Dk. Bashiru Ally : Siku hizi wapiga kura wamekuwa na tabia ya kukaa nyumbani, wanaona ni kituko na mchezo wani mchezo wa kuigiza

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,317
2,000
"Sasa wapigaji kura wajanja wa Tanzania wameanza tabia ya kudharau uchaguzi,” alisema Dk Bashiru mbele ya wakulima waliofurika kwenye ukumbi huo.“(Wameanza tabia) Ya kukaa nyumbani kwa sababu wanaona ni kituko, ni mchezo wa kuigiza. Ndio maana leo kupata watu kwenda kupiga kura imekuwa shida. Note (angalia), tunakoshinda ni chini ya asilimia 30, chini ya asilimia 40. Hakuna mahali ambako wapigajikura wamejitokeza kwa asilimia 50," alisema Dk Bashiru."Na mwaka 2010 ulitia fora. Watu wengi walijiandikisha, kumbe walikuwa wanataka kile kiparata (kitambulisho cha mpigakura), kwa sababu kinatumika kwenda polisi kudhamini, kujitambulisha.

“Walipokipata wakaingia mitini. Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii tulipata Serikali ambayo haina uhalali wa kisiasa kwa sababu wapigajikura wengi zaidi ya ailimia 50 walibaki nyumbani. Tatizo hili halijaisha, lakini wanasiasa wakishashinda, wanasema ameshinda hata kama ni kura moja. Hajali kwamba ushindi ule unatakiwa uwe na uhalali."Alisema mfumo wa uchaguzi nchini umegubikwa na rushwa kiasi kwamba imefika mahali ambapo ukifika uchaguzi wagombea wanauza nyumba.
“Usipomchangia, anakuwa mkali utafikiri anakwenda kutibiwa,” alisema.

"Akishazikusanya fedha anakwenda kuwanunua wale mawakala na mawakala wanajua. Nao wanawanunua wapigaji kura. Msimu wa uchaguzi unakuwa msimu wa rushwa ya uchaguzi. Mnachotakiwa kufanya ni kubomoa na kuharibu soko la kura."Alisema eneo jingine ambalo wanaweza kulitumia ni kuwawajibisha wote wenye vyeo kwa kuwa ni vya wananchi.
“Msichague kiongozi kwa T-shirt (fulana), kofia, kwa ubwabwa na kwa pesa. Kwa kufanya hivyo mnatengeneza watu wanaokuja kuwaonea,” alisema.“Kwa sababu mamlaka ya Serikali yanatoka kwa wananchi. Vyeo vyote vilivyoko serikalini ni vyenu. Isipokuwa kuna mchakato wa kusimamia vyeo vyenu na moja ya michakato hiyo ni uchaguzi."Hebu tujiulize. Tabia na mwenendo wenu katika uchaguzi ukoje? Tuambizane ukweli, Mkishapewa kofia na T- shirt, halafu nyimbo zikaanza kupigwa za mbele kwa mbele, huwa mnahoji sifa ya mnayetaka kumchagua? Je, sifa ya chama kinachopiga mbele kwa mbele mnaijua?"Kwa sababu dhuluma zote hazifanywi na wakoloni, bali wale mliowachagua.Kuhusu masuala ya ushirika, Dk Bashiru alishauri wakulima kuunda ushirika wenye nguvu ili wawe na nguvu ya kuiwajibisha Serikali na kutetea masilahi yao.
Dk Bashiru alisema wakulima wanapaswa kuanzisha ushirika utakaowatetea katika masuala ya ardhi, mikopo na masoko."Tuwe na Ushirika wa wananchi kudai haki za msingi kama ardhi. Kataeni kuuzwa kwa ardhi kama mnavyokataa kuuziwa damu. Tangu nimeingia ofisini, asilimia 99 ya malalamiko ni ya ardhi. Wengi ni masikini, matajiri wanakwenda wizarani. Mtafanywa watumwa kwenye ardhi yenu,” alisema.
 
CaptainDunga

JF-Expert Member
Jul 17, 2009
1,559

Uchaguzi ujao.......Mwenyezi Mungu akinijaalia uhai wala sita hangaika kupanga foleni ili nipige kura.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,744
2,000
Unaendaje sasa munachagua mnayemtaka
Lkn wanamtangaz wanaye mutaka wa fisiem bora kuacha tu ,amini usiamin hii nchi mkate utauzwa 15000
Gun itauzwa 1000,hapo ndipo utajua vita ni vita
Na majigambo kibao, tumeshinda ushindi wa kishindo cha tsunami
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,125
2,000
Tunaowapigia kura kwa wingi na kwa uhakika tunajua wameporwa ushindi wanapewa wengine ambao tuna uhakika kabisa hawakushinda, tutapata wapi moyo na imani ya kwenda kupiga kura wakati 'watu' tyr wana mtu wao mfukoni?
 
Bin Chuma

JF-Expert Member
Dec 13, 2013
298
250
Dr usilaumu wananchi kutokupiga kura, pigania kwanza mfumo wa upigwaji kura uwe wa haki(najua hautaweza). Maana ya kupiga kura ni kushindanisha wagombea kutokana na sera zao, lakini kama kabla kura haijapigwa tayari mshindi anasubiri kutangazwa tu, hiyo sio kura. Wananchi wameelimika Kwa sasa na wanaendelea kuelimika zaidi. Huwezi “kuwadanganya watu wote kwa muda wote” ila utawadanganya watu wachache kwa muda fulani tu”.
 
Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,328
2,000
Ukiambiwa CCM wana sera mbaya kataa kama Ukoma!.
Ukiambiwa CCM ina watekelezaji wazuri wa sera yao kataa kama Ukoma!.
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,375
2,000
Look who's talking!
Hata mimi sizani kama nitapiga kura 2020
Mtakuwa mmetimiza lengo la bashiru,maana porojo zote hizo na kuwapa jina zuri la "wapiga kura wajanja'"ni ili wasijitokeze kupiga kura,kwenye upinzani watu wanahamasishwa wasijitokeze ila huko dodoma watu hadi wanafuatwa majumbani na kubebwa kwa ma Fiat 682 torino!! Ila arusha polisi wanamwagwa kila kona ili kuwatisha watu wasiende kupiga kura!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom