Dk Kikwete hujalitendea haki taifa langu

Dk Kikwete hujalitendea haki taifa langu

Ngurubhe

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,840
Reaction score
1,049
Inawezekana mim nina madhaifu, kuwa sijawahi kumuona rais Kikwete ameonekana amekelwa au hata kuwa serious kukemea wizi hasa mkubwa kama huu uliotokea hivi karbuni. Sasa mimi huwa najiuliza labda kwa kuwa ni rais bas ana hela nying sana kias kuwa hela zinazopotea ni kidogo na hana machungu kabisa.

Hivi angekuwa Mwl Nyerere yuko hai na ndio anahutubia,je taifa lingekuwaje?,bila shakaTaifa lingezizima....na hata watoto wadongo wangejua kuwa leo rais anaongea na wananchi!....sasa jamaa anaongea utadhani anapga stori za kawaida sana kibarazani kumbe anaongea na taifa tena juu issue nyeti hzi za uwajibakaji na uwajibishaji.

Jana rais wangu hujalitendea haki taifa langu, kwanza ulionekana kutoa maamuzi kwa kuogopa, kusitasita utadhani na wewe umeiba hizo hela!
,unasingizia kikohozi kweli, rais?.basi kama ulikuwa hauko sawa kiafya Dactari wako hakuliona hilo?... si angeshauri uhutubie taifa ukiwa sawa kiafya?.. Hvi ulijua kama dunia nzima walikuwa wanakufuatilia?,walio nje na ndani ya Tanzania,walio watanzania na wasio!....

Wewe unaongea na sisi utadhani tumekaa barazani tunapiga stori za mechi za Simba na yanga!,inauma sana .....

Binafsi nilichukia sana, kwani nilitegemea kwa mda wote uliodai wajiandaa ili uongee na wananchi ulitakiwa kuja na majawabu ya maswali mazito yalifungata mioyo ya Watanzania,
yanayowasumbua wananchi hadi sasa!

Ulikuwa unafanya nini, almost siku 23 hadi jana toka ulipoahidi kuongea na kutoa maamuzi juu ya watuhumiwa wa scandal ya ESCROW.Maana umekuja bado wengne unawaweka kipolo kuwa huo mda haukutosha kuwachukulia hatua?.

Skufundishi kazi lakini kwa hili Hujalitendea Haki taifa langu!....

Kwanza hotuba yako ilikuwa ni ya kawaida sana kana kama hakuna tatizo lolote ndani ya taifa!,

Na ulihutubia kana kwamba unatimiza tu wajibu kwa sabab ulishatoa ahadi ya kufanya hivyo,kwani kuna mambo mengi tu yaliyokuwa yanapaswa kutolewa majibu na Mkuu wa Taifa....yamebaki kuwa pending....uhm Dk.,Hujalitendea haki taifa langu....

Rais Kikwete, au ndio na wewe unajua ikoje?Au Ndio maana unaogopa kuwa mkali juu ya wizi kama huu,kwamba hata sku moja muovu hakemeii uovu? Au ndio unataka uondoke salama? Au ndio unataka kutupooza tu wananchi kwa kumtoa kafara mama Tibaijuka?

Inawezekana huyu mama hajui chochote ndio maana mnamuengua hadharani!,wenye siri nzito umewaacha kwani wakja ktaa wataaniaka uvundo ulioko hko?...


Akina muhongo wanajua siri nzito ndo maana mnawaweka kipolo ili wasiwaumbue na nyie. Rais kama utapata nafas nyingne toa hutoba nyingne itakayojibu maswali juu ya mabilion ya fedha kwenye taifa lako, na kutoa mwanya wa uwajibikaji kuchukuwa nafas yake, sio kuongea kana kwamba na wewe ni mwizi hivyo unaogopa utakachoamua wezi watasema mbona na wewe rais tulikuwa pamoja!

Na haki unayoisema ichukuwe nafas sio kumuumiza mlaji unamuacha aliyepika chakuka chenye sumu.

Na swala la uchunguzi kwa mambo ambayo yako wazi ni kuwaibia wananchi. Na serikali yako rais imetia fora kwa kuunda tume kisha hizo tume hata hazitusaidii. Kama unadhani nakuonea kuiponda hotuba yako njoo kitaa usikie..
Usifunike kombe ili mwanaharam apite!....
Sikufundishi kazi lakini kwa hili la escrow..hata bibi yangu anajua kama huu wizi hauvumiliki na hasa alipojua kuwa hizo hela ni nying sana, wakt yeye hata 1000 kwa wiki haioni..... anaichkia sna serkali yako fisadi!..
 
Hata Mi Nilishangaa, Ndita Nyanya Kabisa
 
Kiukweli style nzima ya Mheshimiwa alivyo handle hii issue ya ESCROW sijaipenda. Something is very Wrong here!
 
Kila kitu anaona ni mzahaa tuu,hakufaa hata kuwa balozi wa nyumba kumi.
 
Naunga mkono hoja mia aisee ingekuwa ni Kenya au south afrika naona tungekuwa tunaongea mengine kwa sasa.

