Diwani wa CCM Nzega atimkia CHADEMA

Diwani wa CCM Nzega atimkia CHADEMA

afsa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
1,986
Reaction score
1,592
Joseph K. Malongo ni diwani aliyemaliza muda wake kwa tiketi ya CCM. Ametubu. Ameziacha dhambi zake. Amehamia CHADEMA.

Ni diwani wa kata ya Nata - jimbo la Nzega, amehama na kundi kubwa la wanachama akiwemo mchumi wa CCM kata na aloyekuwa m/kiti wa nata.

Tumewakaribisha, Tumewasamehe dhambi zao. Tunaendelea na ukombozi.
attachment.php
 
Attachments

  • 1437041891982.jpg
    1437041891982.jpg
    36.7 KB · Views: 2,147
  • 1437041927748.jpg
    1437041927748.jpg
    43 KB · Views: 2,075
  • 1437041954830.jpg
    1437041954830.jpg
    27.7 KB · Views: 8,519
Hongereni sana nyie kwanza,lakini pia hongera zao hao kwa kujitambua.Kuwa Ccm ni mzigo mkubwa sana moyoni mwako kwa sababu una unakisaliti kizazi chako!.Karibuni kwenye ukombozi Makamanda
 
Mamluki haooo, naona EL ameanza tuma chambo
SINA IMANI NA UKAWA
 
karibuni sana huu ndiyo mda muafaka wakuipenda nchi yetu!!!
 
ukipiga goti na ukakir mwenyewe mbele ya umma ule unyama uliowateendea raia wenzio bila shaka utasamehewa .
 
Njia raisi ya kuua mti ni kuanza na mizizi au kuchuna magamba ya shina..
 
Mbona wana matumbo makubwa hivyo??
Waambie chadema hatutaki rushwa hata wenyeviti wa mitaa mambo ya barua kukogonga muhuri kuwa 5000 tushakataaa
Kama wanaweza wakaribishwe

Ha ha ha! Indicator No. 1 ya mCCM kuwa na kanafasi japo kiduchu ni kuwa na tumbo linalokaribiana na tembo. Chunguza kwa makini utagundua mijamaa ilivyo na matumbo ya ajabu kuanzia na marehemu Komba na wengineo. Hopefully, akijiunga na makamanda atabadilika kwani hiyo sio sifa kwa wapiganaji.
 
Siasa mi siielewi kabisa....wakiwa CCM ni Mafisadi ,wakihama ni watu safi!Wanasiasa msicheze na akili za watanzania ipo siku ukweli utakuwa wazi na nyote mtaadhibiwa.
 
Siasa mi siielewi kabisa....wakiwa CCM ni Mafisadi ,wakihama ni watu safi!Wanasiasa msicheze na akili za watanzania ipo siku ukweli utakuwa wazi na nyote mtaadhibiwa.

Shangaa na hili mwanajeshi akiwa kwa waasi anaitwa MUASISI/GAIDI/HARAMIA ila akijiunga na jeshi la serikali kupiwapinga waasi ataitwa MWANAJESHI MTIIFU KWA NCHI YAKE...Ni hisia zangu umeelewa hata kidigo
 
Mbona wana matumbo makubwa hivyo??
Waambie chadema hatutaki rushwa hata wenyeviti wa mitaa mambo ya barua kukogonga muhuri kuwa 5000 tushakataaa
Kama wanaweza wakaribishwe

Kweli mkuu pia wapatiwe na msaafu kabisa
 
Hata mie nastaajabu haya ya Musa. hawa jamaa wa CCm wamekuwa wanapewa kila iana ya majina mabovu pamoja na ufisadi. Sasa wanatimkia Chadema wanaonekana lulu. Kulikoni, au huko Chadema hakuna sifa za kuwa kiongozi.
 
Joseph K. Malongo ni diwani aliyemaliza muda wake kwa tiketi ya CCM. Ametubu. Ameziacha dhambi zake. Amehamia CHADEMA.

Ni diwani wa kata ya Nata - jimbo la Nzega, amehama na kundi kubwa la wanachama akiwemo mchumi wa CCM kata na aloyekuwa m/kiti wa nata.

Tumewakaribisha, Tumewasamehe dhambi zao. Tunaendelea na ukombozi.
attachment.php

Kwenye dhehebu letu la kikristo sharti mdhambi kuzijutia dhambi na kudhamiria kutorudia tena, ndipo msamaha kamili kumfikia!
 
Back
Top Bottom