Diwani wa CCM akamatwa

KERO ZA KUTUMIA MADARAKA YA UMMA KULINDA MASLAHI BINAFSI ZITAISHA LINI????????

Waheshimiwa Mawaziri wetu mliotajwa humu, hapo penye wino mwekundu ndio kusema ya kwamba DHAMIRA YENU inawaelekezeni kabisa kutumia ofisi zetu hizo za umma kwa manufaa yenu binafsi kulinda MASLAHI BINAFSI hapa badala ya kutulindia sisi MASLAHI MAPANA YA UMMA ya kutokuongeza jangwa zaidi Same sio??????????

Wana-MAZINGIRA kote nchini tunasubiri sauti zenu katika kashfa nzito hii kwa mawaziri hawa wawili. Inamaana kivingine mawaziri hawa wanasema Tanzania itageuzwa jangwa kwa gharama yoyote ile hata kama ni Mkwewe Rais Kikwete kufyeka misitu yetu na kutafuna taratibu hazina yetu ya taifa kwa vizazi vya kesho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wana-JF tangu sasa tunfuatilia hiyo kesi na faili nyinginezo nyigi tu hapo Same kuhusiana na UHARIBIFU WA MAZINGIRA mpaka kuona mwisho wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Heshima kwa Wana JF, Diwani wa Viti Maalum ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Zaina Shahidi wilaya ya Same amekamatwa na magogo pamoja na Mbao aina ya Kenfa ambazo ni nyara ya serikali na Maafisa mali asili Mwanga Kilimanjaro kwa kushirikina na Polisi wa wa Wilaya ya Mwanga.

Sakata hilo lilijiri wiki iliyopita tarehe 25/08/2011. Habari zaidi zinasema kuwa Diwani huyo alipata tenda ya kuuza magogo kwenye kiwanda cha Kilimanjaro Biochem kilichopo Mwanga, Jitihada za kumtoa mahabusu Diwani huyo Maarufu (Mkwe wa Kikwete kwa Riz 0ne)zimegonga mwamba.

Habari zinazidi kumiminika kuwa Diwani huyo kwa kusshirikiana Katibu wa Uchumi na fedha wa CCM Mkoa wa kilimanjaro Bwana Mohamed Karia ndio wanaoongoza mtandao wa wafyeka misitu katika mkoa huu na wanakingiwa kifua na mawaziri David Mathayo na Ezekiel Maige.

Viongozi mbalimbali wa CCM wa wilaya za Same na Moshi walikuwa wakihaha kujaribu kutafuta removal order ili wamtoe gerezani Kiruru.

Mpaka sasa diwani huyo bado yupo gereza la Kiruru akisubiri sikukuu ya Iddi ipite ndo kesi yake iendelee
 
TANZANIA YETU WAZIRI HUJIUZULU TU AKITUHUMIWA KUBAKA MAMA YAKE SI MAZINGIRA

Kwa mataifa yaliostaarabika, kwa mtaji wa kashfa hii nzito mno kugusia uhai wa misitu yetu na baadhi ya mawaziri wetu kudaiwa KUSHIRI KUSHINDA JUHUDI ZA SERIKALI KULINDA mazingira, kwingineko huko duniani akina DAVID MATHAYO na ndugu yake MAIGE wasingelazimika kusubiri mpaka tuwasukume nje ndio wajiuzulu nyadhifa zao kwa kushinwa kutetea SERA za serikali wanayoitumikia.

Lakini hawa hapa pamoja na kuidhalilisha serikali kwa kashfa hii ya kujichagulia kulinda maslahi binafsi ya Diwani Fisadi Zaina na kutelekeza maelekezo rasmi ya kazi yao ya Uwaziri; Wa-Tanzania bado tutaendelea kuwaona tu watu hawa wakitia timu na kuendelea kukwepa vyombo vya habari vya nchini na kimataifa kila kona.

Na siku watakapobanwa kiuhakika kwenye kona basi mara utasikia wakitamka bila aibu yoyote: "Sitojiuzulu Ng'o sina kosa mie".
 
Mawaziri Mathayo na Maige watupe maelezo ya kina nini wanachokijua kuhusu ufyekwaji ovyo wa misitu yetu hadimu mikoa ya Kilimanjaro na hasa sehemu za Same na Mwanga.

Mama yetu Anna Kilango Malecela ni wakati muafaka kusimama kidete kama kawaida yako KUTETE MASLAHI YA UMMA hapa na wala usiwe kama hawa wanaotumia ofisi zao KUTETEA MASLAHI BINAFSI.

Waheshimiwa Mathayo na Maige; maelezo ya kina kuhusu misaada yenu kuchakaza misitu yetu Kilimanjaro na kwingineko wa si ombi bali ni wajibu we kwetu sisi wananchi pale tuhuma nzito kama hii inapo ibuka.

