Dk. Slaa: CCM kamwe hawatatuweza CHADEMA

Slaa bana,kwanini anapenda kudandia gari kwa mbele? Ccm kinafanya mambo yake, yeye anaibuka na matamko yake yasiyo na tija kwa taifa kwanini asifanye mambo yake kwa ustaarabu aheshimike? Poor slaa
 
Katiba mpya ithibiti wazee wanaoongea bila mpangilio
 
Kweli kinana anamnyima slaa usingizi,kila akistuka anamuona kwenye ndoto.viva kinana
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

DR KACHUJA? WEWE WA KUPIMA UNA KILA DALILI ZA UWENDAWAZIMU, WATANZANIA HATUTASAHAU TNATAKA MAJIBU YA KASHFA ZOTE ZA UFISAD O.W MTUPISHE MMEZIDI WIZI PIA KTUTIA UMASKINI, NYIE MNASHABIKIA TU NA AJAB ATA MAFISAD MNAWASIFIA, KWELI UKU KWETU AKINA NNAPE WAKIJA TUTAWAZOMEa
 
Kweli kinana anamnyima slaa usingizi,kila akistuka anamuona kwenye ndoto.viva kinana

WEWE LAZIMA UTAKUWA ZE KOMED, ATI UMEJIITA RUMNEY, AYA MAKUBWA, WE UNA KILA DALILI ZA UTAHAHIRA, WASEMA VIVA KINANA, IVI WAJUA KINANA NI JANGILI? WAJUA KUWA KINANA NDO MMILIKI WA ZILE PEMBE ZLOKAMATWA HONGKONG, WAJUA KUWA AMEUA TEMBO ZAID YA 50, SHABIKIA TU WEWE KICHWA MAJi
 
Kwa jinsi ninavyowajua watapuuzia, ni upepo tu,
 
Katiba mpya ithibiti wazee wanaoongea bila mpangilio

Ili muendelee kutuibia? Acha kulewa ufisadi wewe hatuwezi kufunga topic hii wakati mnaendelea kutuibia. Katika hili hata mkituua kama siyo Mungu hata Shetani atawachoma moto. We mtanzania wapi mwenye mawazo ya kifisadi namna hii?
 
Huwa napata shida kuelewa neno "Serikali" ninapoangalia (kwa tafsiri) mambo ya hili "genge (mob)" la JK linachofanya.

Hakuna nidhamu wala heshima kuanzia ikulu mpaka afisa wa mtaa. We are the most pitiable creatures on earth.
 
Sawa kabisa, wanataka tupotezee hoja ya ufisadi.

Hakuna kuipotezea, mpaka kieleweke!

Wawakamate mafisadi, wawashtaki, wafilisiwe, wafungwe kwa mujibu wa sheria.

Hatudanganyiki ng'o!!!
 
Tunataka utekelezaji wa vitendo, sio kuzunguka na kupiga siasa.
Serikali ya CCM imefilisika kimawazo na viongozi wa chama wamepanic.
Kwa ufupi CCM ni sawa na mbwa anayeenda haja na kula kinyesi chake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
CHADEMA imefilisika kimawazo na viongozi wake wamepanic ndiyo sababu wanafuatilia chochote kinachofanywa na CCM. Hivi hamna sera jamani? Badilisheni wimbo sasa.Kila siku CCM CCM CCM. Hamjui mnawapandisha chati? Ninyi ndio wauwaji wenu wenyewe. Time will tell, 2015 si mbali.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mpango wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo mawaziri kuanza ziara mikoani, hauwezi kukisaidia chama hicho kujiimarisha kisiasa wala kuathiri kasi ya Chadema ya kujipanua nchi nzima.
Chama hicho kimesema CCM hawatafanikiwa kwa kuwa zimejitokeza tuhuma nzito ambazo hazijajibiwa na serikali ya CCM kwa Watanzania na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali ya chama hicho.

Kauli hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kueleza kuwa Sekretarieti mpya ya Chama hicho inatarajia kuongozana na mawaziri kufanya ziara ya kichama mikoani kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
Nnauye alisema juzi kuwa katika ziara hiyo ambayo itaanza leo katika mikoa ya Mtwara, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, atakuwa akiambatana na baadhi ya mawaziri kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM tangu mwaka 2010.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema ziara hiyo haiwezi kukisaidia CCM kwa sababu hata mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara mikoani kuelezea utekelezaji wa bajeti ya kipindi hicho na bado hawakufanikiwa.

