Dk Slaa amshukia JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa amshukia JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 6, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  ASEMA MAMBO MAZITO YANATATULIWA KISIASA, MAFISADI WA EPA WANATAMBA
  [​IMG]

  Leon Bahati

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa ametoa tathmini ya mwaka mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipoingia kuongoza nchi katika ngwe ya pili, na kusema mkuu huyo wa nchi ameshindwa kutatua mambo mengi mazito yanayohusu uchumi na maisha ya Watanzania.Akitoa tathimini hiyo jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa aliorodhesha baadhi ya matukio aliyoita ya kuhujumu uchumi wa nchi pamoja na athari mbalimbali za maisha ya Watanzania.

  Dk Slaa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi aliangushwa na Rais Kikwete, alisema wakati matatizo hayo yakionekana kuathiri uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania, bado utatuzi wake umekuwa ni wa kisiasa, usiozingatia utaalamu.

  Alifafanua kwamba udhaifu katika kukabiliana na matatizo hayo ya kiuchumi, umezidi kuongeza ugumu wa maisha kwa watu wa kipato cha chini huku neema ikielekezwa kwa wachache, wakiwamo watuhumiwa wa ufisadi ambao pamoja na kuwapo na ushahidi wa kuwashitaki, wamekuwa wakikingiwa kifua.

  "Tumesikitishwa na hali tete na mwelekeo mbovu wa uchumi wa nchi yetu na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi kunakoendelea kusababishwa pamoja na mambo mengine, mfumuko wa bei na thamani ya shilingi kutokuwa imara. Hali hii siyo tu ni tishio kwa maisha ya wananchi bali pia kwa usalama wa nchi kwa ujumla," alisema Dk Slaa.

  Alisema hata hotuba ya mwaka mpya aliyotoa Rais Kikwete, alishindwa kueleza hatua thabiti na za haraka za Serikali katika kukabiliana na hali mbaya na uchumi.

  "Badala yake aliendelea na utaratibu uleule wa hotuba zake za kuorodhesha visingizio vya nje vya uchumi wa dunia bila kuweka mkazo katika kuelekeza hatua za kuinua uchumi wa ndani pamoja na kulinda wananchi dhidi ya misukosuko ya nje," alilalamika Dk Slaa.

  Huku akisisitiza kuwa ana nakala ya hotuba ya Rais Kikwete na ameisoma kwa makini, alisema siyo kweli kwamba hali ya mbaya ya uchumi imesababishwa na tatizo la uchumi wa dunia kama alivyosema mkuu huyo wa nchi, bali ni uzembe unaotokana na watendaji wake.

  Kutokana na Chadema kutoridhika na hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyopo nchini kwa sasa, Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho imeitisha kikao kitakachofanyika Januari 22, mwaka huu kuangalia njia za kuchukua kuwalinda Watanzania.

  Alisema matatizo yote ya kiuchumi yatajadiliwa na kufanya uamuzi wa hatua muafaka za kuchukua, ili kusimamia uwajibikaji wa Serikali kwa maslahi ya umma.

  Mtendaji mkuu huyo wa Chadema, alisema kwa sasa hali inaonekana kuwa Serikali inatatua matatizo ya nchi kisiasa zaidi kuliko kutumia wataalamu wake katika kuweka mikakati imara iliyobuniwa kisayansi.

  Alitoa mfano kwamba, uhaba wa sukari unaolikumba taifa kwa sasa hauwezi kutatuliwa kwa kununua sukari nje na kuitoa kwa mgawo kwani kunaongeza tatizo badala ya kuliondoa.

  Dk Slaa alidai kwamba ana vielelezo vingi vya siri vinavyohusu Serikali, na kwamba utawala wa Rais Kikwete unaogopa kusema ukweli kuhusu sababu zinazosababisha uchumi wa nchi kudorora huku gharama za maisha zikipanda kila kukicha.

  Alifafanua kwamba Serikali inashindwa kueleza ukweli wananchi kuhusu, "Hali mbaya ya kifedha ambayo inalikabili Taifa hivi sasa kwa kupungua kwa mapato ya ndani na nje, ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa."

  Dk Slaa alisema Serikali imeshindwa kueleza mpango wake wa kuongeza uzalishaji na kupunguza matumizi yake.

  Alionya kwamba, baadhi ya viongozi wa Serikali wameendelea kujineemesha kwa kujiongezea malipo huku wakizidi kuongeza bei ya huduma za msingi, zinazotolewa na taasisi zake.

