Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Dkt. Kikwete alikutana na tajiri namba moja Afrika, Alhaj Aliko Dangote kutoka nchini Nigeria na tajiri namba moja duniani, Bill Gates kutoka nchini Marekani
Viongozi hao wamekutana nchini Uswisi katika mkutano wa Dunia wa Uchumi (World Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa uchumi wa dunia
Mbali na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa viumbe mbalimbali
Mkutano huu wanahudhuria viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi nyingine za kiraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.
Source : SwahiliTimes