Dk. Dau: NSSF inastawisha maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Dau: NSSF inastawisha maendeleo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chuma, Oct 20, 2008.

 1. C

  Chuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wadau nimepita raiamwema nikakuta hio artcle...na yenye Kuendelea...plz fuatilia...

  Swali: NSSF ya sasa, hata kwa jina, ni tofauti sana na ilivyokuwa miaka ile
  wakati ulipoingia. Leo mna miradi mikubwa mnayoendesha, kama ya
  ujenzi wa majumba, ni ipi ya aina hiyo inayoendelea? Mna mingapi
  mingine iliyomo mbioni kuanza. Ni ya gharama gani?

  Dk. Ramadhani Dau: Miradi imegawanyika katika makundi matatu; ile iliyokamilika; inayoendelea; na kundi la mwisho ni la miradi ambayo tunatarajia kuianza.

  Tuliyokwisha kuimaliza ni jengo la ofisi la Mwanza (Sh. 12 bn), kuna jengo hili la Makao Makuu ya NSSF, lililokuwa Mafuta House, ambalo sasa ni Benjamin Mkapa Pension Towers (Sh. 23 bn); na kuna nyumba za Serikali ambazo zipo Kijitonyama (Sh. 13.8 bn). Kuna nyumba za Jeshi za Arusha na Dar es Salaam (Sh. 21.54 bn); kuna Hosteli ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sh. 16.4 bn) na nyumba za kupangisha za daraja la juu za Mikocheni, Dar es Salaam (Sh. 2.6) na jengo lililokuwa la Nasaco, sasa Waterfront; jengo la ofisi Mtwara; nyumba za bei nafuu za Kinyerezi, Dar es Salaam, Hospitali ya Mkuranga na majengo ya ofisi Nzega na Mafinga.

  Ukiacha hayo kuna jengo la Ubungo Plaza ambalo tumejenga kwa pamoja na Shirika la Nyumba (NHC) kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa Serikali na pia kuna ukumbi wa Bunge, Dodoma ambao tumeshirikiana na mifuko yote ya Pensheni nchini.

  Miradi inayoendelea ni ofisi za Bukoba zilizogharimu shilingi bilioni 2.88; jengo la ofisi Mbozi lililogharimu shilingi milioni 450; kuna jengo maarufu la Machinga la Dar es Salaam la gharama ya shilingi bilioni 12.41 litakalokwisha Desemba hii na jengo la Makao Makuu ya TAKUKURU la gharama ya shilingi bilioni 3.84.

  Kuna pia hosteli tano za Chuo Kikuu Kishiriki cha Sanaa na Sayansi ya Jamii cha Chuo Kikuu cha Dodoma za gharama ya bilioni 32; kuna nyumba za Jeshi la Polisi za Pemba, Unguja na Dar es Salaam na hosteli, madarasa, kumbi za mihadhara na majengo ya huduma nyingine za Chuo Kikuu Kishiriki cha Sanaa na Sayansi ya Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vya gharama ya shilingi bilioni 56.

  Hivi karibuni tutakuwa na majengo ya ofisi na vitega uchumi katika Mikoa ya Kigoma na Arusha na katika Wilaya za Kahama na Njombe; jengo la kitega uchumi la iliyokuwa AISCO Dar es Salaam, nyumba za kuuza za Mtoni Kijichi na Kigamboni na vilevile daraja la Kigamboni.

  Tuna mipango pia ya kuanzisha mradi wa ujenzi wa Business Industrial Park, ambayo uwezekano mkubwa ni kwamba tutajenga pale Kunduchi, Dar es Salaam kwenye eneo la machimbo ya kokoto. Wazo kuu la kuanzisha eneo hilo ni kwamba pale katika Jengo la Machinga, Karume, mtu ananunua viatu au soksi anakwenda pale anauza, ni shughuli za kununua na kuuza.

