Dk Slaa ang’ara urais; NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa ang’ara urais; NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 4, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 03 August 2011 23:11 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.

  Leon Bahati

  MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.

  Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.

  Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.

  Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: “Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?”

  Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

  CCM wamtaka Dk Slaa
  Utafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.

  Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.

  Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).
  Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.

  Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.

  Mgombea urais CCM 2015
  Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.

  Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).

  Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.

  Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

  Uvuaji gamba CCM
  Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.

  Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.

  Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.

  Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.

  Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.

  Kero kubwa nchini
  Asilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).

  Katiba Mpya
  Miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).

  Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.
  Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  DR. Slaa ndiye Rais wa nchi hii, mtetezi wa wanyonge.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ubaya ni Vigogo wa CCM wanauchumi wa nchi hii...
  Wanaiba kila kona, but hey kuna Mahakama za kimataifa CCM ikiondoka wajichunge, pesa zote zitapatikana...
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Cha kushangaza ni kwa nini EL hayumo. Au alipata sifuri? Lakini kama kutokuwemo kwake hakuulezwi vizuri basi hii yote ni changa la macho.

  Hata hivyo nakubali Dr Slaa ndiye Rais ajaye -- iwapo CCM ina nia ya kuendelea kuwapo kwa amani nchini.
   
 5. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo kila mtu analijua ya kwamba Dr. Slaa ni Rais wa nchi hii hata leo, kwa hiyo taarifa hiyo ya synovate imechelewa mno.
   
 6. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  viva tanzania viva
   
 7. M

  Makirikiri Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  EL yupo kapata 3% kati ya walengwa wa ccm.. soma mwananchi uk.wa 4. EL kabwagwa na Pinda, magufuli,membe,na sita
   
 8. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hizo takwimu sio za kisiasa kweli?? Synovet wanazuga tu kwenye suala la urais ili kuvimbisha kichwa wapinzani, ningewaona wa maana kama mngeuliza kwenye uchaguzi uliopita wangapi walimpigia kura Jk, kuhusu katiba mpya na kujivua gamba kwa wana magamba imekuja right time..thanx.!
   
 9. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Yangu macho ila mjue kuna watu wanasomea saikologia na kuna vita ya kisaikolojia.
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hawa Synovate wameconduct wapi huu utafiti wao?
  Mbona hata wakati wa uchaguzi mwaka jana Dr. Slaa alimpiku Kikwete isipokuwa wao walichakachua matokeo kumfavor JK?
  Hizo asilimia walizoonyesha bado ni ndogo sana, Dr. Slaa anazaidi ya 80% siyo 42%.
  Dr. Slaa anaendelea kuongoza nchi hii kutoka kwenye mioyo ya wananchi wapenda maendeleo. actually huyu ndiye rais wangu.
   
 11. T

  Tekenya Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashangaa sana hivi kwa nin wasingepambanisha wagombea walopita pekee? pinda na dr slaa wanakujaje? sio saizi yake, wangempambanisha Dr Slaa, Kikwete, Ibrahim Lipumba etc.
  mpmbano mwingine labda wangeainisha nafas ya urais kwa ccm uchaguzi ujao.
  kikwete hajamaliza mda wake, na point hapa je kama uchaguzi utarudiwa leo nan atashinda?
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  inawezekana kwenye utafiti wao waliwapambanisha Kikwete akapata sifuri, wameona aibu kudisclose
   
 13. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Swali muhimu sana, au hakuwekwa kwenye list ya wagombea?
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Upuuzi mtupu! Dr. W. Slaa alishinda uchaguzi uliopita kwa kuchaguliwa na wananchi wengi. Na hao watafiti wanajua maana walifanya utafiti kabla ya uchaguzi na matokeo yalikuwa hvhv. Sasa wanaenda kuwauliza tena leo, walitegemea majibu tofauti!? Wakati wa uchaguzi waliambiwa watoe matokeo ya tafiti zao wakakataa kabisa kwakuwa Dr. Slaa alionekana mshindi. Leo wanatuletea unafiki tu hapa!
   
 15. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa ni wanafiki pamoja na utafiti wao , uchaguzi umeisha sasa ndio wanatuletea matokeo!!
   
 16. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  sinoveti is another joke!
   
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Doctor Slaa my President 100% not 42%.
   
 18. WISTON MWINUKA

  WISTON MWINUKA Member

  #18
  Jan 26, 2013
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu zangu wa Tanzania na wana Jf wenzangu,kwanza kabisa poleni kwa pirikapirika na mikikimikiki ya maisha ndani ya nchi yetu.Yote heri,Leo naomba kwa pamoja tujaribu kuitafakari kwa mtazamo wa kisiasa hali ya nchi yetu,Je!kama uchaguzi mkuu ungefanyika leo hali ya matokeo kiasilimia ingekuwaje?CCM,CUF,TLP,NCCR,CHADEMA,nakadharika ingekuwaje?.Mawazo hayo ya kuchangia hapa italeta taswira ya nani atashinda kwa kishindo 2015.Karibuni kwa maoni.
   
 19. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2013
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hatuna tume huru ya uchaguzi, uchakachuzi wa matokeo bado ni tatizo sugu na pia uelewa wa baadhi ya wananchi bado ni mdogo. Kwa hiyo mambo yanaweza kuwa yale yale tu na MaCCM yakashinda.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huwezi kutoa majibu ya maswali hayo kwa kutumia intuition tu, inahitajika research.
  Go to the field and find answers not here on internet, cause here you dont get "representative population".
   
Loading...