Daaaaaaaaaaaaaaaah wananchi mitaani wana hasira ni manung'uniko kila kona!! Kwa hili ki ukweli hapa Taifa hakuna!!! Tushazikwa tungali hai!!! Hii hotuba imetuvunja moyo wengi!!!! Hivi wananchi hatuwezi kuchukua maamuzi yoyote tunusuru nchi hii? R.I.P JK Nyerere!
 
Ngoja tu mm ninyamaze mana nitatukana, watu wengine sijui wapoje yani ishu serious yeye analeta ufyolo ufyolo tu
 
Nashindwa kuwaelewa watanzania juu ya kiwango cha uoga tulichonacho. Binafsi namwambia hivi; "ondoka zako tuachie nchi yetu kwani kitendo unachofanya cha kuwalinda wezi kila wakati ni kuivuruga amani uliyotukuta nayo". Ndiyo, sina amani. Nitapataje amani wakati nadaiwa kila kona kuanzia nyumbani, mtaani hadi china na ulaya?. Nenda kajifiche kama Balali wala hatutakutafuta. Nimekereka sana kwa jinsi unavyorahisisha mambo ya kuudhi na kuyafanyia mizaha na kuigeuza kichekesho. Sijajua kwa uhakika unamfurahisha nani. Kwa taarifa yako umeisambaratisha ccm na kina nape na kinana watakususia ccm yako ya kifisadi unayoijenga.
 
usimwingize Rais kwenye mambo yenu ya kitoto mwache afanye kazi yake utoto wenu fanyeni huko kwenye vibanda vya kuangalia sinema,
 
Kwa kauli na hali aliyokuwa nayo Mh. Rais Kikwete kuna uwezekano mkubwa kuwa:
1. Mamlaka tuliyompatia yalishapokwa na wezi waliomzunguka pale Ikulu.
2. Yeye mwenyewe, familia na hata wasaidizi wake wa karibu wanahusika na wizi huu
3. Rais alitishwa na genge lililomzunguka
4. Uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo
5. Ni mwoga na pengine hajui hata wajibu wake kama Amri Jeshi Mkuu wa Nchi.
 
mkuu unataka jk agawe viroba kwa familia yako?
 
Fikra za utwana utazijuwa tu, mpaka mkemewe mpigiwe kelele kama mnavyokemewa na wachungaji wa Jangwani ndiyo mnaona mnaongozwa.

Amma kweli biblia haijakosea ilipomwita mkanaani Mbwa na nguruwe.
 
watu waajabu sana, yani mlikua mnasubiri Rais awape majibu wakati mlikuwa nayo! ameongea mnasema sio sasa aongee yenu? mwacheni amalizie ngwe yake mtampata Rais mnaemtaka 2015 is just approaching.
 
Fkra za utwana utazijuwa tu, mpaka mkemewe mpigiwe kelele kama mnavyokemewa na wachungaji wa Jangwani ndiyo mnaona mnaongozwa. Amma kweli biblia haijakosea ilipomwita mkanaani Mbwa na nguruwe.

sijakuelewa au nina mawenge ya hotuba ya jana!. Naamini wewe ni mama wa familia. Unaileaje familia yako?. Hujawahi kumfokea mtoto akikosea yale uliyokwisha kumwelekeza mara nyingi?. Mwanao akituhumiwa wizi huwa unamchekea na kumpongeza na sio kumfokea kwa tabia zisizopendeza kwenye jamii?. Rais alitakiwa kuwafokea wote waliotuhumiwa kwa wizi ule na sio kuwachekea kama alivyofanya jana. Kama kufoka si kuongoza basi wewe na yeye ni bora wazazi kwani hamjui kulea. Unamchekea mwizi badala ya kumfokea!.
Kwanza ututake radhi kwa kutuita watwana na kama mkanaani ni wewe usiyejua kulea.
 
usimwingize Rais kwenye mambo yenu ya kitoto mwache afanye kazi yake utoto wenu fanyeni huko kwenye vibanda vya kuangalia sinema,
Ukweli ni kuwa hatuna Rais zaidi ya babu mipasho! Huyu jamaa utadhani hajawahi kukanyaga kunako shule! Hayuko serious na chochote. Naanza kuamini kuwa yale yasemwayo kumhusu na familia yake ni kweli. Anazungumza kana kwamba ni vijisenti tu ndo vilivyoptea. Anazungumza kana kwamba ni mwanaJF fulani anatoa maoni yake. Amesahau kuwa ana wajibu wa kutengua alichoteua....najiuliza iwapo kweli yeye ndiye aliyewateua anaowaogopa kwa kiasi hichi. Ameonyesha woga mkubwa na hapendi lawama...hata kutamka kuwa amemfukuza Tibaijuka anaogopa...hivi likitokea jambo lolote serious zaidi ya hili si atatuuza mara nyingine tena? Nna uchungu na huyu mjamaa basi tu!
 
Ukweli utabakia kuwa tunaye Rais asiye serious hata kwa mambo yaliyowazi. Udhaifu wake ndo legacy atakayoacha na historia itamhukumu
 
Back
Top Bottom