Dk Hoseah akiri Takukuru ‘kunuka’ rushwa

...labda na Kikwete atakubali hivi karibuni kwamba Ikulu yake inanuka rushwa na inaongoza kwa kupokea rushwa kuliko taasisi yoyote ile nchini.

Serikali nzima inanuka rushwa. Mfumo mzima JK aliorithi toka kwa Mkapa na kuuendeleza na kuweka wake ndo shida ilipoanzia. Sasa hivi watu wanakimbilia serikalini kwasababu nje ya mapato yao halali kuna rushwa na upigaji kibao.

Takukuru ni sehemu ya serikali ya JK kwahiyo usitegemee miujiza ya wao kufanya vyema. Takukuru na system nzima haisafishiki hadi uingie utawala mwingine mpya na kusafisha uozo wote wa ccm.
 
Reactions: BAK

Kama Polisi wameshindwa kuwa "imara" sasa hivi kwa hiyo watakuwa "imara" wakipewa kazi ya kupambana na rushwa?
 
...labda na Kikwete atakubali hivi karibuni kwamba Ikulu yake inanuka rushwa na inaongoza kwa kupokea rushwa kuliko taasisi yoyote ile nchini.

Wala haitaji kukiri maana hilo lipo wazi. Haiwezekani kila mahali kukawa na rushwa - polisi, mahakama, serikalini (kwenye wizara mbali mbali), TAKUKURU nk lakini Ikulu ikawa safi.

Siamini kama subordinate anaweza kuwa mla rushwa kama bosi wake si mla rushwa! Huu usemi wa Hosea maana yake nini?

Dk Hoseah alisema ili kupambana na rushwa lazima Serikali iwe na uongozi bora na imara
 
Reactions: BAK
Na mzito mmoja wa PCCB aliyepewa sh millioni 30 na Benki Kuu ya Tanzania wakati wa kashfa ya EPA je? Muda umefika wa kuonyesha alivyopokea na aliyempelekea. Hii ndo itakuwa funga kazi ya rushwa nchini.
wekeni ushahidi hapa tuwamalize mafisi hawa. tumewakabidhi bucha wakati meno yao yamechongoka wanakula hadi mifupa.
 
Taasisi ya
Kuchunguza na
Kusaidia/kusafisha/kuficha
Rushwa kubwa zilizo na maslahi ya wakubwa au zenye maslahi ya kisiasa.

Maono: Usalama na ulinzi wa serikali na wezi walio madarakani dhidi ya rungu la mahakama.
Mkakati: Kuchunguza, kubaini, kuficha taarifa, kuzuia uchukuliawaji wa hatua au inapobidi hatua zichukuliwe na kesi zisimamiwe kwa lengo la kuuhadaa uma lakini matokeo ya kesi hizo hata kama zitahusisha adhabu ndogo ya mwaka mmoja au miwili au kuuambia umma hela ilioibiwa imerudishwa(kiini macho) ili mwishowe ufalme bado usimame na mavuno yawe mengi.


Frankly speaking, mpaka leo sijajua hiki kitengo kilianzishwa kwa madhumuni gani....... serious!
 
Kama Polisi wameshindwa kuwa "imara" sasa hivi kwa hiyo watakuwa "imara" wakipewa kazi ya kupambana na rushwa?
Tatizo unasoma kwa jicho la seriousness sana mkuu, nimesema hao polisi wenyewe yao yamewashinda bora waongezewe na hili itaonekana wana mambo mengi kuliko kutengeneza kitu maalumu kwa ajili ya rushwa alafu linapokuja suala la kushitaki kunakuwa na muingiliano kati ya DPP na PCCB na mwisho wa siku watu wanaachiwa, natambua uwepo wao ila concern yangu wapewe meno na waachiwe wafanye kazi vingenevyo hakuna maana ya kuwa nao,
 
Hivi Edward Hosea ni mfalme ndani ya PCCB? Tangu niifahamu hii idara huwa namsikia tu huyu mzee???

Rais afanye uteuzi upya maana inaoneka Hosea idara imemshinda kabisa.
 
Anasahau yeye kama Kiongozi wa TAKUKURU ndiye aliyeshindwa kusimamia taasisi hiyo vizuri na hivyo chini ya uongozi wake rushwa imekithiri ndani ya taasisi hiyo na Tanzania nzima. Kwa kifupi uongozi wa kupambana na rushwa nchini umemshinda.

Mkuu BAK na bado jamaa anakula mshahara wa nguvu wakati taasisi ya kupambana na rushwa inapokea rushwa naona tuuiite taasisi ya kupokea na kutakatisha rushwa
 
Nakubaliana na yote uliyoandika Bulldog.

 
Last edited by a moderator:
Kilianzishwa kwa usanii tu ili kutuzuga Watanzania kwamba Serikali inafanya juhudi kupambana na rushwa wakati hali halisi haiko hivyo. Pamoja na TAKUKURU kupewa bajeti kubwa sana kila mwaka lakini rushwa ndiyo inazidi kuota mizizi nchini tena hadi ya Ikulu ambapo mabilioni ya peza za walipa kodi yanagawiwa kama njugu na Rais wa nchi akiwa kimya kabisa.

Frankly speaking, mpaka leo sijajua hiki kitengo kilianzishwa kwa madhumuni gani....... serious!
 
Serikali ina pretend kulipa Mishahara ... wafanyakazi wanajitafutia vyanzo vya kujazia vipato vyao... Hali hiii itaendelea hadi CCM ing'olewe madarakani ...
 
Mkuu Sibonike hapo kwenye rangi maana yake uongozi wa nchi ni mbovu na dhaifu hii ni kuanzia ndani ya Ikulu, Baraza la Mawaziri na taasisi nyingine zote nchini ikiwemo TAKUKURU ambazo zinapaswa kuwemo katika hii vita ya kupambana na rushwa. Vita ambayo uongozi huu mbovu nchini umeshindwa vibaya sana.

 
Last edited by a moderator:

Nilitaraji Dr Hosea kujiuzulu Mara moja baada ya ripoti ile inayoonyesha pccb/Takukuru kuwa miongoni mwa taasisi za serikali zinazoongoza kwa rushwa, lakini kwa serikali hii ya chama chawala hiyo ni ndoto isiyo na tija
 
Reactions: BAK
Nilitaraji Dr Hosea kujiuzulu Mara moja baada ya ripoti ile inayoonyesha pccb/Takukuru kuwa miongoni mwa taasisi za serikali zinazoongoza kwa rushwa, lakini kwa serikali hii ya chama chawala hiyo ni ndoto isiyo na tija

Wewe MGOMVI sana ,mara ya mwisho kupelekwa polisi lini?Ajiuzulu halafu kile kiyoyozi kwenye ile VX yake apigwe nani?
 
Nawahakikishieni huyu Dkt anachukia sana jinsi mambo yanavyoenda hapanchini. Mfumo wa sheria umewekewa kigingi na watawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…