Dk. Slaa: CCM wachochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: CCM wachochezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 17, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG][TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]

  na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa wamebaini mpango wa makusudi unaofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani na nje ya Bunge kwa lengo la kuwahujumu.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana jioni, Dk. Slaa, alisema kuwa amelazimika kutoa tahadhari hiyo kutokana na dalili na njama alizoziona zikifanywa na CCM bungeni kupitia kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Uchumi na Fedha, Mwigulu Mchemba, ambaye pia ni mbunge wa Iramba Magharibi.
  "Leo nimemwona Mwigulu bungeni anadai eti Chedema tumefanya vurugu Singida juzi na kumuua kada wao, halafu mchana Mwenyekiti wa UVCCM wa Vyuo Vikuu, Abubakar Asenga, alizungumza na waandishi akaonyesha waraka feki na kudai ni maazimio ya Kamati Kuu ya chama chetu," alisema Dk. Slaa.

  Katibu huyo, alisisitiza kuwa CCM ndiyo waliofanya vurugu kwenye mkutano wa CHADEMA uliofanyika huko mkoani Singida na kwamba taarifa za uwepo wa vujo hizo zilikuwepo mapema lakini akashangazwa na Mwigulu, kukimbilia bungeni na kusema uongo.

  Kuhusu madai ya Spika Makinda kudai kuwa amepokea majina ya wabunge wa CHADEMA wanaodaiwa kumtumia ujumbe wa vitisho Mwigullu, Dk. Slaa alisema anamshangaa kwa kuligeuza Bunge kuwa mahakama na hivyo, akashauri kuwa madai hayo lazima yaripotiwe polisi si bungeni.

  "Sasa hizi ni mbinu zimeandaliwa kwa kuwakodi watu kufanya vurugu kwenye mikutano yetu na kueneza maneo ya uchochezi ili CHADEMA tuonekane ni chama cha vujo. Nimeseme kwamba hatuko tayari kufanyiwa mchezo huo na hao wanaotumika kufanya hivyo waache mara moja," alionya.

  Kuhusu waraka uliosambazwa jana na Asenga, ukidaiwa ni maazimio ya CC ya CHADEMA ya hivi karibuni unaokihusisha na kuchochea mgomo wa madaktari na ule wa walimu unaofukuta, Dk. Slaa, alisema kuwa aliyeuandaa ni mpumbavu kwa vile mambo yaliyoandikwa humo yanaihusu CCM.

  "Kwanza wewe ni shahidi na mchango wa Mwigulu bungeni kila mtu anaufahamu, sasa leo kuandika waraka wa kijinga kama huu ukisema CHADEMA inataka kumdhoofisha kwa kuwa ni mtetezi makini wa watu, napata shida sana huyu ana umakini gani na amemtetea nani bungeni," alihoji Dk. Slaa.

  Mbali na mengi aliyozungumza kuhusu waraka huo, Dk. Slaa alishangazwa kuona ukihusishwa kuwa umetoka kwake lakini hakuna saini ya kuonyesha ukweli kuwa aliiandika yeye badala yake limewekwa jina na salamu ambayo si ya CHADEMA.

  "Sisi salamu yetu ni ‘People's Power'…hiyo ya Idumu Nguvu ya Umma, iliyotumika kwenye waraka huo ni dhahiri kuwa imetoka CCM kwani wao husalimiana ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi'. Mimi nyaraka zangu zote zina saini yangu na hata jina langu huwa naliandika lote kwa kirefu nikitanguliza cheo changu Dr. na si Dk. kama walivyoghushi," alisema.

  Chanzo Tanzania Daima
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli CCM wameishiwa na wanatapatapa kwa kila njia......mpaka mwaka huu uishe tutaona na kusikia mengia.
  Kila kiongozi wa CCM anapanga mikakati na maneno yake mwenyewe lengo' kuidhohofisha 'CDM' ila hawatafanikiwa.
   
 3. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Novemba 2015 ikifika,
  CCM watakuwa wamejichakaza,
  kaa tambala bovu,

  Kugushi nyaraka ni usanii wa hali ya juu,
  kugushi nyaraka ni fani ya watu wenye akili,
  Mwigulu Nchemba hana akili hiyo,
  Hata kwenye Finance & accounts tu ni Pweza.

  Kugushi nyaraka ni taabu,
  kuja na stori ya kuhalalisha nyaraka feki,
  Ni next to impossible,
  Hasa ukiwa mtupu upstairs.

  Nyaraka feki za CCM,
  Siku zote hukubalika,
  kwa sababu serikali ya CCM,
  Hutumia nguvu zake zote,
  kulazimisha watu,
  wakubali nyaraka feki.

  Sasa kunakucha Tanzania,
  Mbinu chafu za CCM,
  Za kudaanganya watu,
  zinagonga mwamba na kusambaratika,
  wanajaribu kuiga,
  ujanja wa Mission Town,
  Hali wao ni washamba wa kuja,
  Machoni bado kuna Tongotongo.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hatimaye spika wa bunge ageuka hakimu
   
 5. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CCM rudini kwetu wananchi mtueleze uzuri wenu na mkanushe tuhuma kwa ushahidi!.
  Uwezo mnao, sababu mnayo na lengo lipo ni kuendelea kutawala. Mnapoteza mda kueneza uhongo fanyeni mambo yakutushawishi. Maana mnajua nini tunataka.

  Hii mnayofanya haitusaidii wananchi ambao mnatuongoza. Hatuitaji tuhuma kutoka kwenu juu ya washindani wenu tunahitaji uwajibikaji wa haki maana ninyi ndio mnaongoza. Sasa mnatuhumiwa nanyi mnatuhumu basi hakuna Serikali hapa Tz.

  Huyo Asenga na Nchemba wapeleke vizibitisho polisi hapo tutawaelewa FULL STOP
   
Loading...