Dk Slaa: Kwanini sikumsalimia JK

Mode, hamishia habari hii kule Chit chat na baadae Hoja Mchanganyiko. Habari hii haistahili Jukwaa la Siasa!. Hizi double standards zitatufikisha pabaya!.
Ikiuma sema....
 
Wana JF,
Poleni kwa misiba miwili ya Wabunge, kuna hili jambo linakuzwa na baadhi ya Watu ya kwa nini Dr. Slaa hakusalimiana na Rais aka JK ??? Naona Dr.Slaa ameliamulia kulitolea ufafanuzi wake. Nitanukuu baadhi ya maelezo yake:

"Siyo hulka ya Dk Slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu,” alisema Dk Slaa.

“Sasa kutoka alipokuwa amekaa Rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia Rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa,” alisema Dk Slaa.

“Mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, Dk Slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia Rais. Katika sehemu kama ile Rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa,” alisema Dk Slaa.

“Msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa” alisisitiza Dk Slaa.

Source: Mwananchi
Nawakilisha
 
Foel na Wana JF,
Nakumbuka tulilijadili kabla ya Mhusika mwenyewe Dr.Slaa kabla ya kulitolea ufafanuzi, sasa hivi amelitolea ufafanuzi. Je kujadili kwetu kumejibu maswali yetu ???

Tulishajadili hili, tena kwa undani.
 

Mkuu hili bandiko liliwekwa hapa tangu asubuhi
 
Safi sana Rais Slaa, umefuata kilichokupeleka full stop! Mambo ya kujipendekeza wewe siyo mpenzi wa ubwabwa kama Shibuda. 2015 naona kama iko mbali mpaka natamani uapishwe kabla ya uchaguzi.
 
Molemo na Wana JF,
Sikuliona hilo liliowekwa humu toka asubuhi, ila hakuna ubaya wowote, Shukrani kwa taarifa

QUOTE=Molemo;3175002]Mkuu hili bandiko liliwekwa hapa tangu asubuhi[/QUOTE]
 
Safi sana Rais Slaa, umefuata kilichokupeleka full stop! Mambo ya kujipendekeza wewe siyo mpenzi wa ubwabwa kama Shibuda. 2015 naona kama iko mbali mpaka natamani uapishwe kabla ya uchaguzi.
rais wa yanga huyo,hana mpya.
 
Acheni uwehu,,,nnchi hii kila kona watu hawajui nini vipaumbele vyetu..kusalimia kuna umuhimu gani kwa maendeleo ya nchi yetu....shenzzzz kabisa
 
 

mi nadhani huyu mwandishi angeweka heading JK HAKUMSALIMIA DK SLAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…