Hivi muda wa kiongozi wa serikali, mfano waziri, kuruhusiwa kuwa on sick - leave ni muda gani? Au it remains kama discretion ya aliye mteua? Huyu ni mchumi mzuri sana, a Toronto PhD, na ile wizara ilimfaa sana. Lakini kama ni mgonjwa, apumzike tu kwani ile wizara ni kiungo muhimu sana cha uchumi wetu. Chami bado ana umri mdogo, akipata nafuu au kupona, atarudishwa tu kwenye baraza la mawaziri kwani wataalam wa aina yake miongoni mwa wabunge, sio wengi sana. Na pengine hii itampa nafasi Migiro kuwa waziri pale viwanda kwani kwa CV yake ya sasa, hawezi kupewa wizara ndogo ndogo, ni aidha Viwanda, Fedha au Foreign Affairs.
Thank you very much... umeweka hoja ya msingi sana, ila sidhani kama watakujibu wahusika, kwani tumempa madaraka makubwa sana presidaa kufanya atakacho, labda tuende study tour kenya
Maskini mbunge wangu! Nakuombea kwa Mungu upone ili uje utengeneze barabara yetu ya Kishumundu, imeharibika kishenzi lami yote imebanduka.Ni kweli Dr Chami ni raslimali muhimu nchini na umri wake unampa nafasi ya kuitumikia nchi muda mrefu, tumuombee apone haraka aendelee na majukumu yake. Najua ni mmoja (kama sio peke yake) wa wapiganaji hodari-alipambana kutoa msukumo sana serikali ikubali matumizi ya makaa ya mawe ili kupata suluhisho la kudumu la tatizo la Umeme vs majenerata ya mafuta*
Kwa ukubwa wa baraza letu la mawaziri, ni heri wapumzishwe lakini wasiteuliwe wa mbadala. Kama kipindi chote wanaumwa kazi ziliendelea kama kawaida, hii inathibitisha kutokuwepo kwao hakuna madhara yoyote. Kwa hali tuliyo nayo kiuchumi, kimefika sasa kipindi tupunguze gharama za kuendesha serikali kwa kupunguza wingi wa mawaziri tulio nao.Mawaziri watatu kutokuwa active ni pengo kubwa sana.wapumzike ili kuweka sawa afya.tunawatakia heri.