“CCM leo ndiyo wameamka, sisi Chadema kama ni kufanya ziara kila siku tupo mikoani, tunakumbuka mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara kama hiyo wakatumia fedha za walipa kodi Shilingi bilioni 2.5 na bado hawakufanikiwa, hawawezi kujibu hoja,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye wakati akizungumza na NIPASHE jana alikuwa njiani akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kichama, alisema CCM hawawezi kuwa na majibu ya kuwatosheleza Watanzania kutokana na kashfa na tuhuma kadhaa ambazo zimejitokeza kipindi hiki ambazo serikali yake imeshindwa kujibu na hivyo kuzua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Alitolea mfano mwaka 2007 wakati Chadema kilipowataja kwa majina baadhi ya viongozi wa serikali na CCM kwa tuhuma za ufisadi, lakini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria licha ya kuwapo kwa ushahidi wa kutosha ambao ungesaidia kuwatia hatiani.
Dk. Slaa alisema kashfa nyingine za hivi karibuni ambazo bado serikali ya CCM haijazijibu ni utoroshwaji wa meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.24 ambayo yalikamatwa na maofisa wa bandari ya Hong Kong.
Aliongeza kuwa kashfa nyingine ambazo Watanzania wanataka majibu ni usafirishaji wa wanyama hai akiwamo twiga kwenda nje ya nchi.

Dk. Slaa alisema CCM lazima itambue kuwa kikatiba kazi ya wapinzani ni kusema na serikaki kazi yake kubwa iwe ni kujibu hoja kwa vitendo kwa kutekeleza mambo yanayokuwa yanalalamikiwa.
“Wapinzani kazi yao ni kusema au kuisema serikali iliyopo madarakani, na serikali kwa upande wake inatakiwa kutekeleza mambo yanayolalamikiwa na nchi inaendelea kusonga mbele, lakini inashangaza unapoona serikali nayo inafanya propaganda za kisiasa, hii ni hatari,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kama serikali itaendelea kuzungumzia propaganda za kisiasa kwa kujibu kwa maneno wapinzani badala ya kutenda kwa vitendo, nchi itaendelea kurudi nyuma kimaendeleo na wananchi wataendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
“Watanzania wanataka kujua lini CCM na serikali yake watachukua hatua za dhati kukabiliana na ufisadi, CCM wasifikiri ajenda ya ufisadi itaishia hewani…hapana itakuwa ya kudumu hadi tutakapoona hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika,” alisema

Source:Nipashe Jumatano

- Ninaposoma mambo kama haya ya Dr. Slaa ninapata maswali mengi sana kuliko majibu, is this man ok? I mean ni majuzi tu Chadema ikiongozwa na yeye imeshindwa Viti vya Udiwani 22-5, halafu anasema CCM hatumuwezi, what planet is this man from?

- Halafu eti kuna mtu anashauri huyu awe na mdahalo na Kinana, on what? I mean huyu ni Mkurugenzi wa viwanda vya uongo ambaye anajua kwamba uongozi wake mbovu ndio umesababisha Chadema kushindwa uidiwani, lakini kwa vile Chadema hawana ubavu wa kuwambia ukweli kwamba hafai na ili kusahaulisha maumivu ya kushindwa kwao, leo anakuja na hizi nyepesi nyepesi, halafu eti Katibu Mkuu wa CCM ndio akaingie mdahalo na huyu Kiongozi loser!! aghhrrrrr!!

please somebody take me to another planet!!

Le Mutuz!!
 
Molemo
Juzi tu ulituletea thread jamvini ukimnukuu Dr. Slaa akimtaka Mwenyekiti wetu aache kuisema Chadema; nashangazwa na huyu babu yako yeye CCM haimtoki mdomoni hivi hana sera za kuwaeleza watanzania? au yeye ni ruksa kuisema CCM na mh. JK ni dhambi akiitaja Chadema? Yeye anahofu gani? kama ni tathmini ya kuona mafanikio ya ziara ya mawaziri tunaye mtu wa kufanya kazi hiyo!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mpango wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo mawaziri kuanza ziara mikoani, hauwezi kukisaidia chama hicho kujiimarisha kisiasa wala kuathiri kasi ya Chadema ya kujipanua nchi nzima.
Chama hicho kimesema CCM hawatafanikiwa kwa kuwa zimejitokeza tuhuma nzito ambazo hazijajibiwa na serikali ya CCM kwa Watanzania na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali ya chama hicho.

Kauli hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kueleza kuwa Sekretarieti mpya ya Chama hicho inatarajia kuongozana na mawaziri kufanya ziara ya kichama mikoani kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
Nnauye alisema juzi kuwa katika ziara hiyo ambayo itaanza leo katika mikoa ya Mtwara, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, atakuwa akiambatana na baadhi ya mawaziri kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM tangu mwaka 2010.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema ziara hiyo haiwezi kukisaidia CCM kwa sababu hata mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara mikoani kuelezea utekelezaji wa bajeti ya kipindi hicho na bado hawakufanikiwa.