  Pale Kunduchi tunataka kiwango kipande, badala ya kununua na kuuza, wawe na uwezo wa kuunda vitu. Kwa mfano, ananunua soli na ngozi anaunda kiatu. Ananunua mbao anapiga randa anaunganusha meza, anauza, na kwa maana hiyo, anaweza kuwa na watu wengine wawili au watatu. Sisi tutatoa huduma za maji, na miundombinu nyingine pamoja na majengo yenyewe.

  Endelea mwenyewe.....

  Raia Mwema - Dk. Dau: NSSF inastawisha maendeleo

  Maoni yangu...kwa Haya machache waliyoyafanya NSSF ni mambo mazuri na ni ya kupongezwa na kutiwa nguvu ili waweze endelea na kuwekeza ktk Vitega uchumi vya mda mrefu.

  Binafsi yangu, ujenzi wa Nyumba TZ umekuwa Hovyo MNO, kwa style ya NSSF ya kujenga nyumba za bei nafuu ni jambo ambalo lingekuwa vyema likawa so tu NSSF, bali unakuwa mpango wa serikali nzima. Hili lingepunguza Ujenzi wa Mabondeni, na Ujenzi wa kiholela usio ktk Master Plan ya Miji.

  Last natoa Pongezi kwa Dr. Dau na wengine wote wanaosimamia maendeleo huko NSSF... Usikate tamaa wala usikatishwe tamaa...Kama mie ningekuwa mshauri wako, basi Uwekezaji wote ungekuwa ktk REAL Estate... nchi nzima...Nchi ingependeza. na Inalipa sio SIRI..!!!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mtu akikuibia ng'ombe na kesho yake akaja kukuuzia ng'ombe huyo na unajua ni ng'ombe wako utampongeza kwa kumlisha na kumtunza ng'ombe wako? Je utamnunua?

  NSSF imehukumiwa katika ripoti ya vifo vya Tabora na inashangaza huyo mwandishi hakumbana Dr. Dau kuhusu hilo. Maendeleo ya vitu ndiyo wanaendeleza lakini maendeleo ya watu (watoto 19 kufa) NSSF haistahili pongezii yoyote zaidi ya kufikishwa kizimbani na kuwawajibisha kuanzia na Dr. Dau, mama Nyoni, NSSF Tabora n.k. Hakuna cha kupewa pongezi hadi watakapokubali kuwajibika kutokana na vifo vya watoto wa Kitanzania 19, ukitaka kumpa pongezi ya majengo.. please go ahead, miye nawapa lawama ya maisha na roho za watoto 19!
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..waangalie uwezekano wa kujenga office/business complex maeneo mengine ya dar-es-salaam. kila mwananchi analazimika kuja city center, WHY?
   
 4. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unayesema NSSF wawekeze kwenye majumba tu umenishangaza sana!

  Ni lazima tujue kuwa NSSF zile hela wanatushikia tu sisi (wafanyakazi) - NSSF hawana tofauti na benki au bima za maisha. Ni lazima kuna siku inabidi wazirudishe tena kwa faida kwa wenye nazo - hasa wanapokuwa wamstaafu. Kwa hiyo ni muhimu mno kwa NSSF kuwa makini na vitega uchumi vyao! Kujenga majumba na madaraja (kigamboni) ni kuweka rehani vibaya hela za watu! Labda wawe wamefanya upembuzi yakinifu wa kutosha!

  Watu wengi wanachanganya makato ya NSSF na PAYE ya TRA! PAYE ni kodi (si mali mkatwaji) lakini NSSF ni hela binafsi za mkatwaji asiliamia 100% wala sio za serikali! Serikali ina mkono kwenye pension funds kwa ajili ya kutulindia pesa zetu na wala sio kuzitumia au kuzifanyia maamuzi! Nchi nyingi ulaya nk pension funds zao ni binafsi (privately sponsored) na watu wanahiari ya kuchagua ama kuweka pesa kwa hizo pension funds au kakata bima za maisha! TZ tunalazimishwa kuweka hela NSSF, PPF, PSPF, LAPF, ZSSF, GEPF! KIbaya sana ukifika uchaguzi mkuu serikali inawaambia hao wakurugenzi wa hizo pension funds kununua majumba ya akina Manji (Quality industrial Business Park, Quality plaza nk) kwa bei mara kumi ya bei halali!!!!! Kwa namna hiyo wanachukua hela zetu kwa mlango wa nyuma!!!

