Dk. Slaa: CCM kamwe hawatatuweza CHADEMA

Dk. Slaa: CCM kamwe hawatatuweza CHADEMA


Jamani mtoto mwingine kazaliwa anaitwa Jangili tena kashika HATAMU!!!
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

We ndo umechoka kusikiliza ukweli unataka kudanganywa tu...wapenda maisha duni...na hata akilini ni zero kabisa
 
kodi zetu zilifujwa mwaka 2007 kwa ushenzi na leo tena wanaamua kuzifuja,si bora zikanunue ambulance.. mwisho wenu waja.

Hivi cdm hawapokei ruzuku kutoka serikalini?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mpango wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo mawaziri kuanza ziara mikoani, hauwezi kukisaidia chama hicho kujiimarisha kisiasa wala kuathiri kasi ya Chadema ya kujipanua nchi nzima.
Chama hicho kimesema CCM hawatafanikiwa kwa kuwa zimejitokeza tuhuma nzito ambazo hazijajibiwa na serikali ya CCM kwa Watanzania na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali ya chama hicho.

Kauli hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kueleza kuwa Sekretarieti mpya ya Chama hicho inatarajia kuongozana na mawaziri kufanya ziara ya kichama mikoani kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
Nnauye alisema juzi kuwa katika ziara hiyo ambayo itaanza leo katika mikoa ya Mtwara, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, atakuwa akiambatana na baadhi ya mawaziri kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM tangu mwaka 2010.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema ziara hiyo haiwezi kukisaidia CCM kwa sababu hata mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara mikoani kuelezea utekelezaji wa bajeti ya kipindi hicho na bado hawakufanikiwa.

“CCM leo ndiyo wameamka, sisi Chadema kama ni kufanya ziara kila siku tupo mikoani, tunakumbuka mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara kama hiyo wakatumia fedha za walipa kodi Shilingi bilioni 2.5 na bado hawakufanikiwa, hawawezi kujibu hoja,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye wakati akizungumza na NIPASHE jana alikuwa njiani akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kichama, alisema CCM hawawezi kuwa na majibu ya kuwatosheleza Watanzania kutokana na kashfa na tuhuma kadhaa ambazo zimejitokeza kipindi hiki ambazo serikali yake imeshindwa kujibu na hivyo kuzua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Alitolea mfano mwaka 2007 wakati Chadema kilipowataja kwa majina baadhi ya viongozi wa serikali na CCM kwa tuhuma za ufisadi, lakini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria licha ya kuwapo kwa ushahidi wa kutosha ambao ungesaidia kuwatia hatiani.
Dk. Slaa alisema kashfa nyingine za hivi karibuni ambazo bado serikali ya CCM haijazijibu ni utoroshwaji wa meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.24 ambayo yalikamatwa na maofisa wa bandari ya Hong Kong.
Aliongeza kuwa kashfa nyingine ambazo Watanzania wanataka majibu ni usafirishaji wa wanyama hai akiwamo twiga kwenda nje ya nchi.

Dk. Slaa alisema CCM lazima itambue kuwa kikatiba kazi ya wapinzani ni kusema na serikaki kazi yake kubwa iwe ni kujibu hoja kwa vitendo kwa kutekeleza mambo yanayokuwa yanalalamikiwa.
“Wapinzani kazi yao ni kusema au kuisema serikali iliyopo madarakani, na serikali kwa upande wake inatakiwa kutekeleza mambo yanayolalamikiwa na nchi inaendelea kusonga mbele, lakini inashangaza unapoona serikali nayo inafanya propaganda za kisiasa, hii ni hatari,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kama serikali itaendelea kuzungumzia propaganda za kisiasa kwa kujibu kwa maneno wapinzani badala ya kutenda kwa vitendo, nchi itaendelea kurudi nyuma kimaendeleo na wananchi wataendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
“Watanzania wanataka kujua lini CCM na serikali yake watachukua hatua za dhati kukabiliana na ufisadi, CCM wasifikiri ajenda ya ufisadi itaishia hewani…hapana itakuwa ya kudumu hadi tutakapoona hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika,” alisema


Source:Nipashe Jumatano

Mkatae mkubali slaa ni kiboko ya ccm tu.. na imebakia kidogo tu tutokomeze huyu mdudu ccm.
 
NAPE kuwa na huruma,hospital ya BOMBO tanga ndio kituo cha afya,hosp ya wilaya na mkoa!kila mgonjwa anashare nusu shuka
 
Naona magamba humu ndani mapovu yanawatoka kumbe ukweli unaumae,jamani dr.wetu ni noma!
 
Hapo kasema Facts zipi mkuu? au ndo wale wale bendera fuata upepo, madam kasema SLAA basi ni facts.

