Dk. Shein ataka usawa mambo ya Muungano

Dk. Shein ataka usawa mambo ya Muungano

2019 uchaguzi wa serikali za mitaa
2020 uchaguzi mkuu,
Naamini haya yote yatajibiwa na wazenji + Shein
 
Wezi wakubwa jengo moja bilion 7 wakati sisi yakwetu 20 tumetumia bilion 10 ujinga hatupendi
 
tunavyofahamu sisi unaposema serikali ya muungano maana yake ni serikali ya Tanganyika yaani bara kwa hiyo lazima serikali ya bara ipate mara mbili ya serikali ya Zanzibar
 
Idadi ya wazanzibar haizidi milioni 2 na Tanzania bara milioni 50 usawa upo wapi?
 
Hahaha kwani Tanganyika na Zanzibar ni watoto mapacha?! Hata tarehe za kuzaliwa ziko tofauti tutapewaje sawa?! Hahaha serikali inahamia dodoma sasa hilo nalo tuwe sawa sijui wao watahamia wapi au nao wanataka kwenda Dodoma?! Au Zanzibar nayo inataka Bombadier?! Lakini Bombadier bila makinikia hahaha hata haipendezi hahaha. Huyo rais aangalie Magufuli asije mtumbua kama yeye Shein alivyomtumbua mwanasheria mkuu wa Zanzibar kwa kudai, hahaha alianza hivyohivyo.
Kashtuka tukihamia dodoma, magogoni hatukuwepo mtu nauli itapanda hadi dodoma duh shida. Wampe magogoni tukihamia dodoma apunguze hasira.
Lakini waziri wa muungano yupo angempelekea malalamiko yake, walisema chama kina vikao v ya kusikiliza malalamiko kwanini yeye kasema hadharani na juzi tu katoka kwenye mkutano mkuu wa chama na wahusika wote walikuwepo?!
 
añyamaze huko Tanganyika ndo imemuweka ikulu, akizingua anashushwa!!

by the way tumewabeba sana hawa waswahili, ni wabaguzi kinyamaa,
 
Kama tunaendelea na muungano ambapo rais wa Tanzania bara ndiyo anakuwa rais wa serikali ya muungano, kamwe hapatakuwa na usawa wa pande mbili za muungano. Tanzania bara kwa wingi wao wataendelea kuwa na turufu kwa mambo yote ya muungano kwa vile hakuna chombo kilicho juu ya rais wa munngano ambapo Zenj wanaweza kupeleka malalamiko.
 
Aache chokochoko..... Rasimu ya Katiba ya Warioba iliwapa uwiano sawa wao wakaitaka ya Sitta. Atulie!!!
 
Naona koti alilovaa lishaanza kumvuka
Aangalie asije akavuliwa hapo Chamwino akifikiria mamlaka wanayo Mchambawima ama Kiembesamaki
 
Kama tunaendelea na muungano ambapo rais wa Tanzania bara ndiyo anakuwa rais wa serikali ya muungano, kamwe hapatakuwa na usawa wa pande mbili za muungano. Tanzania bara kwa wingi wao wataendelea kuwa na turufu kwa mambo yote ya muungano kwa vile hakuna chombo kilicho juu ya rais wa munngano ambapo Zenj wanaweza kupeleka malalamiko.
Unadhani suluhisho sahihi ni lipi hapa? Mi nionavyo ni kuwepo kwa nchi moja iliyoungana tu, jeshi moja, serikali moja, Bunge moja nknk, wewe je?
 
Hesabu Za sehemu si zinajulikana? Either Kwa kutumia population au eneo au??? Formula tuliopewa ya 4% + 96%= 100
 
Wazee wa changu changu,chako chetu.!!hawataki ujinga kabisa yaani.
 
Back
Top Bottom