Diwani wa CCM Arusha aongoza maandamano kupinga posho za wabunge huku wamevaa magunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa CCM Arusha aongoza maandamano kupinga posho za wabunge huku wamevaa magunia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 21, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WANANCHI wa Manispaa ya Arusha, bila kujali itikadi zao za kisiasa, jana waliandamana kwa amani wakiwa peku huku wamevaa magunia kupinga ongezeko la posho za wabunge na kutishia kuandamana hadi mjini Dodoma iwapo Rais Jakaya Kikwete ataidhinisha ongezeko hilo.

  Wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wananchi hao walisema ni udhaifu wa Rais kukubali posho hizo zianzwe kulipwa kwa wabunge kabla hajasaini kama sheria inavyoelekeza na kumtaka kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika na ukiukwaji huo wa sheria za nchi alizoahidi kuzilinda katika kiapo chake.

  “Iwapo kweli tayari wabunge wamejilipa posho hizo bila Rais kuidhinisha na hadi sasa hakuna mtu amewajibishwa, basi atakuwa ameonyesha udhaifu mkubwa kiuongozi, tutaandamana nchi nzima kupinga posho hizi bila kujali itikadi zetu kisiasa,” alisema Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maandamano hayo, Mawazo Alphonce

  Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya maandamano hayo ya kilomita Saba, Mawazo ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wazalendo Associate ya mjini Arusha, na Katibu wake, John Mchasu walisema kitendo cha Spika wa Bunge, Anne Makinda kutetea posho hizo ni kielelezo cha ubinafsi unaoonyeshwa na viongozi nchini.
  “Spika kutetea posho hizo kuwa zitasaidia wabunge wake kuacha kuwa omba omba imetia doa nishani aliyotunikiwa na ni kielelezo cha ubinafsi na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwa kundi moja dogo kujihalalishia mgawo mkubwa wa keki ya Taifa huku kundi kubwa likibaki bila matumaini,” alisema Mawazo.

  Mawazo ambaye ni diwani wa Kata ya Sombetini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema Spika alipaswa kuwakumbuka na kuwazungumzia makundi mengine yanayotaabika kwa kipato kidogo na ugumu wa maisha kama walimu, wauguzi, madaktari na omba omba waliozagaa kila sehemu nchini, badala ya kutetea posho za wabunge wenye kipato kinachokadiriwa kufikia milioni 12 kwa mwezi.

  Alisema ubunge sasa siyo wito wala uwakilishi wa umma bali ni fursa ya kujitajirisha ndiyo maana siku hizi watu wanauza rasilimali zao kufanikisha kushinda ubunge na ndiyo maana wakishaingia bungeni wanaanza kutetea ongezeko la posho kama inavyoshuhudiwa hivi sasa.Alihoji uhalali wa wabunge kudai nyongeza ya posho wakati malipo yao kwa siku mbili ni zaidi ya mshahara wa mwezi mzima wa mwalimu na watumishi wengine wa kada ya chini serikalini.

  Alitaja baadhi ya ishara za ubinafsi na matumizi mabaya ya madaraka kuwa ni kitendo cha viongozi wengi, watoto wao, ndugu, jamaa na marafiki kuishi maisha ya anasa na ufahari mara tu baada ya kuingia madarakani akitoa mfano wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyoongoza kwa uadilifu kiasi cha kushindwa hata kujenga nyumba hadi alipojengewa na serikali baada ya kustaafu.

  Kuhusu kuvaa magunia na kutembea peku kwenye lami lenye joto kali mchana Saa 7:00, Mawazo alisema ni ujumbe unaowakumbusha jamii kusimama imara kupinga na kuzuia malipo ya kufuru na posho zisizo na maelezo ya kutosha na kuongeza kuwa katika siku zijazo hali hii ikiendelea maisha ya watanzania yatakuwa magumu na hawatamudu kununua hata nguo wala malapa kutokana na viongozi kujigawia keki yote ya taifa.