  Siku nyingine wakiamka (serikali) wanawaambia jamaa (akina Dau na wenzake) chukua hizo hela jenga daraja la Kigamboni! (wanataka kumaintain jimbo kule). Wanasema malizia Mafuta House (mkapa tower, sijui) hata bila kufanya upembuzi yakinifu!!! Jenga soko la wamachinga!!!!!! Nenda kajenge majengo lukuki chuo kikuu dodoma - halafu credit inakwenda kwa Kikwete - yeye alichofanya ni kuwaamrisha jamaa wakajenge kwa hela za watu! Jenga mabweni ya UDSM mabibo (big brother)! Jenga jengo jipya la kisasa la Bunge dodoma! Kopesha Kagera sugar mabilioni! By the way, katika nyumba za serikali za Dodoma (Area C nk) NSSF walijenga zaidi ya nyumba 250! Na mengine mengi!

  Sikatai majengo yanapenzesha miji, lakini leo hii wangekuambia wewe ukatwe mshahara wako wapendezeshe miji na credit apate Dau au serikali ungeona sawa! Kibaya zaidi ni pale wewe unapokuwa huna hata nyumba ndogo! Afadhali hata wachukue mshahara wawekeze diligently! Lakini kwa holela hivi! Trust me, pamoja na kwamba unaona hela za NSSF nk zinatumika vizuri kujenga majengo unayoyafahamu, yawezekana pia kuwa zile private villas kule masaki, oysterbay nk zimejengwa kwa hela hizohizo (10% nk). Na hapa sisemi NSSF (Dau) tu nina maana pension funds zote! Tuendelee kufurahia hayo ma villa ya wenyewe kwa mtindo wa kula ugali kwa picha ya samaki! Mimi nashakushauri kabla hutujapumbazwa (sio tusi) na majengo marefu yanayochipua kama uyoga tujiridhishe kuwa mahesabu yanabalance vizuri!

  Ukisema real estate ni investment nzuri unaweza kusema ni namna gani leo hii kama wachangiaji wa PPF au NSSF au PSPF au LAPF wakiachishwa kazi watapata fedha zao ili wasife kwa kukosa mshahara? Una maana zitauzwa PPF Tower, Ubungo plaza nk ili kuwalipa? Nani atanunua majumba kama kwa harakaharaka TZ? Hivi unajua return ya real estate Tz? Hivi unajua capital growth ya real estate Tz? Nenda hata kwenye annual reports za NSSF uone kama hata wamekuwa wakipata a +real return kutoka kwenye hayo majumba! Ni hasi (-) kwa miaka mingi tu! Wanasema majumba yana appreciate value, waulize wakutafsirie kwa US dollars uone kama zinapanda kama wanavyosema! Kwa sababu ya liquidity problem (sijui kiswahili chake) ndio maana serikali ikatunga sheria kulinda hizo pension funds kuwa hata mfanyakazi akiachishwa kazi asipewe hela mpaka afikishe umri wa kustaafu!! Haya ni maajabu! Unakufa kwa umaskini (pressure au magonjwa yanayotibika) wakati hela zako zipo kwenye matofali ya nyumba za NSSF na wenzie!

  I beg to differ! Real estate kwa mtindo wa uwekezaji wa pension funds za Tz (hasa NSSF) ni kichaka cha kuibia pesa - (money laundering)!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Turudi nyuma kidogo.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hongera NSSF chini ya uongozi mahiri wa Dr. Ramadhani K. Dau;

  Hivi kina PPF chini ya Erick Urio wanafanyaga nini na mabilioni ya fedha ngono??

  Hivi kina PSPF, LAPF, NHIF, GEPF etc wanafanyaga nini na hela zetu cha maana kwa jamii??

  Maana; mafao machache kulinganisha na NSSF, Kiwango cha malipo ya mafao ndogo ukilinganisha na NSSF ..

  What are they good at???
   
Loading...