Ama kweli Nape Mnauye naona alisema yote kuhusu vyanzo vyote vya dhuluma nchini, kwa njia moja au nyingine, wananchi tutasikia ama mtoto wa waziri kahusika mara mtuhumiwa ni mtu wa karibu sana na mtoto wa rais ...

Jamani ni keeerrroooo kubwa CCM kurithishana uongozi wa taifa letu keeeerrrrrrrroooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii yanikumbusha wakati marehemu Ditto akiwa Ukonga JK would use the state motorcade and our money to visit the prison every night kusema na mshikaji wake mwisho kesi ikaenda kasi akatemwa na hili nalo naamini ni matter of time utasikia polisi wamechoka mno na kumwachia Mtanzania namba moja alie oza binti ukoo wa kifalme na mfalme Kikwete na hakutakuwa na zaidi .Maana ma CCM yanadhani ndiyo matanzania namba moja sisi ni second hand citizens
 
Hii issue ilivyotoka kwenye wizi wa nyara hadi kuingizwa Ridhiwani imenitoa jasho. Mtoa taarifa kuna wakati unaweza kuinyima taarifa credibility bila sababu yeyote mi sioni jinsi ulivyomwingiza huyo kijana na kifalme katika hilo sakata kama ni sahihi kama ni kweli ni tukio la ukweli.

Labda kama ni kweli wana uhusiano basi hiyo ilipaswa kuwa habari nyingine kabisa inayojitegemea kwa ushahidi wake. Maana unaweza kutumia ushahidi wa kukamatwa kwa Diwani kwa wizi wa nyara za Umma kuwa ushahidi wa Ridhiwani kuwa na uhusianao na huyo mtuhumiwa kitu ambacho hakitoshelezi kuwa ushahidi unajitegemea.
 
Laiti kungaliku na uwezekano kuazima sheria nyingi za wenzetu Wachina za kuhakikisha uadilifu kwa viongozi, nadhani Tanzania huenda viongozi wetu 'Tungewanyonga' wengi sana kwa zaidi ya asilimia 90 % kwa kuwa uadilifu nchini ulizikwa siku moja pale alipozikwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kule Butiama.

Na wale wote wanaomkingia kifua kwa kigezo cha "mkwe"
 
sielewi nchi hii kama Nyerere aliondoka na uongozi...kuna laana nchi hii somewhere. Mungu utusaidie!
 
Ndugu Arfat,

Katika sakata hili endapo mtu utajali kujiuliza swali la kwamba 'Jeuri hii ya Diwani Fisadi Zaida kudiriki kwenda kuchukua tenda mahala ili arudi kufyeka misitu ya Same kinyume na sheria kapata wapi?' basi moja kwa moja utjikuta ukilazimika pia kutaka kujua wafadhili wake wa karibu na wle wa mbali kidogo katika sakata zima.

Naamini sana tu kwamba hivyo ndivyo huyu mleta habari livyojikuta akielekeza mikono huko unakotafuta na wewe kukingia kifua kiaina hapa jukwaani.


Hii issue ilivyotoka kwenye wizi wa nyara hadi kuingizwa Ridhiwani imenitoa jasho. Mtoa taarifa kuna wakati unaweza kuinyima taarifa credibility bila sababu yeyote mi sioni jinsi ulivyomwingiza huyo kijana na kifalme katika hilo sakata kama ni sahihi kama ni kweli ni tukio la ukweli.

Labda kama ni kweli wana uhusiano basi hiyo ilipaswa kuwa habari nyingine kabisa inayojitegemea kwa ushahidi wake. Maana unaweza kutumia ushahidi wa kukamatwa kwa Diwani kwa wizi wa nyara za Umma kuwa ushahidi wa Ridhiwani kuwa na uhusianao na huyo mtuhumiwa kitu ambacho hakitoshelezi kuwa ushahidi unajitegemea.
 
Kama kazi wanazofanya viongozi wa viti maalum nchini ndio kama hivi anavyofanya huyu Zaina mchuuza magogo

na yule mwenzake Chatanda na vurugu za kule Arusha basi walipakodi hatuhitaji huu mzigo tena bora kiondolewe kabisa kwenye katiba.

Mkuu unaishi kwa Gude kweli
 
Kiongozi wa ngazi ya udiwani anapochukua panga na kuanza kufyeka misitu ya asili na kusababisha kuenea kwa jangwa kama ambavyo tunavyojua kule Same hali halisi ilivyo, je ni nani atakayeweza kuwazui wananchi wa kawaida anaowaongoza wasifnye mara kumi ya madhara kama hayo yanayoripotiwa hivi sasa??????????
 
Kama CCM chenyewe kimetumia wingi wao bungeni vibaya kushinda hoja ya msingi ya CHADEMA kule kuondolewa marupurupu kwa wabunge, je kuna hatari gani mbunge wa CHADEMA kujiamulia kupokea posho hizo akazipelekee walazwahoi ukilinganisha na Diwani Zaina kuingia katika misitu yetu ya asili na kutafuna dhuluma hizo mwenyewe tu???????????????
 
Back
Top Bottom