  Moja ya mabango yaliyobebwa na watoto walioshiriki maandamano hayo lilisomeka “Wakati wabunge wanadai posho zaidi, watoto hatuna madawati, tunakaa chini kwenye mavumbi hivyo tunalaani nyongeza hizo,”

  Diwani huyo ambaye kabla ya kuhamia CCM alikuwa katika Chama cha Tanzania Labour alikoshinda udiwani wa Sombetini alisema wako tayari kuandamana hadi Dodoma hata ikibidi kuuawa kwa kupigwa risasi kwani hata wakifa watafia ukombozi wa jamii iliyochoka kimaisha kutokana na viongozi wengi kujali maslahi binafsi badala ya umma wanaouongoza.
   
 2. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kuvaa magunia inamaanisha nini ?
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kwa desturi inaashiria kuomboleza.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi maziko ya CCM ni lini jamani maana naona kihi chama kimesha kufa......
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Good, Utaifa kwanza, Uchama baadaye...
   
 6. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuomboleza.CCM inaombolezewa maana imekwisha kufa yamebaki masalia.
   
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  kuomboleza kwa kuvaa magunia ni ishara kubwa sana kwa kati ya mungu na mwanadamu, taifa limepelekwa kusiko ee MOLA sikia kilio cha waja wako utawala huu uwe na hofu ya MUNGU.
   
 8. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  Ogopa sana kitu kiitwacho kuvaa magunia, maana kinaashiria maombolezo
  mbele za MUNGU ya hali ya juu sana. CCM wangekuwa wakijua maana yake
  wangeyapiga marufuku kabisa. Nilipoona jana ktk TV nikaona safari kubwa
  imeaanza, TANGU TUPATE UHURU SIJAWAHI ona waTZ wakilia kilio hiki.
  TAFAKARI: K
  UVAA MAGUNIA NA KULIA MBELE ZA MUNGU SIO KITU CHA KAWAIDA
  kuna kitu kikubwa kinakuja. TAFAKARI
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  safi sana bado maandamano ya wanachuo nchi nzima.
   
 10. n

  nyalufunjo Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona taabu sana pale ambapo mtaalamu aliyeteseka kwa miaka mingi kusomea kazi yake, na baada ya kupata ajira anaendelea kufanya kazi ngumu ktk mazingira magumu na analipwa kidogo na baada ya kustaafu analipwa mafao yasiyofaa kwa mda usiofaa baada ya kusota sana. Lakini mwanasiasa analipwa babu kubwa na mafao yake anapata kabla hajatoka kwa ofisi. Je tutafika? Ona sasa watoto wengi wanakosa motisha wa kusoma masomo ya SCIENCE! Je tutafika?
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Uzalendo zaidi ndo unahitajika ktk hili suala
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  CCM wanajua kucheza na vichwa vya watanzania
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ubinadamu kazi Mkuu!
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa nini awe diwani sasa hivi nasi lema (mbuge)? au amewageuka? nyie machalii wa arusha imekula kwenu. pole.
   
 15. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hali ngumu na duni... Yaani anawakilisha wenye kipato kidogo, wasio na hakika ya mlo wa kesho!
   
 16. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  huwaambii kitu na Lema wao! Pata historia ya Lema kabla ya kuwa mbunge kwa mkazi yeyote wa Arusha...
   
 17. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Well, a good question!
  Kuvaa gunia inamaanisha kwamba, Wananchi wamekata tamaa, na hawana matarajio na wamekosa imani na uhakika wa kesho yao. Inaashiria hawana uhakika kama kesho wataweza kupata kipaato na kununua nguo ya kuvaa na hivyo watavaa magunia, wanaonyesha namna ya nchi ilivyoshindwa kusimama na hivyo kuwa kama gunia, bila kulishikilia haliwezi simama. Gunia halina mawazo wala fikra, gunia ni tupu, gunia halifikiri na gunia halina maamuzi, kwahiyo waandamanaji wanawakilisha gunia na viongozi wa Tz, gunia halifuliwi, kwa hiyo gunia ni chavu na limechoka, hiyo ndiyo tanzania yetu. Tanzania ni gunia
   
 18. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,278
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Hii kilio Mungu ataisikia tu na atatujibu siku si mingi
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nasikia hii mbinu ya kuvaa magunia ibuniwa na Nape baada ya CCM kupoteza umaarufu Arusha, hivi washona suti au makombati.
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  machoko wabunge wa ccm ndio tatizo
   
Loading...