Dk.Slaa apata wakati mgumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk.Slaa apata wakati mgumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Oct 10, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Dk.Slaa apata wakati mgumu
  Na Muhibu Said  10th October 2010
  [​IMG] Aliyemnadi kwa Chadema akataliwa
  [​IMG] Aambiwa chaguo ni NCCR-Mageuzi
  [​IMG] Ni yale yale yaliyomkuta kule Kyela  [​IMG]
  Dk. Willibrod Slaa


  Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amepata wakati mgumu kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama hicho, Muslim Hassanali, baada wananchi wote mkutanoni kumueleza kinagaubaga kuwa watakayemchagua ni mgombea kupitia NCCR- Mageuzi jimboni humo, David Kafulila.
  Kafulila kabla ya kujiunga na NCCR-Mageuzi, alikuwa ni Afisa Habari wa Chadema makao makuu jijini Dar es Salaam.
  Hali hiyo ilimkuta Dk. Slaa juzi baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni zake za kuusaka urais wa Jamhuri ya Muungano katika eneo la Uvinza, lililopo Wilaya mpya ya Uvinza, mkoani hapa.
  Baada ya kuhutubia mkutano huo, Dk. Slaa alimsimamisha Muslim karibu na meza aliyotumia kuhutubia na kuwauliza wananchi waliokwenda kumsikiliza kuwa ni wangapi watampigia kura Kafulila.
  Alipouliza hivyo, uwanja mzima walinyoosha juu mikono kuashiria kwamba, watamchagua Kafulila.
  Mara ya pili Dk. Slaa aliuliza ni wangapi watampigia kura Muslim, wakanyoosha juu mikono watu wachache.
  Dk. Slaa aliuliza mara ya tatu kuwa ni wangapi watampigia kura yeye (Dk. Slaa), uwanja mzima wakanyoosha juu mikono.
  “Naona kura ya urais ipo, lakini huku (anaonyesha kwa Muslim) hakuna,” alisema Dk. Slaa na kujibiwa kwa msisitizo na wananchi hao kuwa: “Tunaye mtu wetu, Kafulila.”
  Hali hiyo ilimfanya Dk. Slaa kueleza mkutanoni hapo kuwa anazo taarifa kwamba, Kafulila aliwahi kutamka akiwa katika Kijiji cha Nguruka, wilayani humo kuwa anaungwa mkono na mgombea ubunge kupitia Chadema Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
  Kutokana na hali hiyo, Dk. Slaa alisema atampeleka Zitto eneo hilo kisha amuulize amtake mbele yao athibitishe madai hayo ya Kafulila kama ni ya kweli.
  Hali kama hiyo iliwahi kumkuta Dk. Slaa baada ya wananchi wa Jimbo la Kyela, kumkataa mbele yake mgombea wa Chadema, Ado Makata na kumweleza kuwa wanayemtaka ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimboni humo, Dk. Harrison Mwakyembe.
  Awali, Dk. Slaa aliwaahidi wananchi hao kuwa iwapo watampa ridhaa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu na kuingia madarakani, atashughulikia haki za waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha chumvi cha Uvinza ili kutatua mgogoro wa muda mrefu uliopo kati yao na serikali baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa.
  Alisema anafahamu kuwa kiwanda hicho kilikuwa ni mali ya serikali, lakini imeamua kufumba macho na kuziba masikio kuhusu kulipa haki za wafanyakazi hao licha ya wabunge kulipigia sana kelele suala hilo bungeni.
  “Mkinipa ridhaa tutalichukua kwani haki za wafanyakazi haziwezi kupotea,” alisema Dk. Slaa.
  Pia aliahidi kushughulikia tatizo la uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uendeshaji wa kiwanda hicho kutokana na kutumia nishati ya kuni kwa wingi.
  Jambo lingine aliloahidi kulishughulikia iwapo ataingia madarakani, ni kero ya upatikanaji wa umeme wa uhakika mkoani hapa.
  Alisema atashughulikia tatizo hilo, baada ya serikali kushindwa kulipatia ufumbuzi kwa visingizio mbalimbali, ikiwamo madai ya kugundulika kwa vyura katika Mto Malagarasi uliotarajiwa kuzalisha nishati hiyo.
  “Hoja hiyo ina utata, kwani vyura hao wamegundulika baada ya fedha kupatikana. Kama kweli vyura hao wapo, je, hatima ya wana Kigoma kupata umeme ni ipi,” alihoji Dk. Slaa.
  Alisema kinachomsikitisha ni kauli ya serikali kwamba, umeme wa uhakika mkoani hapa ulikuwa unatafutwa kwa njia mbili, ikiwamo ya reli ya uhakika na kusema hana uhakika kama serikali imedhamiria kuwakomboa wana Kigoma.
  Kutokana na hali hiyo, alisema atakapoingia madarakani, atafanya kila linalowezekana kuitafutia ufumbuzi kero hiyo kwa vile Kigoma ni sehemu ya Tanzania.
  Alisema mkoa wa Kigoma umebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa, ambao ungetumika vizuri ungeweza kuzalisha chakula na kulisha Tanzania nzima, lakini haujapewa kipaumbe.
  Leo Dk. Slaa anatarajiwa kuendelea na mikutano yale ya kampeni katika Jimbo la Kigoma Kaskazini na majimbo ya Buyungu na Muhambwe, baada ya kufanya mikutano hiyo katika majimbo ya Kasulu na Kigoma Mjini, mkoani hapa, na kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Rukwa juzi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama alikuwa hafamu ni nani anapendwa kwenye Kugombea ubunge wa jimbo hilo.

