Dk Bashiru: Tukishindwa kusimamia haki mtutose

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Dk Bashiru: Tukishindwa kusimamia haki mtutose

Moro/Dar. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema kama chama hicho kitashindwa kusimamia haki na kuwapatia maendeleo wananchi ni bora wakakitosa katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na hakitakuwa na haki ya kuongoza nchi.

Amesema CCM inapaswa kusimamia misingi ya haki na usawa kwa wananchi na kama ikishindwa kufanya hivyo ni wazi kwamba itatetereka na kukumbatia watu wanaotenda dhuluma.
Dk Bashiru alisema hayo jana akiwa wilayani Kilosa wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa za wilaya na Mkoa wa Morogoro, pamoja na wananchi wa kata tisa za wilaya hiyo.
Kauli hiyo ya mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ameitoa ikiwa zimepita siku chache tangu baadhi ya wabunge wa upinzani kuitaka Serikali bungeni kuruhusu mikutano ya hadhara ili wajiandae na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika mkutano huo, Dk Bashiru alisema CCM ya sasa inawasikiliza wananchi na kuwatetea katika kila nyanja, hivyo kama itashindwa kusimamia hayo ipasavyo haitakuwa na haki ya kuongoza.

“Uchaguzi unakuja wa serikali za mitaa, ni bora tukapigwa katika chaguzi kama tutashindwa kusimamia misingi ya haki na usawa kwa wananchi wetu, lakini naimani wananchi wetu wana imani na chama katika kuwatetea,” alisema.
Alisema kazi ya CCM sio tu kupigiwa kura, bali ni pamoja na kusimamia masuala mbalimbali ya utawala bora, siasa na hata maendeleo kwa wananchi na kwamba ikishindwa kufanya hivyo hakutakuwa na sababu ya kuongoza nchi. Alisema katika chaguzi zinazokuja, ni lazima wachaguliwe viongozi wenye uwezo wa kusimamia haki na masilahi ya wananchi kuliko wale wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Dk Bashiru alisema kwa sasa kila mwenye mali ni lazima ijulikane alizipataje na iwapo ni kwa njia ya halali ataeleza hata kama ni mtu mwenye utajiri wa namna gani.

Alisema watu wote wenye utajiri usioeleweka namna walivyoupata hawatatoka salama.
“Nimesikia watu wakinong’ona kuwa nakuja kila mara Kilosa, hii Kilosa ndiyo inaongoza kwa migogoro ya ardhi, hivyo kupitia CCM ujumbe huu wa haki na usawa katika ardhi utafikia nchi nzima kupitia wilaya hii ya Kilosa na ndiyo naifanya kama mfano.”

Awali, katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka alisema wapo baadhi ya viongozi siyo waaminifu na hawana nia njema na chama hicho wakikitumia kama mwamvuli wa kufichia maovu yao na mkoa wake umejipanga kuwafichua.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoi alisema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na ile ya siasa tayari wameshawabaini baadhi ya viongozi wanaosababisha migogoro ya ardhi kwa kuiuza kinyume na taratibu.

Alisema wamepanga kuanza kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya dola.
Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema kuwa amemsikia Dk Bashiru na kumtaka kama ni mkweli na ana dhamira ya anachokisema aanze na Spika wa Bunge.

“Kutetea wananchi ni pamoja na kuwapa wanachokiamini (kuwa) kipo sahihi ikiwamo Katiba mpya waliyoitolea maoni kwa miaka miwili,” alisema Mrema.

Mrema aliungwa mkono na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT - Wazalendo, Ado Shaibu aliyesema anafuatilia ziara za Dk Bashiru aliyewahi kumfundisha, lakini akasema kwamba haamini kama yote anayoyazungumza anafanya hivyo kwa dhati na hakika.
Alisema Dk Bashiru anazungumzia masilahi ya wakulima na wafanyakazi ilhali viongozi wenzake ni watu wa vijembe na siasa zisizoeleweka na kwamba kukosa uwiano huko ni dalili kwamba anayoyasema ni hadaa.

Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi alisema hashangazwi na kauli hizo na kwamba ni aina ya siasa za CCM unapokaribia uchaguzi, lakini akadai kuwa wananchi wanaosemwa kuwa ni wanyonge wanaotaka kuwasaidia, hawapati misaada hiyo zaidi ya wale wa mjini.
 
Nchi ya Propaganda kwa 100%

Kwanza haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaotaka haipo - Wizi wa kura na hakuna kukaa mita 200

Pili - Hakuna haki ya kupata mafao yanayostahili - Serikali ya CCM inadaiwa Trillioni 4

Tatu - Wamefyeka FAO LA Kujitoa

NNE- Ukiacha mwenyewe hupati mafao (Sheria zao mpya)

5 - Marufuku kuhoji matumizi ya kodi tunazolipa - Rejea sakata la CAG

6 - Wafanyakazi hakuna nyongeza mshahara

Bashiru..Wewe ni kipofu?

Mwambie Mwenyekiti aisee
 
Maneno ya Dr bashiru ni ya ajabu kwani kuna kila dalili kurudi katika maisha ya ujamaa kama ilivyokua katika utawala was ml nyerere ndiko tunakorudi ni mbaya sana tunapotezwa badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakika mmeshindwa, iko wapi haki ya watumishi ya annual increment na madaraja, hakika mnaboa sana, mnaona masilahi yenu na chama ni bora zaidi kuliko wananvhi, hakika hiki chama kimekosa utu, Eee Mungu utusamehe waja wako kuzaliwa katika taifa lililolaaniwa

MBONA TAYARI MMESHASHINDWA...MUONDOKE TU
 
Yule wa Sudan Leo kapelekwa jela ile ile aliyokuwa akiagiza tu "weka ndani "wapinzani wake.Saddam alinyongwa na jaji yule yule aliyekuwa akimuamuru kuwanyonga wapinzani wake,yule wa Romania alipigwa risasi adharani wote na mke wake na askari wale wale aliokuwa anawaagiza kuuwa watu.Kiongozi wa kiafrica ni sawa na kenge hawasikii hadi siku wakiokotwa kwenye makaravati.Kanuni ya kifo inasema ukiuwa wenzio ni lzm nawe utauwa.Dikteta hana heshima ya mwisho mwema.
 
Maneno ya Dr bashiru ni ya ajabu kwani kuna kila dalili kurudi katika maisha ya ujamaa kama ilivyokua katika utawala was ml nyerere ndiko tunakorudi ni mbaya sana tunapotezwa badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ujamaa ujima backwardness utaendelea kuwepo hadi hichi kizazi cha Nyerere kipite.
 
kwa hiyo uchafuzi huo wa serikali za mitaa mkishajitangaza washindi mtasema mnakuballika?bwana bashiru unaikumbuka hii kauli?YAANI WEWEMKURUGENZI NIKULIPE MSHAHARA,NIKUPE GARI NA NYUMBA HALAFU UNAMTANGAZA MPINZANI MSHINDI?

Wakati mwingine huwa zinarudi watamfukuza achunge,ccm mpya kusema ukweli ni mwiko wwe ni sawa na muhaini
 
Back
Top Bottom