  Ingawa Dk Slaa hakuweka wazi suala hilo, lakini nyongeza ya posho za wabunge kwa sasa zimekuwa zikitikisa taifa. Posho za vikao za wabunge ziliongezeka kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku kwa kigezo cha kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma.

  Dk Slaa alirejea kuonya, "Hali hii ikiachwa iendelee itakuza pengo la wenye nacho na wasio nacho katika taifa na wakati huo huo itaongeza zaidi gharama za maisha kwa wananchi hususani wa kipato cha chini, tofauti na ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania."

  Ufisadi
  Dk Slaa alisema Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia matatizo ya ufisadi, ambayo yamelikabili taifa na kusababisha mabilioni ya fedha za umma kuchukuliwa na wachache.

  Alisema licha ya watuhumiwa kufahamika wazi na kwamba chama hicho kiliwatangaza hadharani, hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

  Alisema Sh70.7 bilioni zilizorejeshwa na waliozichota kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), hadi sasa hazijulikani zilikoenda jambo ambalo tayari taasisi za kimataifa zimeingilia kati na kuitaka Serikali itoe maelezo.

  Dk Slaa alisema Watanzania wengi, wakiwepo waandishi wa habari wanaelekea kusahau sakata la marejesho ya fedha za EPA, lakini mataifa yanayochangia bajeti ya Serikali wamekuwa wakihoji suala hilo.

  Alisema ana barua iliyoandikwa kwa Serikali ikihoji ziliko fedha hizo ambazo ni sawa na asilimia 54 ya fedha zote zilizochotwa kwenye akaunti hiyo ya EPA, mwaka 2004/05.

  Katika kuthibitisha kwamba Serikali imekuwa ikiwakingia kifua watuhumiwa wa ufisadi ili wasichukuliwe hatua, alitoa mfano chama chake kiliwasilisha kwa Mkurugezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ushahidi dhidi ya mtuhumiwa wa ufisadi wa ununuzi wa rada.

  Kwenye ushahidi huo ambao uliambatanishwa na vielelezo vya uchunguzi wa Taasisi ya Uingereza ya Kuchunguza Makosa ya Jinai (SFO), Dk Slaa alisema zilionyesha jinsi mtuhumiwa alivyojipatia Sh1 bilioni na kuziweka kwenye akaunti nchi za nje.

  Alisema hali hiyo inashangaza kwani watu wa kawaida wanaotenda makosa hata kwa kuhisiwa tu wanakamatwa na kupelekwa mahabusu kabla ya kufikishwa mahakamani, lakini vigogo wa Serikali wanaonekana kulindwa.

  Dk Slaa alisema wananchi wanataabika kutokana na migogoro mbalimbali ikiwepo ya ardhi, elimu, afya na maji.

  Alisema migogoro hiyo inashindwa kutatuliwa kwa sababu badala ya kushughulikia chanzo, Serikali imekuwa ikitafuta ufumbuzi wa matokeo yake.

  Dk Slaa alitoa mfano wa migogoro hiyo ya ardhi kuwa ni ile kati ya wananchi na wawekezaji, wakulima na wafugaji na ile ambayo Serikali yenyewe imejikuta ikipambana na raia wake.

  Migogoro mingine, alisema ni ya wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini akasema tayari amewasiliana na Umoja wa Vijana wa chama hicho (Bavicha) kufuatilia kwa ukaribu suala hilo ili kuweka wazi hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa.


  Source:
  Mwananchi
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Hali ni mbaya kwakweli!

  Jana nilikuwa maeneo ya tegeta kutokana mwezi huu kuwa dume plus nikasema nikanunue dagaa wa kutosha kuongeza ujazo nyumbani, Loh! Kuuliza kilo ya dagaa shilingi ngapi, nikaambiwa sh 5,000! Nikamwambia muuzaji sitaki wa kigoma (najua huwa wana bei kidogo) nataka wa Mwanza akasisitiza ndio bei yake! Nikachoka kwakweli! Dagaa kilo sh 5,000?

  Sisi Watanzania tutaiona pepo kwa uvumilivu wetu!
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nakukubali sana DR na ndio maana unamkubali EL kuwa ni mtendaji.
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ni tathmini nzuri sana kutoka kwa Slaa.tatizo serikali yetu sio sikivu kama inavyojidai
   
 5. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Ukweli ni kwamba Tz muda si mrefu itakuwa failed state kama zilivyo afghanistan na somalia. Haileti akilini kwamba bei za vyakula zinapanda tu kila siku halafu watu kipato ni kile kile. Itafika muda uzezeta wa watz hautahimili vishindo vya njaa na ugumu wa maisha.
   
