Dk Mwakyembe arejea nchini

Cjalkuelewa

wabongo our line of thinking is becoming questionable ila tunashukuru mwakiembe karudi salama
Swali je kabla ya ccm kudaka agenda ya cdm ya kupinga ufisadi ina maana viongozi hakuwa wanaugua kama ilivyo kawaida kwa binadamu kuugua?
 
Hivi hamna aliyebahatika kuipata picha yake alipotinga jijini ili tujionee yaliyosemwa uongo na ukweli wake
 
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya. Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

“Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama .Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake.” Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

::Mwananchi::


...ndugu zanguni, nashukuru MUNGU kama kweli Kamaradi Dr Harrison Mwakyembe amerudi akiwa na afya njema!! Mimi mtanisamehe, kwani utambuzi wangu wa ziada (sixth sensory ability) unaniambia hali si njema kama inavyosemekana. Niko pessissmitic kwa sababu kubwa mbili:
1. Kama hali yake ni njema, kwa nini madaktari wake kule India waliamua kukaa kikao kizito cha maamuzi ya kumruhusu kuondoka au la;
2. Kwa hulka ya Mpambanaji huyu, yeye ni kipenzi cha vyombo vya habari na anapenda na yeye mwenyewe akiwa pia mwandishi wa habari ana-enjoy kuongea na vyombo vya habari kwa kwenda mbele. Kitu gani kilimfanya asionekane hata kidogo kwa waandishi? (japo hata picha tu kama kuongea alikua hawezi!).

Labda ni wasiwasi wangu tu lakini....mnhh!
 
Back
Top Bottom