Huyu Nanyaro ni mnafiki,tena wa wazi hasa kwa sababu zifuatazo:-
1.Maelezo yake yamekuwa na utata na hasa kuelekea kupima upepo humu ndani,alishiriki kwenye kikao na akiwa mjumbe na anatambua muafaka ulifikiwa.Iwapo hakuafiki mbona hatukusikia sauti yake kama kweli yeye ni Mwanademokrasia.Iweje leo ndio ajitokeze na kudai hakubaliani na muafaka huu.HUU NI UNAFIKI TENA WA KICHAWI,kuna aina ya typing error sio hii ya kukosea neno zima tena na maana yake.
2.Hakutueleza wazi,kama alikuwa mwakilishi wa muafaka je baada ya kuona mambo hayaendi alijitoa?au anataka kutuaminisha kuwa kura zilizoharibika moja ni yake.Kama alifikia hatua ya kupigia kura kitu asichokiamini alitarajia nini?Hapa tukisema matokea ya kura yanajustify kuwa demokrasia ilichukua mkondo wake kwa maana ya wengi wape ni makosa?
3.Madiwani wanafiki wa muundo wake hawapaswi kuvumiliwa hata kidogo.Ni muhimu ukasimamia katika msimamo wako na kuamini ulichokitenda hata kama utatishwa vipi.Iwapo maamuzi ya chama yatapitishwa nashauri wewe uwe wa kwanza kufukuzwa kwa maana ya Usaliti wako na huu upotoshaji.Pia ukiwa muongo siku zote,jitahidi kutosahau unayoongopa sasa comment yako ya pili inaonyesha jinsi ulivyosahau udanganyifu wa kwanza kwamba muafaka ulifikiwa eti unatetea kuwa it was a ''typing error''.Tafadhari Nanyaro usituuzi na wala sisi sio kwamba hatukuenda shule ama hatujui kuchambua na kutafakari mambo.Ebu tueleze ukweli badala ya kutulaghai.