 6. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ila Slaa nae kazidi kulalamika! Ila yeye mshahara wake amesahau? mbona sijawhi kusikia amesaidia hata mbuzi kwa ajili ya sikukuu kama mzee wa kaya JK? YEYE ZAKE ANAWEKA MFUKONI ANATULIA HALAFU ANAWANYOSHEA WENZIE KIDOLE! SIASA BWANA KAMCHEZO KACHAFU SANA!:lol:
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,678
  Trophy Points: 280
  Serikali yenye kiburi.
   
 8. p

  pilu JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani yote hayo jk atakua anayajua coz yanatoka kambini mwake,ila ninacho amini kwa sasa jk anahamu muda wake wa uprezdent uishe akapumzike zake,sababu mambo mengi yanayoendelea yeye si rahisi kuyatolea uamuzi kutokana na ukweli kwamba wengi walofanya madudu ni watu muhimu'sana' kwake,mifano ya watu hao ipo mingi tu wote twajua!

  FUNZO: Tuache kuchagua marafiki katika sehemu nyeti kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu, kwani marafiki wanapovurunda utawaonea aibu kuwaadhibu!
   
 9. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa namna yako ya kufikiri, Tanzania ina safari ndefu ya kufika kwenye mabadiliko.

  1. Hivi kwako wewe umahiri wa kiongozi na uadilifu wake ni kununua mbuzi kwa hela yake na kugawia watoto yatima vituoni au?

  2. Katika mambo yoote yaliyozungumziwa, wewe hujaona la maana kwa hiyo ulichokiona ni kama 'Dr.Slaa analalamikia mambo yake binafsi kwa kuwa anamuonea wivu JK' au?

  3. Kwa akili yako Dr.Slaa alikuwa anazungumzia mishahara pale au?

  4. Kwa hiyo kwako wewe (sijui ni mwanamke au kitu gani), Dr.Slaa hapaswi kuzungumzia wizi kwa kuwa mshahara wake hanunui mbuzi na kugawa mitaani?

  Kweli tuna safari ndefu. Kama haya ndio mawazo yako sijui ni wangapi wako kama wewe. Yaani ukisikia 'ulofa' ndio huu. Mbuzi na tuzawadi tudogo tudogo ndio tuna-justify madudu ya mtu na kumtakasa awe malaika mbele yako. Kuna maneno ningekwambia lkn nimesikia hapa kuna kakitu kanaitwa 'BAN', lkn we jua kuwa you are very disappointing. Na kwa akili za watu kama wewe, wanawake wanadharaulika.
   
 10. p

  pilu JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ongea mambo ya kimsingi mkuu, zawadi za sikuku zitasaidia bei kushuka? Zitasaidia wanafunzi kupata mikopo? Zita saidia umeme, maji na ajira kuwapo?
  Wewe waona hizo zawadi za msimu ni muhimu sana kwa wa Tz, acha kuwa na fikra fupi kama meno yako!
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mbona anaongelea mambo yaliyopita au kujirudisha kwenye chati maana ameporomoka kweli kweli.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  itabidi tuombe kukutana na rais ikulu kama ilivyokuwa kwenye issue ya katiba ili DR naye apate fursa ya kunywa juice ya magogoni
   
 13. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hongera Dr Slaa kwa tathmini nzuri ingependeza ukawa na utaratibu wa kujibu hotuba za kila mwezi za rais ili kuondoa upotoshaji unaoweza kujitokeza.
   
 14. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii serikali inahitaji msaada wa kiroho kwani ina pepo la kutojua nini cha kufanya. Sometime last year, Zitto Kabwe alisema serikali imefilisika kiasi haina fedha za kulipa mishahara, Mkulo akaja juu na kuleta maneno meengi ya vitisho. Sasa jana Naibu waziri wa Afya kamwaga mambo hadharani bila kujua anatoa siri.

  Mimi siwashangai sana viongozi wa CCM kwani wao wanachokiwinda wanakipata na familia zao zinaneemeka. Shida yangu ipo kwa ndugu zangu VIBARAKA NJAA WA CCM.

  Hivi watu wameiba FEDHA ZA EPA, kibao, wameshtukiwa, badala ya kupelekwa mahakamani wameambiwa warudishe. Baada ya kurudisha bado fedha hizo hizo (chache manake sio zote) bado hazijulikani zilipo. Huku sio kuchezeana? Hivi ikifikia sehemu tukapigana kwa ajili ya kutoridhika na haya mambo, tutasema ni CDM ndio wameanzisha vurugu?

  Nyie ndugu zetu mnaoshabikia magamba, tutumie akili jamani. Tanzania inatuhitaji kwa ujumla wetu. Kama haya yatakuwa ya Dr.Slaa peke yake tutakuwa tunatawazwa mpka lini ilhali tumekuwa wakubwa na mikono tunayo? Tuupinge ufisadi huu kwa kura. Bunge likihodhiwa na CCM haya ndio madhara yake wajamini tuamke, mbona tunajinafiki wenyewe?
   
 15. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hayo ni mawazo yangu toa yako, ktk siasa za tanzania usitegemee mwanasiasa alete maendeleo, wote ni wachumia matumbo tu, nimetoa mfano tu kwa dr slaa kuhusu mshahara wake, ila kwa sababu humu watu ni washabiki wa chadema hawakubali kuambiwa ukweli. Chadema wanaongoza majimbo mangapi na wamefanya nini pale? Usikurupuke kunishambulia hata mie haya ni mawazo yangu, toa yako tambaa mbele!
   
 16. p

  pilu JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole mkuu kwa mshahara wa dr.slaa kukupa mawazo,

  pia natiashaka na wewe kama mpaka sasa hujaona impact za chadema katika maendeleo ya tz, kwani upo hapa hapa tz mkuu?
   
 17. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ina maana we Jakubumba na ukubwa wako wooote huo. Ukiona Mbuzi na Mchele na vitu vingine vinatolewa na Rais kwa ajili ya sherehe ama sikukuu unajua ametoa pesa yake mfukoni...?? Vingine hata hajui nani kanunua yeye ni kama mzinduaji tu wa hafla gharama hazimuhusu...........! So fanya tafiti kabla ya kuanza kuropoka humu kwa wakubwa wenzako !
   
 18. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yaani mkuu huyo mwanamke kanichefua haijawahi kutokea mwaka huu. Yaani sijui watu wengine wameumbwaje. Watu wako kwenye ishu serious, wao wanaongea habari za KUHONGWA. Hivi tutaishi kweli kwa kuchekacheka tukipewa mbuzi? Inaelekea Dr.Slaa angejipapasa mifukoni akamnunulia huyu (kidemu mpenda kuhongwa) wanja na poda basi angemuona ndio anafaa.

  Ni kwa sababu hii kina Plato na Aristotle waliweka azimio la enzi zao kwa wanawake wasipige kura. Amini nakuambia, wkt wa uchaguzi wapo waliompigia kura 'Dokta wa Msoga' kwa kuwa wanaamini kuwa ana sura nzuri. Yaani mustakabali wa nchi unaamuliwa na watu wasiojua nini wanahitaji ktk maisha.

  Tuwe serious Watanzania, hivi mtu wa akili hizi unaweza umkubali awe business partner wako kama kweli unataka biashara ikue. Tena cha kushangaza kwenye signature yake ameandika
  kuna uchangudoa mwingine zaidi ya kuomba viongozi wakununulie mbuzi siku za sikukuu?

  Wewe JAKUBUMBA nenda MMU ukajadiliane kule. Zipo mada nyingi tu nzuri za saizi yako:
  1. Mpenzi wangu simuelewi
  2. Kwa nini wanaume wengi hawajui kukea
  3. Hivi mwanaume asipokupa zawadi kilisimasi ni kweli anakupenda?
  4. Mpenzi wangu kaniacha je akirudi nimkubalie?
  Nafikiri mada za namna hii ndio unaweza kuzijadili kwani ni hisia na sio akili.
   
 19. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Big up mkuu, hiyo ni tathmini nzuri sana, nawashangaa watu wanaoleta ushabiki kwenye ishu muhimu kama hiyo.KATIKATI endelea na ushabiki wako lakini kumbuka watu wanataabika kutokana na uongozi mbovu uliopo madarakani.
   
 20. d

  demokrasia Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nahisi wewe utakuwa ni kula kulala ndio maana huyajui matatizo ya nchi yako. Nasikitika kuwa hujui hata wajibu wa Kiongozi kwa Wananchi waliomchagua. Naomba nikuelimishe kuwa, hatuchagui Rais kwa ajili ya kununua mbuzi wa sikukuu. Tunachagua Rais ili asimamie ipasavyo uchumi na maendeleo ya nchi.
   
Loading...