MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile (CCM) amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Bara la Afrika kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Ukimwi (IAS) ambapo atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne.
Hiyo ni mara ya pili kwa Dk. Ndungulile kushika nafasi hiyo baada ya kipindi cha mwaka 2008 - 2012 kumalizika.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Dk. Ndungulile, ilieleza alichuana na wagombea wengine 13 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambazo ni Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Morocco, Sudan na Misri.
Alisema majukumu ya taasisi hiyo yenye makao makuu yake Geneva, Uswisi ni pamoja na kuhamasisha njia bora na ya kisasa katika mapambano dhidi ya ukimwi, kutoa elimu na kujenga uwezo wa wataalamu wa ukimwi katika vita dhidi ya ugonjwa huo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.