Dk. Rashid na mabosi wake hawakuiva | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Rashid na mabosi wake hawakuiva

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Sep 26, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  UHUSIANO mbaya kati ya uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Bodi ya Shirika la Umeme (TANESCO) na Mkurugenzi Mkuu Dk. Idris Rashid ndio chanzo cha nafasi yake kutangazwa harakaharaka kuwa i wazi, Raia Mwema imeambiwa.

  Tangazo la kumtafuta mrithi wa Dk. Rashid lilichapishwa wiki iliyopita katika magazeti bila yeye ama menejimenti ya TANESCO kujua, na habari zinasema liliandaliwa kwa siri. Kwa mujibu wa mkataba wake wa miaka mitatu, Dk. Rashid anafikia mwisho wa ajira yake TANESCO Novemba mwaka huu.  Dk. Idris Rashid
  Vyanzo mahsusi vya habari vimeiambia Raia Mwema ya kuwa pamoja na Bodi na Wizara kufahamu kwamba Novemba ndio mwezi wa mwisho wa Dk. Rashid kufanya kazi, si yeye wala menejimenti iliyopewa taarifa ya kutangazwa kwa nafasi yake wakati wa maandalizi ya tangazo hilo.

  "Menejimenti imezungukwa. Haikufahamu wala kushirikishwa kwa chochote kuhusu kuandaliwa na hatimaye kutangazwa kwa tangazo kwamba nafasi ya Mkurugenzi ipo wazi," kilidokeza chanzo chetu cha habari.

  Wizara ya Nishati na Madini inaongozwa na mawaziri vijana, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, ambao wote, kwa nyakati tofauti walipata kufanya kazi chini ya Dk. Rashid, na kwamba uhusiano wao mbaya ulianzia huko.

  Ngeleja, kabla ya kwenda kugombea ubunge wa Jimbo la Sengerema alikoibuka mshindi, alikuwa akifanya kazi kama mwanasheria wa kampuni yenye mtandao mkubwa wa simu za mkononi ya Vodacom ambayo ilikiwa ikiongozwa na Dk. Rashid.

  Kabla ya kuukwaa uwaziri, alikuwa naibu waziri katika wizara hiyohiyo akifanya kazi chini ya Nazir Karamagi, mfanyabiashara na Mbunge wa Bukoba Vijijini ambaye sasa ni majeruhi wa sakata ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

  Kwa upande wake, Malima, ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuingia serikalini, ametokea Jimbo la Mkuranga na alipata kufanya kazi Benki Kuu (BoT) ambako Dk. Rashid alikuwa Gavana.  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima
  Taarifa zinasema katika nyakati hizo, wote wawili wanaweza kuwa hawakuwa na mahusiano mazuri na bosi wao, na habari zaidi zinasema kwa upande wake Malima aliondoka BoT wakati huohuo wa Dk. Rashid.

  Habari zinasema akiwa bosi katika asasi hizo, Dk. Rashid alipata kufanya uamuzi uliowagusa vijana hao wakati huo na hali kati yao haikutengemaa hata baada ya kukutana tena na Dk. Rashid TANESCO safari hii wao wakiwa mabosi kwake.

  "Unajua Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO (Peter Ngumbulu) ni mgonjwa. Sasa kilichobainika ni kwamba kulikuwa na mawasiliano na maelekezo kati ya Wizara, Bodi na mmoja wa watumishi waandamizi ndani ya Sirika," kilidokeza chanzo chetu cha habari.

  Taarifa zaidi zinaeleza kwamba ukiacha uhusiano wao mbaya kama watu, ilizuka migongano mingine kati yao iliyotokana na uamuzi wa Dk. Rashid wa kutaka Wizara ya Nishati na Madini ilipie kodi ya pango kwa jengo inalotumia kama makao makuu yake, ambalo ni mali ya TANESCO.

  Mbali na jengo hilo, Dk. Rashid pia amekuwa akitaka Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam inayotumia majengo ya TANESCO kuendesha huduma zake ilipie kodi TANESCO, na wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kirejeshe au kilipie kodi jengo la TANESCO, lililopo Area D, Dodoma, ambalo limekuwa likitumika kama Rest House ya chama hicho. Taarifa zaidi zinasema ya kuwa baada ya mvutano wa muda mrefu, sasa CCM imekubali kurejesha Rest House hiyo TANESCO.

  Habari zaidi za kutoka ndani ya TANESCO zinasema pia ya kuwa hata huko Dk. Rashid hakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya maofisa waandamizi, wengi ambao alipofika aliwashusha vyeo, wengine akawafukuza kutokana na kupungukiwa sifa za utumishi na yeye kuja na timu mpya.

  Lakini kama alipata laana ya vigogo kadhaa, alipata pia kuungwa mkono na wafanyakazi wa chini waliomfurahia kwa uamuzi wake wa kuanza kuwalipa bonusi inayodaiwa haijapata kulipwa tangu mwaka 1964.

  Baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na Raia Mwema wamekuwa wakisema walipewa uhuru mkubwa wakati wa Dk. Rashid, uhuru walioukosa kabla kutokana na baadhi ya maofisa kujigeuza miungu watu.  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja
  Tatizo jingine linalotajwa kuzuka baina ya Dk. Rashid na Bodi yake ni kinachoelezwa kwamba Waziri Ngeleja ana nguvu nyingi ndani ya Bodi hiyo kupitia kwa mjumbe mmoja, Beatus Segeja, anayedaiwa kuwa alipata kuwa meneja wake wa kampeni jimboni Sengerema.

  Hata hivyo, pamoja na hayo, kwa upande mwingine Dk. Rashid anahusishwa na mambo mbalimbali zikiwamo tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

  Dk. Rashid anahusishwa na kashfa hiyo akiwa Gavana wa BoT. Kashfa nyingine anayohusishwa nayo ni kutumia mabilioni ya fedha za mkopo uliochukuliwa na TANESCO kwa kukarabati nyumba ambayo anadaiwa kulenga kujiuzia kwa ya chini kuliko thamani ya ukarabati.

  Anadaiwa pia alikuwa mstari wa mbele kushinikiza kununuliwa kwa mitambo ya kufua umeme kutoka kampuni ya Dowans, akipingana na Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, iliyosisitiza kuwa ununuzi huo ni kukiuka sheria ya manunuzi ya umma.

  Kwa upande wa watumiaji umeme, uongozi wa Dk. Rashid umekuwa ukitafsiriwa kuwa mstari wa mbele kuongeza bei ya umeme kuliko kuboresha huduma kwa wateja.

  Kwa mujibu wa matangazo ya magazetini, waombaji wa nafasi hiyo ya Dk. Rashid ambaye amekwisha kusema ya kuwa anapumzika baada ya kufikisha miaka 60, wamepewa hadi Oktoba 2, kuwa wamewasilisha maombi.

  Source: Raia Mwema

  Mie naomba niongezee kwamba tatizo la Tanesco na mashirika mengine ya umma ni kwamba hakuna utawala bora. Dk Rashid ni mtu mwadilifu na siamini skendo zinazomhusisha yeye (ie. Radar na nyenginezo amehusika but uchunguzi unaendelea tutajua ukweli au ni smear campaign) but ni kwamba ni mtu ambaye alikuwa anapenda watu wote wafaidike na sio wateule wachache. Kiukweli hili ndio tatizo na la Tanzania na mashirika yake kwamba mtu akiingia serikalini anaona anaenda kujitajirisha na sio kutumikia na kulipwa ujira wake.

  Binafsi huyu jamaa alipokuwa BOT yeye na yule naibu gavana (mbaye) ambaye walimsimamisha pia walikuwa ni watu waliokuwa wakiisafisha BOT kutokana na uozo uliokuwapo. But wakaonekana maadui wa system kwasababu walikuwa wakiinyima system mshiko na nilijua siku alipoteuliwa Tanesco hatakaa muda mrefu kwasababu ni mtu wa principle na hupenda atende haki kwa wote mkitaka kufahamu zaidi waulizeni watu waliokuwa wakifanya kazi NBC wawaambie alipokuwa md wao.

  Kimsingi mambo matatu yamemponza Dk Rashid:
  a). Kuwa mkweli jambo ambalo watu wengi hawalipendi wanataka uwe mnafiki mnafiki ili mambo yao yaende fresh.
  b) Kuwa muwazi viongozi wetu wengi wa mashirika ya umma hupenda majungu na umbea huyu jamaa ukipeleka jungu anaitisha mkutano mnadiscuss wote waulizeni tena watu wa NBC watawaambieni ,
  c). Anaipenda dini yake (uislamu). Safari moja walifanya mkutano ijumaa jamaa akawaambie mkutano mwisho saa tano maana anaenda kusali ijumaa. Sasa kimsingi mtu ukiwa hivyo katika mashirika ya umma utaonekana mdini au mtu fulani mwenye msimamo mkali. kiufupi baada ya muda utaangushwa tu. Anayependwa ni yule mtu anayepindisha mistari ya dini, ndio anafaa.

  In summary haya ndio mambo yaliyomponza jamaa but ukweli iko siku utafahamika. But viongozi wengi wa mashirika ya umma watakikana wawe waongo, wanapenda majungu, wanafiki na mwisho wa siku shirika likishakufa yeye yuko tayari kujitoa muhanga kwa wakubwa ilihali apate ujira wake.

  Swali je Tutafika????
   
 2. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  This is a very interesting conspiracy theory...but in my eyes its not abt ngejela and malima ..hao ni wanasiasa dagaa tuu they have nothing to loose...uliza nani wananguvu kuhusu vodacom na wakina nani ndo walikuwa na bado wanaendelea kuomba mikataba ya kuzalisha umeme kwa ubia na tanesco ambayo mingi rashid kachomolea...its deeper than malima and ngejela people!
   
Loading...