Kasema kwamba wanakwenda kundi kubwa wanatumia mabilioni ya walala hoi kukagua miradi ya milioni tano kama shule za kata na zahanati na wakati huo huo hata kama wakikuta uozo hawataushughulikia maana ni kawaida yao kuwalinda wezi.Vip kwani wewe hujiongezi hata kidogo?Yaani tumechoka hii misafara isiyo na tija kama vile mwenge.Wanatumia mabilioni kukagua miradi ya ajabu alafu wanasafirisha kondom ili watakao lala kwenye mwenge wasiathirike sasa kama ndo hvyo kwann wasisitishe hiyo mikusanyiko ili kupunguza maambukizi maana wapo wengi wanakuwa wamelewa sana kiac kwamba hawawez hata kukumbka kuvaa hyo zana.Mkuu CCM IMECHOKA,IMEFIRISIKA,IMEZEEKA,NA HAINAJPYA.NAWASHANGAA WASIOELEWA HUU UKWELI.
 
Huyu SLAA mbona kazi yake ni kufuatilia tu CCM? CCM wao wamesema KINANA anafuatana na mawaziri kukagua shughuli za maendeleo, yeye anakuja na hoja kuwa CCM haitawaweza, kwani CCM wanakwenda kwenye kampeni au kukagua miradi ya maendeleo? SLAA aache kumuogopa KINANA na kuanza kuomba msaada wa wananchi kwa propaganda zake.


Siyo kosa lako huelewi mlolongo mzima ulivyoanza, CCM wamesema wanaenda kujibu mapigo ya CCM kwa kutumia Secretariat Mpya na Mawaziri kuzunguka inchi nzima..... Sasa Chadema wakisema hawatuwezi kuna tatizo gani...

Hivi madai ya Ufisadi na wizi wa mali za umma yatajibiwa kwa kwenda kuzunguka mkoani au kwa kupeleka wahusika mahakamani????

Hivi madai ya Madaktari na Waalimu yatatatuliwa kwa kwenda kuzunguka mikoani????

Hivi mfumuko wa bei utapungua kwa kuzunguka nchi nzima na kujilipa allowance kweli????

Mimi nadhani kuna tatizo, CCM inatakiwa kuwaweka watu ambao wako safi madarakani ni si hawa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kila kukicha.
 
ukweli ni kuwa ccm inamuogopa slaa na cdm kwa ujumla
 
Lazima afuatilie kwa maana Magamba wamesema wanafanya ziara ya kichama! KICHAMA kwakutumia kodi zetu? Haki ya MUNGU naapa kufa kwa kupambana na magamba! kawaambie hatuchagui magamba tena alaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!
 
Huyu SLAA mbona kazi yake ni kufuatilia tu CCM? CCM wao wamesema KINANA anafuatana na mawaziri kukagua shughuli za maendeleo, yeye anakuja na hoja kuwa CCM haitawaweza, kwani CCM wanakwenda kwenye kampeni au kukagua miradi ya maendeleo? SLAA aache kumuogopa KINANA na kuanza kuomba msaada wa wananchi kwa propaganda zake.

Wewe nawe kama kichwa cha panzi kinAchofikiria kula na ----. Hujiulizi kuwa fedha zetu za walipa kodi zitatumika na mashAngingi ya mawaziri na maofisa wengine wa serikali? Hata usikute wameshachota fedha zingine za walipa kudi kuanzia mkutano mkuu, sasa ni safari kwa kwenda mbele.

NAOMBA HUKU WAJIBU MASWALI YA WANANCHI YAKIWEMO NA KUJIBU TUHUMA WATAKAPO ULIZWA.

Hata hivyo kauli ya Dr. Slaa inawahusu inayowahusu wewe na wenzio hampo.
 
Hivi huyu mzee anatumia ulevi gani siku hizi? naona kichwa kinazidi kuvurugika kila kukicha.
 
Slaa anazeeka vibaya sana akalee kajukuu kake tu siasa haziwezi huyu
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

gamba wewe, utakuwa ni mmojawapo au unaenufaika na ufisadi...., huwezi badili nyekundu kuwa nyeusi,Magamba mmechokwa na watanzania wanahitaji mabadiliko.... ova
 
Slaa ni mfamaji aishi kutapatapa
Nyie nyote mnaompinga Rais wetu mtarajiawa Dr wa ukweli achana na hao Drs uchwala aka magumashi mbona hata hamzidi watatu? Hamuoni aibu tuuuuu??????
 
Nyie nyote mnaompinga Rais wetu mtarajiawa Dr wa ukweli achana na hao Drs uchwala aka magumashi mbona hata hamzidi watatu? Hamuoni aibu tuuuuu??????

Dr Babu Junior....hahaha Babu anazeeka vibaya sana mpka akina KIBANDA na MBOWE wamemwaga
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

Na hilo la ufisadi mnaloliona sio jipya, ambalo mnajua ndilo lililolata kuvuana magamba halitaisha na kama hamtalichukulia hatua litawatafuna slowly but completely. Huu si upepo haupiti. Kwani si kwa sababu ya ufisadi huduma za jamii ni mbovu?
 
Back
Top Bottom