Dk Slaa: Nimeunasa waraka wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Nimeunasa waraka wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Maxence Melo, Aug 4, 2010.

 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Tumaini Msowoya, Iringa na Brandy Nelson, Mbeya
  Mwananchi

  August 3, 2010


  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Willibrod Slaa jana aliendelea kuvuta watu wengi kwenye mikutano yake mjini Mbeya na Iringa ambako aliwaeleza wananchi kuwa ameinasa barua kutoka makao makuu ya CCM kwenda kwa wakuu wa wilaya ikiwataka kuwakusanya wafanyabiashara katika maeneo yao ili wawachangie fedha kwa ajili ya kampeni za chama hicho.

  Dk Slaa alikuwa mjini Iringa na Mbeya kusaka wadhamini baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya Chadema, alikumbana na tatizo la kunyimwa kutumia Uwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa baada ya Jeshi la Polisi kuelezwa kuwa sehemu hiyo itatumika kwa ajili ya shughuli za mbio za mwenge na baadaye mchana kuzuiwa na CCm kutumia Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

  Akihutubia umati wa wakazi wa manispaa ya Iringa waliofurika kwenye viwanja hivyo, Dk Slaa alisema barua hiyo ameinasa wakati ikienda kwa wakuu wa wilaya.

  “Huu ni wizi wa mchana, tena kweupe," alisema mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Karatu. "Hili limeniumiza sana... (hii barua) inawasihi wafanyabishara wawachangie fedha kwa ajili ya kampeni. Hili limeniumiza sana.”

  Alisema kuwa ni vyema michango hiyo ingekuwa ikichangishwa kwa ajili ya kuinua maisha ya Watanzania ambao wamekuwa wakiishi maisha duni tofauti na falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Kuhusu wafanyakazi, Dk Slaa aliibeza kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba hahitaji kura zaidi ya laki 300,000 za wafanyakazi nchini ambao waliitisha mgomo kuishinikiza serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara na madai mengine wanayostahili.

  “Simtukani ila yeye mwenyewe kwa kinywa chake alisema hahitaji kura za wafanyakazi. Mimi nazihitaji sana kwani hawa ni wavujajasho wanaonyonywa huku watu wengine wakineemeka, mfano mzuri ni walimu wa shule za msingi ambao hulipwa Sh160,000 tu,” alisema.

  Alieleza kuwa kwa siku mbunge amekuwa akilipwa kiasi cha Sh160,000 kila akiwa bungeni wakati kiwango hicho cha fedha ndicho hulipwa mfanyakazi kwa mwezi na kukielezea kitendo hicho kuwa ni sawa na unyonyaji.

  “Walisema maisha bora kwa kila Mtanzania; maisha gani bora ambayo yamepandisha bei ya vitu huku kiwango cha mshahara kikiendelea kuwa kile kile? Bila huyo mwalimu ambaye amenifanya leo hii niitwe Dk Slaa, sidhani kama ningesimama mbele yenu,” alisema.

  Mgombea huyo aliitumia nafasi hiyo kumtangaza mwenyekiti wa wilaya ya Iringa Mjini, Dk Peter Msigwa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

  Mjini Mbeya, umati wa watu ulianza kufurika Uwanja wa Ndege kuanzia saa 8:00 mchana na wakati akiwasili helikopta iliyomchukua ilizunguka angani maeneo ya mjini Mbeya, kitendo kilichokusanya watu wengi kabla ya kutua.
  Baada ya Dk Slaa kupewa nafasi ya kuongea, alieleza jinsi

  alivyosikitishwa na kitendo poilisi kuizuia Chadema kutumia uwanja huo kama ilivyokuwa mjini Iringa.

  “Unajua kuna watu ambao wanadhani hii nchi ni mali yao peke yao," alisema. "Nimesikitishwa sana na tabia ya CCM kutunyima Uwanja wa Sokoine kufanya mkutano wakati viwanja hivi ni mali za wananchi wote kwa kuwa vilijengwa wakati wa kipindi cha chama kimoja."

  Alisema kuwa Chadema haitavumilia kitendo hicho na kwamba endapo kama chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kitanyang`anya viwanja vyote na kuwa ni mali ya Watanzania wote.

  Dr Slaa pia aliwashambulia polisi na kuwataka kuacha mara moja kufanya mchezo wa kuisaidia CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

  “Nawatahadhalisha kabisa msije mkapata matatizo... muache mchezo wenu wa kuisaidia CCM katika uchauzi mkuu. Mkitaka kufanya hivyo, mvue magwanda yetu muingie kwenye shughuli za Kisiasa”

  Kuhusu uamuzi wa kugombea urais badala ya ubunge. Dk Slaa alisema kitendo cha wananchi kujitokeza kwa wingi kinamfanya aamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa ufahamu wa kufanya hivyo.

  Akiwa mjini Iringa, Dk Slaa pia alipinga vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kumzuia kutumia Uwanja wa Mwembetogwa wa mjini Iringa kwa madai ya shughuli za mwenge.

  “Sisi tumeomba uwanja saa 4:00 asubuhi, cha ajabu polisi wanazuia uwanja huu tusiutumie ili kuuachia nafasi mwenge ambao unawasili saa 8:00 mchana kwa ajili ya kuzindua mradi. Hii maana yake nini? Au wanataka tufanyie mikutano angani? Polisi hawana mamlaka ya kuzuia matumizi ya uwanja kwa ajili ya kampeni. Nawashukuru viongozi wangu kwa kuamua kuufanyia mkutano huu hapahapa tena kwa mabavu,” alisema Dk Slaa.
   