“CCM leo ndiyo wameamka, sisi Chadema kama ni kufanya ziara kila siku tupo mikoani, tunakumbuka mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara kama hiyo wakatumia fedha za walipa kodi Shilingi bilioni 2.5 na bado hawakufanikiwa, hawawezi kujibu hoja,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye wakati akizungumza na NIPASHE jana alikuwa njiani akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kichama, alisema CCM hawawezi kuwa na majibu ya kuwatosheleza Watanzania kutokana na kashfa na tuhuma kadhaa ambazo zimejitokeza kipindi hiki ambazo serikali yake imeshindwa kujibu na hivyo kuzua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Alitolea mfano mwaka 2007 wakati Chadema kilipowataja kwa majina baadhi ya viongozi wa serikali na CCM kwa tuhuma za ufisadi, lakini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria licha ya kuwapo kwa ushahidi wa kutosha ambao ungesaidia kuwatia hatiani.
Dk. Slaa alisema kashfa nyingine za hivi karibuni ambazo bado serikali ya CCM haijazijibu ni utoroshwaji wa meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.24 ambayo yalikamatwa na maofisa wa bandari ya Hong Kong.
Aliongeza kuwa kashfa nyingine ambazo Watanzania wanataka majibu ni usafirishaji wa wanyama hai akiwamo twiga kwenda nje ya nchi.

Dk. Slaa alisema CCM lazima itambue kuwa kikatiba kazi ya wapinzani ni kusema na serikaki kazi yake kubwa iwe ni kujibu hoja kwa vitendo kwa kutekeleza mambo yanayokuwa yanalalamikiwa.
“Wapinzani kazi yao ni kusema au kuisema serikali iliyopo madarakani, na serikali kwa upande wake inatakiwa kutekeleza mambo yanayolalamikiwa na nchi inaendelea kusonga mbele, lakini inashangaza unapoona serikali nayo inafanya propaganda za kisiasa, hii ni hatari,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kama serikali itaendelea kuzungumzia propaganda za kisiasa kwa kujibu kwa maneno wapinzani badala ya kutenda kwa vitendo, nchi itaendelea kurudi nyuma kimaendeleo na wananchi wataendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
“Watanzania wanataka kujua lini CCM na serikali yake watachukua hatua za dhati kukabiliana na ufisadi, CCM wasifikiri ajenda ya ufisadi itaishia hewani…hapana itakuwa ya kudumu hadi tutakapoona hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika,” alisema

Source:Nipashe Jumatano

- Absalom Kibanda, my good and close friend, ni wa kumsamehe cause yeye anaajiriwa na Gazeti la Mbowe, Tanzania Daima ambalo mission yake inafahamika ya kuitukana CCM kila kukicha so is wafanyakazi wote wa Mbowe wanajulikana kuwa moja ya masharti ya kulipwa ujira wao ni kuitukana CCM at any cost, sasa ningeshangaaa sana asingemuogopa KAtibu Mkuu Mpya wa timu ya ushindi, hasa baada ya KAtibu asiyemuogopa kuongoza Chadema kwenye kushindwa Udiwani!!

- Absalom ni wakati mufaka sasa kutangaza conflict of interest, maana huwezi kuajiriwa na Mbowe halafu ukawa objective inapokuja ishus za CCM!!

Le Mutuz!!
 
Huyu SLAA mbona kazi yake ni kufuatilia tu CCM? CCM wao wamesema KINANA anafuatana na mawaziri kukagua shughuli za maendeleo, yeye anakuja na hoja kuwa CCM haitawaweza, kwani CCM wanakwenda kwenye kampeni au kukagua miradi ya maendeleo? SLAA aache kumuogopa KINANA na kuanza kuomba msaada wa wananchi kwa propaganda zake.
Wewe ulitaka awafuatilie Cuf? au TLP?
 
Ccm ijibu hoja za wapinzani kwa kuleta maisha bora kwa watanzania na siyo wanapiga maneno kama vile nao ni wapinzani. A j a b u u u u u . Toa majibu kwa maswali uliyoulizwa. Mfano;- twiga hai, meno ya tembo, madini, bandarini, nk.
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

sijajua kama upo kwenye udini au siasa..kama siasa ni hivi swala la ufisadi haliwezi kuisha sababu ni kansa inayouwa watz..hatutaach a kusema ufisadi maana umetuzunguka wakati huo huo ni adui wa 1..
 
Back
Top Bottom