  Anafahamu wazi kabisa kuwa hali iko hivyo. Ila anaaingia kwa gia ya "mimi ninataka hivi......."

  Wananchi wanamwambia "sisi tunataka hivi, na sisi ndiyo wapiga kura......."

  Yeye anamaliza kwa kusema "mie ni msikivu wa Wananchi wa Tanzania, nipo hapa ili nikutumikieni na si kuwatawala. Ridhaa yenu ndiyo AMRI kwangu na nitafuata na kuheshimu maamuzi yenu........."

  Mkutano unaisha kwa MAKUBALIANO na wananchi wanakuwa WAMEFURAHI kuwa kwenye mechi ya leo, WAMEMFUNGA goli Slaa. Ila pia wanaona kuwa ni mtu mwenzao kama wao kwani HABISHI tu ila anajadiliana nao na kufikia maamuzi. Cha muhimu ni kuwa mwisho wa siku, hata Wana Kigoma, Kyela nk wanaona kuwa si mtu wa kuhutubia tu na anaondoka, ila pia anasikiliza wananchi wanataka nini na kukubaliana nao.

  Kikwete yamekuwa yakimkuta hayo. Ila kwa kuwa analipa watu kwenye mikutano ili wamshangilie, hilo huwa halionekani. Sehemu alizohutubia huku watu wameweka bendera za Chadema na wakimuonyesha vidole viwili, ilibidi awe na busara na kukubaliana nao kwa kusema "ok, mbunge wenu ila Urais kwangu". Yeye hafanyi hivyo. Slaa anakubali iwe hivyo na mwisho wa siku utaona kuwa karibu woote watamchagua Slaa na mbunge watampa wanayemtaka.

  Hili jambo ni JAMBO la kujivunia saana hasa hiyo mikoa kwani wameshaanza kuona mbali kwa wao wenyewe kuchagua MBUNGE wao wanayemtaka na kumchagua RAIS wao wanayemtaka na si CHAMA kama ambavyo CCM na baadhi ya MIJINGA inavyotaka iwe. Hii ndiyo DEMOKRASIA katika hali ya juu.................
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  David Kafulila ni mpiganaji naamini atapita, bila shaka Chadema watamkubali mbunge wa NCCR Mageuzi.
   
Loading...