Dk Mwakyembe agoma kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Mwakyembe agoma kujiuzulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 3, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Boniface Meena, Dodoma, Kelvin Mtandiko, Dar
  WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema hawezi kujiuzulu kutokana na ajali ya Mv Skagit kwa sababu hahusiki na suala hilo.

  Pia, amesema kitendo cha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud kwasababu ya ajali hiyo kimechelewa kwa kuwa alitakiwa afanye hivyo tangu wakati wa ajali ya Mv Spice Islanders.

  Dk Mwakyembe alisema hayo jana bungeni alipokuwa akijibu hoja za wabunge katika hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13.

  Alisema kujiuzulu ni kitendo cha heshima na inashangaza sana mtu anapojiuzulu kiuwajibikaji halafu anaanza kulalamika kwa pembeni.

  “Kwa hili langu halina msingi wowote wa mimi kuweza kujiuzulu kwa kuwa Rais wa Zanzibar amelizungumzia vizuri na pia Rais wa Jamhuri ya Muungano amelizungumzia pia,”alisema Dk Mwakyembe.

  Alisema uhusiano wake kimamlaka na upande wa Zanzibar unaishia Chumbe tu kwa kuwa hana mamlaka kwa upande huo mwingine wa visiwani.

  Dk Mwakyembe alisema, sheria za awali iliyokuwa inasimamia pande hizo mbili ilikuwa inasimamia vyombo vya majini kwa umakini na kwamba baada ya kutenganishwa kwa mamlaka za usimamizi, kila mamlaka ikawa na sheria zake.

  “Uhusiano wangu kwa upande wa Zanzibar mwisho wangu ni Chumbe hivyo sijiuzulu, sheria yetu iko strictly(makini) kwenye masuala ya vyombo vya majini lakini ya Zanzibar haibani hivyo,”alisema Dk Mwakyembe.


  Katika hatua nyingine, amepiga marufuku kuanzia sasa kwa mabasi ya abiria yaendayo mikoani kusimama eneo lolote njiani kwa madhumuni ya abiria kujisaidia haja ndogo.

  Akizungumza jana wakati wa kutoa pendekezo la kuungwa mkono na wabunge kwa bajeti ya wizara yake, Mwakyembe alisema endapo basi litaonekana barabarani limepaki kwa ajili ya kuchimba dawa litafungiwa leseni.


  "Hali hiyo inamdhalilisha sana mwanamke, amezaliwa na umbile la kujisitiri sijui kwa mwanaume lakini inashusha heshima ya wazazi wetu,abiria wote wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kwenye vituo vikubwa wanavyosimama,"alisema na kuongeza kuwa:

  "Tutatoa onyo kwa mara ya kwanza,ya pili kama hatutajirekebisha basi tunachukua maamuzi[uamuzi] wa kumfungia leseni,kumuona mama yako anajisaidia ni sehemu ya kujilaani,hatuwezi kudhalilisha hivyo mama zetu,huo si utamaduni wetu".

  Waziri wa ujenzi' Dk.John Magufuli wakati wa kupitisha bajeti yake alizungumzia suala hilo baada ya kuulizwa na wabunge kuwa hali hiyo ni sehemu ya uchafuzi wa mazingira.

  Waziri Maghufuri alisema, Serikali kwa sasa haina uwezo wa kutekeleza yote na kutoa milango wazi kwa mwekezaji yeyote atakayeweza kujitokeza ili kujenga vituo hivyo njiani kwa barabara zote za mikoani.
  Dk Mwakyembe agoma kujiuzulu

   
Loading...