Dk. Chegeni|Mgeja|Chizi wajitosa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Chegeni|Mgeja|Chizi wajitosa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 25, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumamosi, Agosti 25, 2012 06:43 Na Waandishi Wetu, Dar na Mikoani

  HARAKATI za kuwania uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeshika kasi baada ya makada wa chama hicho, kuendelea kujitokeza kuchukua fomu.

  Uchaguzi wa ndani wa CCM, umewaibua makada wa chama hicho, akiwemo aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Misungwi Dalali Shibiriti ambaye amechukua fomu ya kuwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) kupitia wilaya hiyo.

  Akizungumza na MTANZANIA, baada ya kuchukua fomu hiyo Shibiriti, alitamba kuibuka kidedea huku akiahidi kuzaliwa upya kwa CCM Misungwi.

  Wakati Shibiriti akichukua fomu, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), jimbo la Busega umemshinikiza aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni achukue fomu za kuwania kiti cha Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC), kupitia wilaya ya Busega.

  Vijana hao, ambao waliongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Busega, Samwel Ngofilo walimchukulia fomu na kumpelekea Dk. Chegeni nyumbani kwake kwa maandamano.

  "Dk. Chegeni ni mwana Busega wa kweli, akiwa mbunge alifanya kazi kubwa katika kulijenga jimbo letu, tuna hakika atatusikiliza kilio chetu na kujaza fomu tuliyomchukulia na kuzirejesha kabla ya muda kuisha kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi,” alisema Ngofilo.

  Mgeja aibuka kutetea nafasi yake

  Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja amewataka wanachama wa CCM, kufanya uchaguzi wa kistarabu, badala ya kupakana matope .

  Mgeja aliyasema hayo jana, baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa mara ya pili.

  Aliwataka wagombea wenzake watakao chukua fomu kufanya uchaguzi, bila malumbano na badala yake wajenge hoja ambazo zitakuwa hazina madhara kwa chama hicho.

  “Ndugu zangu, chanzo cha makundi ndani ya CCM ni mpasuko unaosababishwa na uchaguzi nawaomba wenzangu tuwe wastarabu.

  Matson Chizzi

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) makao makuu, Mattson Chizzi amejitosa kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar e Salaam.

  Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Adam Makulilo aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana kuwa Chizzi alichukua fomu za kugombea nafasi hiyo na kufanya wagombea wa nafasi hiyo, hadi sasa kuwa sita mpaka kufikia jana mchana.

  Wengine waliochukua fomu, ni Mwenyekiti wa sasa John Guninita, Ramadhan Madabida ,Omary Kimbau, Isaya Christabera na Rashidi Kakozi.

  Katika hatua nyingine, mgombea wa nafasi ya Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa, Amos Kabis amesema endapo atachaguliwa kushika nyadhifa hiyo atahakikisha anawasimamia viongozi wa serikali katia kutekeleza ilani ya chama hicho.

  Katika hatua nyingine,jumla ya wagombea zaidi ya ya 41 wamechukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika kinyang’anyiro hicho, huku uchukuaji ukitarajia kufungwa Agosti 29, mwaka huu.

  Habari hii imeandaliwa na John Maduhu, Mwanza, Neema sawaka, Shinyanga na Simon Nyalobi, Dar es Salaam

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa wanaiomba maiti damu. Ina maana hawajagundua CCM iko mochuari inasubiri siku ya mazishi?
   
 3. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  .................walale mahali pema peponi, na wapumzike kwa amani!
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi kumbe nafasi ya ukatibu itikadi,siasa na uenezi ni ya kugombea?au ni ngazi ya mkoa na taifa ni mteule?
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wote wachumia matumbo tu hao!
   
 6. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  njaaaaaaaaaaaaa
   
 7. L

  Lyogohya Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wenyewe wanasema nzi hufia kwenye kidonda, wamigeuzakeki yetu ya taifa kuwa kidonda.
   
 8. a

  andrews JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kitendo cha waislamu kugomea sensa ni rais wa tz ndiye wa kulaumiwa sababu sheikh ponda ni muumini mwenzake rais na anashindwa kuwachukulia hatua kama alivyofanya kwa mgomo wa madaktari na walimu huu ni uzembe na udhaifu wa kikkwete kama rais anaweka dini mbele kuliko taifa anaamini katika hilo ushahidi upo mwingi.na kama taifa hili litaingia kwenye vita ya kidini kiongozi atakayebeba mzogo huu ni jakaya kikwete.kama angelikuwa ni mchungaji mtikila kasema wakristo wasusie sensa basi manyang'au wa usalama wa taifa na polisi wangeshamuweka ndani mtikila sasa kikwete acha udini na ongoza taifa kwa misingi ya uongozi na si vinginevyo ubaguzi wa kidini utazikwa nao hata ukienda kaburini maan wewe ndie muanzilishi n​a unaendekeza.
   
Loading...