Dk Kafumu akata rufaa Igunga

Dk Kafumu akata rufaa Igunga

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
ALIYEKUWA Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), ambaye alivuliwa ubunge na Mahamaa Kuu Kanda ya Tabora Agosti mwaka jana, amekata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Mary Shangali, alitaja vipengele sita alivyotumia kutengua matokeo ya ubunge wa Dk. Kafumu. Alisema vipengele hivyo vilikuwa ni pamoja na matukio yaliyojitokeza wakati wa kampeni za uchaguzi huo ambapo ni kutolewa kwa ahadi ya kutojengwa daraja kama hatachaguliwa Kafumu.

Hata hivyo, katika rufaa yake hiyo aliyoiwasilisha mahakamani juzi, Dk. Kafumu alisema anaamini atashinda kutokana na sababu zilizotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu kuwa dhaifu na zisizomhusu yeye.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Dk. Kafumu alisema kuwa atawakilishwa na mawakili watatu ambao aliwataja kuwa ni pamoja na Dk. Masumbuko Lamwai, Kayaga na Kanyama.

Dk. Kafumu alisema sababu za kutaka rufaa mbali na kwamba ni haki yake Kikatiba lakini pia anaamini kuwa mahakama kuu ilikosea
kumhusisha na vurugu zilizosababisha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Igunga, Fatuma Kimario, kuvuliwa Hijab na wafuasi wa CHADEMA.

Alisema kitendo cha Magufuli kutoa ahadi ya daraja ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye binafsi hakuhusika kutoa ahadi hiyo. Katika mahojiano hayo, Dk. Kafumu alilalamika kuwa baadhi ya waandishi wa habari walimlisha maneno kuhusu uamuzi wake huo wa kukata rufaa na hivyo kufafanua upya kile alichokisema baada ya hukumu. "Nilisema nimetoka mahakamani, bado mapema nawasiliana na chama changu, lakini hata kama nikipoteza ubunge na ukamishna wa madini, mimi bado ni mtaalamu nitafanya kazi nyingine, sikusema sitakata rufaa," alisisitiza.

Katika kesi hiyo mlalamikaji alikuwa Joseph Kashindye, aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA.

Katika hukumu yake Jaji Shangali alisema ahadi hiyo ilikiuka mwenendo wa kampeni za uchaguzi. Aidha Jaji alisema pia kitendo kilichofanywa na upande wa walalamikiwa cha kwenda kutembelea hospitali na kutoa misaada mbalimbali kilikiuka taratibu na hivyo kuathiri zoezi zima la uchaguzi huo.

Kipengele kingine alichokitaja kukiuka taratibu za uchaguzi ni pamoja na kitendo cha ugawaji mahindi ya msaada siku chache kabla ya upigaji kura katika jimbo hilo na hivyo kuwafanya wananchi kupiga kura kutokana na ushawishi wa misaada hiyo.

Pia kupanda katika majukwaa ya kampeni kwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), akiwa amening'iniza silaha kiunoni nako kuliathiri mwenendo mzima wa uchaguzi huo.

Source: Tanzania Daima
 
Hya sasa...Obviously hii ni baada ya shinikizo la JK alipotembelea Igunga majuzi!!
Na mtaniambia matokeo ya rufaa hiyo!
 
baada ya kushauriwa na JK sio, subirini yetu macho na masikio
 
Hivi kisheria ni muda gani unapita ili rufaa iwe valid baada ya hukumu? Maana huyu imeshapita miezi minne sasa, au ndo ile ya tukose wote baada ya kesi kuahirishwa mpaka 2015?
 
Ngoja tuanze tena kusikia purukushani za IGUNGA na ulaji wa UBWABWA........
 
Hee kumbe hotba ilifanya kazi!

Siyo huyu aliyedai anaachana na siasa kabisa anajirudia zake alikotoka? Au 'alinukuliwa' vibaya?
 
Hapa hamna kitu, ni kiini macho tu. Style ya kampeni ya CCM, huwa inawapa technical knockout. Hawaamini katika demokrasia ya kweli, mengi yamejificha. Ngoja tuone mahakama zetu, maana naona kama zimezinduka katika haki. Tumuombe Mungu wetu haki itendeke.
 
