vya upinzani ni kama klabu za watu binafsi, ambazo ukigongana na mwenye klabu umekwisha.

Sisemi vyama vya upinzani vinakufa leo au kesho, la hasha.
Kuvipa madaraka ni heri umpe mtoto akuendeshee lori la tani 20 akufikishie mzigo wako Mwanza wakati haa leseni!

Ndugu yangu unapozungumzia mazingira ya kitanzania,unazungumzia moja ya makosa makubwa ya watawala wa sasa. Watanzania makini na safi hawataki kujiingiza ktk siasa wakihofia kusakamwa na vyombo vya usalama na dola na watawala wala rushwa! Natambua demokrasia kiasi imekua ktk utawala huu wa awamu ya nne,lakini hali ilikua mbaya awamu ya tatu!
 
una kadi ya chadema? maana mimi ninayo mkuu.... If you want to learn, then accept criticism, Slaa need to up his game to match Mbowe, Mnyika, Zitto, nk. we cant depend on one single year in year out

Hayo mengine ongea na mamako, anajua zaidi kwanini mimi ni anko wako

senzy
unaweza ukawa na kadi lakini moyoni ukawa gamba, ushabiki wa kizembe hatuwezi kuukubali, tunachoangalia ni ukweli wa kilichosemwa na si nani amekisema. Tunaipenda tanzania kuliko unavyojua!
 
una kadi ya chadema? maana mimi ninayo mkuu.... If you want to learn, then accept criticism, Slaa need to up his game to match Mbowe, Mnyika, Zitto, nk. we cant depend on one single year in year out

Hayo mengine ongea na mamako, anajua zaidi kwanini mimi ni anko wako

senzy
JF siku hizi hakuna ban? msiji tu mka:fencing:kisa wana siasa, ila matusi mazito siyo staha, tupambane kwa hoja:A S 100:
 
FYI.... Kama ujinga ni pesa, basi wewe ni bilionea

Manina wahed, laanakum nambari wani na **** wa kwanza.... KAMA NI MATUSI TU, NAYAJUA SHENZI WEWE KIMBA LA ASUBUHI, MAANA TUKIWAACHA HIVIHIVI HUWA MNAZOEA KUTUKAMA MAAMUMA MKUBWA WE
JF siku hizio raha kuna jukwaa la matusi?....Well done Mods:A S 41:
 
ni mitazamo ya kla mmoja wetu na wote hatuna ushahidi wa hcho tuambiwacho ushahidi ukiwekwa wazi dr ataendelea kuchukua watanzania siye kuwa wake lkn kwa nadharia anazofanya mimi naungana na hao wanaotaka singo mpya yenyekuakisi jamii 2liyopo siyo hyo ya kujua peke yake.
 
Katika viongozi vimeo ninaowajua mmoja wapo ni huyu Mzee wa kimbulu. Anachotaka kukiona ni vurugu na maneno yasiyo na tija. Mipango ya chama kingine inamuhusu nini? au hana la kufanya nini. Namshauri aende karatu kulima nagono maana hana capacity hata ya kujadili hoja badala yake amekuwa mtu wa lawama na kuibua hoja zilizopitwa na wakati. Hivi hoja ya EPA ndiyoo itamfikisha ikulu kwa sasa. Nawashauri Chadema wajipange vizuri kama chama, waje na hoja za kitaifa na watuonyeshe uwezo wao kuliongoza taifa hili. Petty politics kwa ajili ya watu ni hatari kwa taifa letu. Siioni Tanzania yangu chini ya huyu mzeee ambae hata mke hana.
 
Yeye si ana ushahidi? na ana uchungu na nchi hii? kwanini azunguke zunguke na ushahidi ktk majukwaa ya siasa badala ya kuwashitaki mahakamani? unapozunguka kila kona na ushahidi wa uongo majukwaani una lengo la kuchochea wananchi ili wakasirike na kuamua kuvunja sheria kama wanavyofanya sasa huko Mwanza!

Ndugu nchi hii ina mahakama, tupeleke kesi zetu huko na tuache kutafuta umaarufu kupitia mgongo wa machinga!

Du Kwahiyo EPA ni UONGO?
 
Katika viongozi vimeo ninaowajua mmoja wapo ni huyu Mzee wa kimbulu. Anachotaka kukiona ni vurugu na maneno yasiyo na tija. Mipango ya chama kingine inamuhusu nini? au hana la kufanya nini. Namshauri aende karatu kulima nagono maana hana capacity hata ya kujadili hoja badala yake amekuwa mtu wa lawama na kuibua hoja zilizopitwa na wakati. Hivi hoja ya EPA ndiyoo itamfikisha ikulu kwa sasa. Nawashauri Chadema wajipange vizuri kama chama, waje na hoja za kitaifa na watuonyeshe uwezo wao kuliongoza taifa hili. Petty politics kwa ajili ya watu ni hatari kwa taifa letu. Siioni Tanzania yangu chini ya huyu mzeee ambae hata mke hana.
kwa hiyo hoja ni kutokuwa na mke dk? Ufisadi wa Epa sio hoja? Kama kuna mtu aliwahi fanya ufisadi hata kama mwaka 47 huyo hatufai! Ccm hawana lengo la kulisaidia taifa hili ni ufisadi na kujuana tu.
 
Ha ha ha !
Padiri hana uwezo wa kingine, afanye nini!
Amekariri ukurasa huo huo tena na tena,na tena!
Kisiasa ndio mwisho wa lami!

Kwenye UFISADI ndiyo ukurasa unaotusumbua sana,CCM wameshikilia sana hapo! wanakwiba kama hawana akili nzuri! EPA,MEREMETA,TICS,GREEN DEEP,DOWANS,RICHMOND,MIKATABA FEKI na mengine mengi tu machafu
 
Ukurasa wa kuimba ufisadi hadi watoto wa cheechea wanaujua, mwambieni Padiri aanze kuimba wimbo tofauti wa jinsi ya kupeleka maendeleo vijijini.
Wengi wetu hatuna imani naye kujifunzia kazi akiwa ikulu.
Kulaumu na kunyooshea vidole ndiyo vitu pekee anavyofahamu.
Mbaya zaidi maadili yake hayambebi.

Kama neno ufisadi linawakera sana si muuondoe sasa? Hayo maendeleo unayosema Padri Slaa ayazungumzie yatapatikana vipi wakati kila fedha zinazochumwa ili zilete hayo maendeleo zinatafunwa na wabaka uchumi wa aina ya Kinana mnaowapa vyeo sasa? Yaani akili yako ya kawaida inashindwa kutambua kwamba ufisadi na maendeleo havikai pamoja?

Kama mnapiga kelele tu neno ufisadi lisitamkwe bila kuuondoa hakika hamtafanikiwa na hakuna mpuuzi atakayewaachia.Mtafukuzwa na kuzomewa mitaani kote as far as mnachotafuna ni mali ya umma na si ya mtu binafsi.Bahati nzuri kwenye ufisadi si suala la chama ni mapambano ya umma mzima dhidi ya mafisadi wachache
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom