Dk. Shein ataka usawa mambo ya Muungano

Dk. Shein ataka usawa mambo ya Muungano

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,188
shain+pic.jpg

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametaka jambo linalohusu Muungano linalofanyika Tanzania Bara, lifanyike pia na visiwani humo bila ubaguzi wowote.

Dk Shein ametoa kauli hiyo jana katika ufunguzi wa jengo jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) liliopo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Huku akitolea mfano jengo hilo alisema, “Kukamilika kwa jengo hili ambalo linafanana na lile la Dodoma ni ishara mojawapo ya kuwa ipo haja kwa kila jambo la muungano linalofanyika Tanzania Bara na Zanzibar linapaswa kufanyika pia ili kutoufanya upande mmoja kujiona kama umetengwa. Si busara kwa mambo ya muungano kufanywa upande mmoja tu au upande mmoja kuonekana unajivutia wenyewe kila kitu, hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa katika utendaji wa masuala ya muungano.”

Alisema watendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri na watendaji wote wanapaswa kuelewa kuwa mambo ya muungano yasifanywe na upande mmoja.

Alisema jambo hilo likifanyika litasaidia pande zote mbili za Muungano na kusisitiza kuwa ametoa kauli hiyo kwa kuwa ni mzoefu akiwa ametumikia miaka tisa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Dk Shein aliishukuru Benki ya Dunia (WB) kwa misaada yake kwa Zanzibar kupitia Serikali ya Muungano, jambo ambalo alisema litarahisisha utaratibu wa ukusanyaji wa takwimu.

Mtakwimu Mkuu wa SMZ, Mayasa Mahfoudh Mwinyi alisema Sh7.9bilioni zimetumika katika ujenzi wa jengo hilo la ghorofa nne lenye vyumba 60 ambalo linatarajiwa kutumiwa na watumishi 164.


Chanzo: Mwananchi
 
Mmmmmh hii kauli japo ni nzuri Ila inaukakasi flani hivi. Haiwapendezi ndugu wale wa mama yule wa upande ule. Time will answer each question when it comes
 
Simuelewi anachotaka atakisimamia vipi kwani ili kitimie au aweze kudai ni muhimu kuwa na serikali 3. Kila mshiriki atakuwa na uwezo wa kudai huduma sawa toka serikali ya muungano vinginevyo ni maneno matupu. Au ndio anapeleka ujumbe kwa yule Jamaa Pale Magogoni (jpm)?
 
Mbona jengo hilo limetumia gharama kubwa wakati wale waliojenga hostel za Udsm walitumia pesa kidogo na wamejenga maghorofa mengi tu.!
 
Kinachoniuma ni kuona mpaka leo kuna Wazanzibari wanatembea peku peku... Changamoto za umaskini bado ni kubwa visiwani Zbar, ipo haja ya kuongeza jitihadi za kuhakikisha kila mzanzibari anapata fursa za kiuchumi ili kuweza kukidhi mahitaji ya msingi na ya ziada...
 
Ishu ya muungano, IPO siku atakuja Farao asiyemjua Yusufu huko Zenji atasumbua sana, ni bora tukayahandle haya mambo mapema kupitia katiba Mpya otherwise itakuja Kuwa too late
 
Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametaka jambo linalohusu Muungano linalofanyika Tanzania Bara, lifanyike pia na visiwani humo bila ubaguzi wowote.

Alisema watendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri na watendaji wote wanapaswa kuelewa kuwa mambo ya muungano yasifanywe na upande mmoja.

Usawa wa nini wakati hawachangii hata senti!?!

Nina mwaka wa saba sasa napita bajeti za mawizara ya Zanzibar, sijawahi ona fungu la kugharamia mambo ya Muungano kama Deni la taifa, Mahakama ya Rufaa, Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Jeshi la Polisi, Uhamiaji, JWTZ, Wizara ya mambo ya nje, na nk.
 
Back
Top Bottom