Dk. Hoseah, katimuliwa au muda wake umekwisha?

Dk. Hoseah, katimuliwa au muda wake umekwisha?

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,793
Reaction score
7,165
DK. HOSEAH, KATIMULIWA AU MUDA WAKE UMEKWISHA?

Kufutwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, wala hakunishangazi sana.

Kwani, tangu mwezi Novemba mwaka huu alishaandika barua ya kuachia ngazi. Alifikia uamuzi huo kutokana na umri wake, hivyo alihitaji kupumzika na kufanya shughuli zingine za binafsi.

Hivi sasa Dk. Hoseah ana umri wa miaka 57, na umri wa kustaafu kwa hiari kwa Tanzania ni miaka 55 au 60.

Hivyo basi, kwa uamuzi uliochukuliwa wa kumfuta kazi Dk. Hoseah kipindi hiki, wala hakijanistua na wala hakuhitaji pongezi ya aina yoyote...
Kwasababu, hata kama asingeng'olewa. Ilikuwa kwa lazima, mwaka huu huu Dk. Hoseah aachie ngazi (kwa mujibu wa umri wake).
Ukijua mambo mengi kama mimi, huwezi kupongeza kila kitu..

Hakika Dk. HOSEA ameonewa tu. Kama mtakumbuka amewahi kurekodiwa mwaka 2011. Kwenye mtandao wa wamarekani kuwa Tanzania ina nia ya dhati kupambana rushwa. Tatizo siyo Hosea, tatizo ni mfumo wote wa serikali. Ikumbukwe Hosea amewahi kulalamika kuwa wanakamata wala rushwa ila kes ikifika kwa DPP. haipeleki mahakamani, sasa Walitaka awapeleke mahakamani yy kama yy?. MM mwenyewe na chukia rushwa ila kwa mfumo uliokuwepo.
 
Another Team Lowassa. By the way, how do you feel after posting this nonsense thread? Rais atengue uteuzi wewe utuletee yako ya moyoni? mtaacha lini kujikomba kwa Lowassa!
 
Another Team Lowassa. By the way, how do you feel after posting this nonsense thread? Rais atengue uteuzi wewe utuletee yako ya moyoni? mtaacha lini kujikomba kwa Lowassa!
Dr. Hoseah bado ni mtumishi wa Umma, kilichotenguliwa ni uteuzi wake kama Mkurugenzi lakini ataendelea kuwa mtumishi mpaka itakapoamriwa vinginevyo au mpaka muda wake wa kustaafu utakapofika. Hata hivyo, hana kesi ya kujibu. What do you mean by "Another team Lowasa !!!" Unataka kutudanganya kuwa kuchukuliwa hatua kwa sababu hiyo ??
 
Ni utaratibu wa kawaida kupumzika kazi kwa wakurugenzi wakuu na muda wao wa kutumikia nafasi hiyo huwa miaka minne minne na muda wa mwisho kabisa ni miaka 8. Hivi karibuni hata mkurugenzi wa NBS utasikia kapumzishwa kazi hiyo baada ya kutimiza miaka nane.
 
kuna watu wanaumia sana MAJIPU yanavyotumbuliwa
 
Wapo watendaji wa umma wakitimuliwa unaweza kusikitika sana labda kutokana na uwajibikaji wao wanapokuwa kazini.
Lakini kwa Dr Hosea mimi nimefurahi na tena nimeona maamuzi yamecheleweshwa sana.Huyu ni mtu toka enzi ya JK alipashwa kuwa benchi siku nyingi sana
Dr Hosea amekuwa ni mtu wa kulalamika tu bila kuchukua hatua,Na hata ilikuwa ukimwona amechukua hatua baasi juwa amekamatwa mpinzani wa serekali kwa tuhuma za rushwa
Tena ofisi yake mara zote ilikuwa ikidili na tatizo la rushwa kipindi cha uchaguzi tu kana kwamba rushwa hutolewa wakati wa chaguzi pekee
Taasisi zilizokubuhu kwa rushwa ni Mahakama,Polisi n.k. lakini hosea sikumsikia akidili na watu wa maeneo haya,zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari akilalamika tu.
Kuondolewa kwake ni afya kwa taasisi hii tena walimchelewesha sana alistahili kukamuliwa jipu miaka iilee
 
Mpiga zumali hupiga kufatana na wimbo ulivyo.Kama mwimbaji JK aliimba hivyo yeye ulitegemea apige je zumali? Mfumo mfumo TAKUKURU hawana meno wapeni na tuiweke kwenye katiba kama alivyoshauri Mzee Warioba.
 
Kutengua uongozi wa mtu ambaye amebakiza muda mfupi kustaafu ni njia ya kuonyesha kuwa hafai ili asiondoke na heshima asiyostahili
 
Alivyokuwa kiutendaji haikuwa bahati mbaya, hawa ni wale wateule wachache waliowekwa ili kupanga na kutekeleza project za kifisadi ili hatua zozote za kisheria zisichukuliwe dhidi ya wahusika. Hawa badala ya kufichua kilichokuwa kikiendelea, wao ndio walikuwa wana escort wahalifu hadi kuhakikisha dili limefikia mwisho pasipo tatizo lolote.Haingii akilini haya madudu yanayofichuliwa ndani ya mwezi mmoja tangu uongozi mpya kuingia madarakani eti katika kipindi chote alichokuwa madarakani hakuyaona. Acha asulubiwe kwa haki yake aliyoitimiza.
 
hata muhimbili alitengua uteuzi wa kaimu mkurugenzi na kuvunja bodi iliyo maliza muda wake .
 
Wakati mtoa post unamtetea yeye Hosea akihojiwa na Nipashe anasema hana taarifa.
Kuwa MD kutamu bwana
 
kuna watu wanaumia sana MAJIPU yanavyotumbuliwa
Sana tu. Kumbuka kwamba kuna watu wana maslahi na hao "WATUMBULIWA", wengine ni wazazi wao, wenzi wao, kaka zao, dada zao nk. Sasa mtu akitumbuliwa kuna wengi wanaathirika, ndio hawa wanaokuja kumwaga povu na kumalizia hasira zao humu JF
 
Bado kuna wanaosemaa nguvu ya soda......
Soda hiyo soda gani kila siku inaongezeka nguvu?????

Au sisi tunaona soda kumbe mwenyewe ameweka madawa yaliyopigwa marufuku michezoni ya kuongeza nguvu???
 
tatizo ni check and balance. Hosea hana kosa, shida ni kibohoyo DPP NDIE AFUKUZWE PIA DPP OFFICE IFUTWE. PCCB IPEWE MENO ZAIDI.
 
Back
Top Bottom