 2. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  CCM hawatakosa la kufanya kuhakikisha ushindi wao..
  Tumeshuhudia rabsha ya wao kwa wao sembuse wa-nje..
  Wapinzani hasa Dr Slaa wasimame imara kwa kampeni zilizopangiliwa...
  Dr Slaa awahamasishe pia waende kukipigia kura Oktoba...
   
 3. r

  rimbocho Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi katika wafanyakazi 300000 ambao Kikwete kasema hataki kura zao POlice na Jeshi hawapo? au hawa si wafanya kazi? kama wapo basi ni wakati wao wakuunga mkono mageuzi ya kuondoa kiburi cha JK, na CCM. Piua nawapongeza CHADEMA kwa kuliona hili la viwanja nchi nzima kumilikiwa na CCM, huu ni ufisadi wa hali ya juu sana lazima tuvirudishe. Wana JF mnao jua sheria hili vipi tukilidai mahakamani? CCM watupe hati za umiliki wa viwanja hivyo na kodi wanayolipa serikalini kwa umiliki huo wa viwanja na majumba, mfano jengo la umoja wa vijana CCM lilijengwa na vijana wote wa nchi hii wakati wa mfumo wa chama kimoja iweje leo wafaidi akina Riziwani pekee?:hippie:
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwaka huu CCM kazi wanayo na watakiona cha moto.
  Maana wanachama wenyewe wa CCM wanamkubali Dr.Slaa kwa kile wanacho sema JK kawaangusha.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Dr simama imara Mungu yuko pamoja nawe na watanzania hasa wafanyakazi wako pamoja nawe.
  HAKIKA UTASHINDA URAISI.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  No way, hatupendi iwe hivyo, lakini kwa maslahi ya Watanzania, hii itabidi kutumika sana tu katika baadhi ya maeneo October...
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwikwikwiiiii.. endelea kuota mchana kweupeeeeee.. eti bado? endelea kusubili CHADEMA MOTO MDUNDO mpaka kieleweke!
   
 8. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "URAIS HAUZWI KAMA KALANGA"


  Redline"naomba tafsiri ya haya maneno maana siyaelewi ni lugha ya kiswahili au ni lugha gani hii,msaada wana JF.KALANGA Ninavyoijua ni kijiji kiko Togo,neno hili linatumika zaidi huko Botswana na Zimbabwe.
  Au ni malaria imepanda kichwani.
   
 9. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa hizo kura za wafanyakazi 350,000 ni kadirio la chini. Nadhani wafanyakazi hao wanawahudumia ndugu zao wengi masikini wa mjini na vijijini. Kwa hiyo ni kura za wafanyakazi hao ongeza na kura za ndugu zao wanaowategemea.
   
 10. K

  Kihega JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 1,338
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Dr.Slaa kaza buti chapa mwendo.CCM wanatapatapa,Kura zako hata ziibiwe vipi bado zitatosha kukupeleka Ikulu.
   
 11. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mungu atamuongoza... lakini nafikiri pia hao wafanyakazi na hata mtu mwingine yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yake anatakiwa sasa kuwaelewesha jamaa zao walioko vijijini, hasa mama na dada zetu kuwa ni wakati wa mabadiliko... lakini sio kupiga porojo tu...

  Inawezekana sisi wengine tunafanya kazi mjini (tuko kwenye hilo kundi la wafanyakazi 300,000 ambao JK haitaji kura zao) lakini vijijini hatuendi, wala ndugu na jamaa zetu hawamjui Dr. Slaa, wanaendelea kudanganywa na kudanganyika na kushawishika na ahadi hewa za chama tawala kwa Kanga/Vitenge au T-Shirts. Ni wakati muafaka sasa wa kuwafumbua macho ili waone mabaya na uongo wa hicho chama ili wakubali mabadiliko...

  Mungu Ibariki Tanzania...:amen:
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Slaa Silaha yetu..
   
 13. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Walimkubali mrema sembuse slaa!
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ccm anaondoka na ushindi mwaka huu.................labda baada ya miaka mitano mengine! hawa watu wako soo corrupted kwa marginal difference hawaondoki ikulu hawa
   
 15. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #15
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Weweeee ...........TIDO Mhando huna maaana na TBC yako...Usituletee umwagaji damu kama Kenya.....TANGAZA HABARI za cha CHADEMA...KUDADADEKI weeeeeeeeee.............
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yani uchaguzi against CCM ni sawa na Vita! Watatumia kila mbinu, kisa washinde tu. Bila kuwa na mentality ya kuwa vitani, CCM hutaweza kuitoa.
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  katika Ujumla wake, Dr Slaa anaweza kushinda uchaguzi, ikiwa Tu hawa wafanyakazi waserikali wakatambua haki zao za Msingi, vilevile Manesi walimu, wakulima na vijana woote vijiweni, kama kila jamii itaanza kuelimishana tangu nyumbani, makazini, mashambani na hata kwenye mabaa, bila kuchoka kwa umoja wenu nchi itakomboka toka kwenye makucha ya Mafisadi wakiongozwa na Kikwete na wenzao .
   
 18. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  zion train is coming...!
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uko tayari wewe!!
  bahati mbaya wewe siyo Mungu, na kama ni mungu basi wa mapangoni
   
 20. L

  Luveshi Senior Member

  #20
  Aug 4, 2010
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Dk. slaa lazima uchukue ushindi kwa kishindo ,.......
   
Loading...