Dk. Slaa: Nitaendelea kuwaumbua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: Nitaendelea kuwaumbua CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Facts1, Dec 31, 2009.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na Joseph Mwendapole
  31st December 2009


  [​IMG] Asema anachunguza kama mali zote zimelipiwa kodi
  [​IMG] Aahidi kuwa baada ya hapo ataweka wazi kila kitu


  [​IMG]
  Dk. Wilbroad Slaa


  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amesema kuwa ataendelea kufichua ufisadi unaofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema) ameendelea kuwaweka tumbo joto viongozi wa CCM, baada ya kutangaza kuwa ameanza kuchunguza mali zote za chama hicho kama zililipiwa kodi na kisha ataweka mambo hadharani. Vile vile, amesema (CCM), inapaswa kulipa kodi ya Sh. bilioni sita kwa magari 200 iliyoagiza badala ya bilioni 1.7 kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.

  Akizungumza na Nipashe, Dk. Slaa alisema atafuatilia hadi dakika ya mwisho kuhakikisha CCM kinalipa kodi hiyo ili iweze kuwanufaisha Watanzania wengi maskini.

  “Sitaki malumbano na mtu yeyote, ninachotaka kuona ni CCM inalipa kodi yote hiyo ili shule, hospitali, barabara na huduma zingine za jamii zipatikane,” alisema Dk. Slaa.

  Akiwa mkoani Tanga wakati wa operesheni Sangara iliyoendeshwa katika wilaya zote za mkoa huo pamoja na Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Dk. Slaa alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa CCM kimeingiza nchini magari 200 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwakani bila kulipia ushuru wa Sh. milioni 600.

  Hata hivyo, anasema kuwa alinukuriwa vibaya na kwamba kiasi sahihi cha kodi inayostahili kulipwa na chama tawala kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni Sh. bilioni sita.

  Alisema kama Makamba alisema walilipa kodi ya bilioni 1.7 alipaswa kuwaeleza waandishi wa habari kiasi cha jumla ya kodi yote ya magari 200 waliyopaswa kuilipa.

  Kuhusu kauli ya CCM iliyotolewa na kuwa haitamshitaki kwa kuwa aibu iliyompata mbele ya jamii kwa kusema uongo inatosha, Dk. Slaa alisema hawezi kulumbana na Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Amos Makala, kwa kuwa sio saizi yake.

  “Aliyeitisha mkutano na kusema maneno hayo ni Makala, sasa mimi si wa kujibishana na mtu kama huyo maana si saizi yangu,” alisema na kuongeza: “Wananchi ndio wataamua nani kapata aibu kati yangu na CCM na kwa taarifa yao nitaendelea kuchunguza ukwepaji wao kodi,” alisema Dk. Slaa, ambaye amekuwa akiibua kashfa mbalimbali za ufisadi dhidi ya Serikali.

  Siku chache baada ya Makamba kumjibu Dk. Slaa akisema kuwa chama chake kimeyalipia magari hayo kodi ya Sh. bilioni 1.7 na kutishia kuwa kitamchukulia hatua za kisheria, Makala naye aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa chama hicho tawala hakina tena mpango wa kumshitaki Slaa, kwa kuwa aibu aliyoipata ya kusema uongo kwa jamii inamtosha.

  Septemba 15, mwaka 2007 katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam Dk. Slaa alitaja majina ya vigogo kadhaa wa serikali na CCM kuwa ni mafisadi kwa kuwa wanahusika katika tuhuma kadha za vitendo vya ufisadi.

  Baada ya kutoa tuhuma hizo, baadhi yao walitishia kumfikisha mahakamani lakini hadi leo hakuna hata kigogo mmoja miongoni mwao aliyemshitaki.

  Hata hivyo, baadhi yao walikumbwa na kashfa za ufisadi na kulazimishwa kujiuzulu na wengine kufunguliwa mashitaka mahakamani huku baadhi yao wakiendelea kutuhumiwa ingawa hawajachukuliwa hatua za kisheria.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. e

  echonza Senior Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo, hiyo ni vita ya wote. Lakini si kwa kuwalenga CCM tu, bali kama wananchi wazalendo tutahakikisha kila anayetakiwa kulipa kodi anafanya hivyo. Na kama sivyo basi tukiwa na taarifa tuwashitaki kwa umma haraka iwezekanavyo. CCM kama chama tawala, wanatakiwa wawe mstari wa mbele kuhakikisha mapato ya nchi yanaongezeka kupitia ukusanyaji wa kodi mbalimbali ikiwemo ilipwayo na chama hicho.
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mchimba kisima huingia mwenyewe, Muosha huoshwa
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mchimba kisima huingia mwenyewe, Muosha huoshwa
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safi sana katika kujua na kuona kuwa kila mtu anafaidi rasilimali za taifa hili maana kuna kila haki ya kujua mali zote na vyanzo vyao
   
 6. M

  Mulugwanza Member

  #6
  Dec 31, 2009
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Naomba email address ya Dr. Slaa. Asante!
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Endelea baba tuko nyuma yako.Waambue mpaka kieleweke
   
 8. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  I can tell you Dr. Slaa is un-tishable to use Kiswanglish! This has really rattled CCM out it hole!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Makala bwana na maneno yale . Yaani aka twist oh ni magari 150 , Makamba akasema n magari 200 na ushuru umesha lipwa . Sasa kuonyesha ukweli ni kwamba Makala gawa doc zenye info sahihi za idadi ya magari na kodi iliyo lipwa maana si siri tena . Ili uweze kusema Dr.Slaa kaumbuka .Usikimbilie kusema hakuna mahakama kwa kuwa kaumbuka how ?Mkienda Mahakamani ujue itakuwa moto zaidi docs kibao zitaombwa na ukweli utakuwa kama bahari na kama CCM mnabisha nendeni hata kama Mahakama ni zenu
   
Loading...