...labda na Kikwete atakubali hivi karibuni kwamba Ikulu yake inanuka rushwa na inaongoza kwa kupokea rushwa kuliko taasisi yoyote ile nchini.
hivi first appointment wa hii taasisi huwa wanalipwa kiasi gani wakuu?
Anasahau yeye kama Kiongozi wa TAKUKURU ndiye aliyeshindwa kusimamia taasisi hiyo vizuri na hivyo chini ya uongozi wake rushwa imekithiri ndani ya taasisi hiyo na Tanzania nzima. Kwa kifupi uongozi wa kupambana na rushwa nchini umemshinda.
Anayo mapungufu yake lakini anafanya kazi ktk mazingira ya aina gani? Wewe ungepewa nafasi yake ktk mazingira haya ungefanyaje?
Usitake kubadili huu uzi kama anafanya kazi katika mazingira ambayo hajaridhika nayo kuna kitu kinaitwa kujiuzulu kutokana na mazingira magumu ya kufanya kazi badala ya kuendelea kupokea mshahara na marupurupu makubwa huku taasisi ikishindwa vibaya sana na matokeo yake rushwa kuzidi kukithiri nchini.
Huu ndio unafiki tunao waafrika wengi....
Kuwajibika kwetu ni mwiko ila kulaumu na kuzoza tu....
Huyo Hosea amewahi anikwa na wikileaks. akiwa analalamika jinsi JK alivyo kikwazo ktk kupambana na Rushwa but still anakalia office mpaka Leo....
BAK Jk hana ubavu wa kumtambua Hosea hata iweje.! Kwakuwa ni 'mshirika muhimu' 'kibiashara', biashara zile ambazo hazina hasara hazikatwi kodi, na faida zake ni nono.!Nakumbuka Mkuu jinsi Hosea alivyokana kwamba yeye alihusika na yaliyoandikwa kwenye wikileaks ambayo yalikuwa ni ukweli mtupu. Wengi tulidhani Kikwete angemtimua au angemwambia ajiuzulu kama ilivyo kawaida yake lakini hadi leo hii bado kakalia kiti. Shinikizo la Kinana na Nape kwa Kikwete labda lingeweza kumng'oa lakini ndiyo hivyo tena awamu ya DHAIFU aliyechoka ndio inaelekea ukingoni.