Dk 45 ITV J3 Warioba Kunguruma

Dk 45 ITV J3 Warioba Kunguruma

matasha

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
378
Reaction score
400
Msikose kipindi cha dk 45 itv kesho j3 saa tatu usiku ambapo jaji warioba atanguruma kuhusu mchakato wa katiba
 
Karibu. Ila we ndio producer wa kipindi au? Samahani lakini.
 
Msikose kipindi cha dk 45 itv kesho j3 saa tatu usiku ambapo jaji warioba atanguruma kuhusu mchakato wa katiba

Nakisubiri kwa hamu sana! Tatizo la Dk 45 muongozaji wake hana weledi wa kuuliza hard questions. Nitakiangalia simply ni Judge Warioba vinginevyo ni kipindi ambacho huwa sikiangalii kabisa.
 
Big up! Yaani wananchi msikae mbali na runinga zenu ili mpate kumsikia na kuchuja ili hatimaye msifanye maamuzi kwa kushinikizwa.
 
TaanenskoCcM watakata umeme

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Warioba ni moja ya mipini bora kabisa ya TANGANYIKA bora uhojiwe kuliko majembe ya xxm kwani yana tundu la kuingizia mipini kama Lissu.
Live Long Life Warioba
 
namuomba Warioba asikose kuelezea kama tanganyika iliungana na zanzibar kwanini bado zanzibar ipo tanganyika isiwepo kama hofu kwamba zanzibar ingepotea kwani nbona bado tunaita mzanzibar,mpemba na bado tuna tanzania na mtanzania kwani tunaposema mpemba sio mtanzania?sasa inashindikanaje kusema Mtanganyika? mimi nadhani hakuna haja ya kuogopa kusema mtanganyika hii ni kuonyesha tu,kwamba mtu huy katokea upande gani wa Tanzania kama ilivyo kwa mtanganyika anavoeleweka ametoka upande gani wa tanganyika aidha dar,kigoma mara morogoro tabora mwanza N.k
 
Tv zingine siku hiyo zitakosa watazamaji chezea ITV wewe

Yaani mie hapa niko soko kuu nachagua Generator nzuri kwa ajili ya moto,maana najua TANESCO watakata umeme iwe isiwe.Nikimaliza kuangalia kipindi nitaitunza tena kwa ajili ya kusubiri mikutano ya UKAWA huku bara,mbona raha.
 
Naomba wadau wenye mawasiliano ya moja kwa moja na mh. Jaji Warioba pamoja na waendeshaji wa kipindi naomba wajikite ktk kufafanua hoja zinazojengwa kupinga muundo wa s3 hususan gharama za kuendesha serikali 3 ukilinganisha na hizo s2, pili jambo la serikali ya muungano kuelea na hofu ya muungano kuvunjika na jeshi kuchukua nchi katika s3.
 
Yaani mie hapa niko soko kuu nachagua Generator nzuri kwa ajili ya moto,maana najua TANESCO watakata umeme iwe isiwe.Nikimaliza kuangalia kipindi nitaitunza tena kwa ajili ya kusubiri mikutano ya UKAWA huku bara,mbona raha.

Umesikika ngoja niweke mafuta generator langu likae standby wakikata tu linajiwasha.
 
Yaani mie hapa niko soko kuu nachagua Generator nzuri kwa ajili ya moto,maana najua TANESCO watakata umeme iwe isiwe.Nikimaliza kuangalia kipindi nitaitunza tena kwa ajili ya kusubiri mikutano ya UKAWA huku bara,mbona raha.
Mkuu kwani UKAWA hawatarudi bungeni?
 
Msikose kipindi cha dk 45 itv kesho j3 saa tatu usiku ambapo jaji warioba atanguruma kuhusu mchakato wa katiba

Asante mtoa taarifa. Namwamba mwongoza kipindi aandae maswali mapema na sio maelezo ili amwache one of Titans of Tanzania atoe elimu tosha. Dakika 45 ni kipindi kifupi mno kwa mtu kama Warioba maana anayo mengi yakutueleza ambayo yamepotoshwa. Mwongozaji ajiepushe kuwa kama Makwaia wa Kuenga ambaye huwa yuko biased na hutumia muda mwingi koungea yeye badala ya anayehojiwa
 
Mimi nadhani Warioba angekaa kimyaa sasa. Kazi yake na tume imeshakwisha. Atuachie sisi tufanye yetu na maamuzi.
 
Back
Top Bottom