Hya sasa...Obviously hii ni baada ya shinikizo la JK alipotembelea Igunga majuzi!!
Na mtaniambia matokeo ya rufaa hiyo!

Mkuu PJ, hii rufaa ina lengo la kuzuia by election jimbo la igunga ili kuikinga ccm isipate aibu ya karne kama si kuizuia sauti ya mabadiliko isipokelewe na watanzania maeneo ambayo bado wanaikumbatia ccm.
HAKUNA JAJI ANAWEZA PANGUA SABABU ZOTE SABA HADI KAFUMU AWE MBUNGE HALALI IGUNGA.
 
Hee kumbe hotba ilifanya kazi!

Siyo huyu aliyedai anaachana na siasa kabisa anajirudia zake alikotoka? Au 'alinukuliwa' vibaya?

Mjini jua kali sana, watu hawajui wewe mtaalamu au chokoraa. Nasikia amehamia Pugu kajungeni anaganga njaa huko. Nchi hii ina dhambi sana, yaani mtaalamu kama huyu wanam-ground halafu matapeli wanapeta mjini!!
 
Hili ni jaribu lingine zito kwa mahakama, kwani ndiyo itakuwa nafasi nyingine tena kwa Mahakama ya Rufaa kutenda haki bila kuingiliwa na wanasiasa!
 
Magufuli alitoa ahadi za ujenzi wa daraja la Mbuntu ambalo ni moja ya changamoto jimboni humo. Alitoa ahadi za kugawa mahindi ya njaa kwa wananchi wa jimbo hilo. Pia alitoa viapo kwa baadhi ya ahadi alizokuwa akizitoa katika majukwaa ya kumnadi Dr. Kafumu.

Magufuli aliyasema haya yote jukwaani akiwa amevalia jezi ya CCM mbele ya Dr. Kafumu, na wala Dr. Kafumu hakukanusha kuwa kitendo cha Magufuli kutoa ahadi ya daraja ilikuwa ni sehemu tuu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye binafsi hakuhusika kutoa ahadi hiyo.

Hata kama ahadi ya daraja ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa yeye alikuwa anagombea kutekeleza ilani ya chama kipi? Zipo mpaka video za kudhibitisha kuwa Magufuli alitoa hiyo ahadi mbele ya Dr. Kafumu na akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa daraja hilo litatengenezwa.

Baada tuu ya Magufuli kuyasema hayo, Dr. Kafumu badala ya kukanusha kuwa Magufuli kutoa ahadi ya daraja ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye binafsi hakuhusika kutoa ahadi hiyo, alisema "Nilikuwa nanong'ona na Mh. Magufuli hapa..... anasema hivi … kwamba chochote kutoka kwangu kuhusu mtandao wa barabara….na mimi nitafanya…"

Kwa ushahidi kama huu hii ni appeal nyingine laini mno ambayo haitampa shida kabisa mwanafunzi wa sheria mwaka wa pili unless aingiliwe kisiasa.

 
Last edited by a moderator:
Na akishindwa asitegemee CCM itamlipia deni!!!!!!!
hao huwa wanalianzisha halafu wanakimbia..........
 
MaCCM bana so leo ndio yanaona umuhimu wa kkukata rufaa? Hii ni kuwapoteze haki na mudda wao wana Igunga.
 
Na aliapa mbele ya Mungu kuwa atajenga daraja na akaahidi akitoka tu kwenye mkutano ataelekea kwenye daraja la Mbutu. maccm ni janga.
 
Hya sasa...Obviously hii ni baada ya shinikizo la JK alipotembelea Igunga majuzi!!
Na mtaniambia matokeo ya rufaa hiyo!
We mkali mkuu yaani hata sababu anazozitoa KAFUMU ni zile zile aliseama JK eti UTEKELEZAJI wa Ilani Ya chama!
 
Hapa kuna shinikizo, siyo bure, I smell some shit here!
 
mbona huu uzi unarudiwa rudiwa humu? ulukwisharipotiwa kitambo kwa Heading hii
 
Back
Top Bottom