Diwani mstaafu CCM ajiua kwa risasi

Diwani mstaafu CCM ajiua kwa risasi

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
886
Reaction score
206
Diwani huyo mstaafu na kada maarufu mjenga chama wilayani muheza amejipiga risasi alfajiri ya leo;mpaka sasa uchunguzi unaendelea wa kubaini nini kimemsibu hadi kuamua kujipiga risasi mwenyewe;jina lake ni ndugu mkufya

=====================================
Habari Zaidi
=====================================

BY STEVE WILLIAM
9th June 2014

Constatine-Massawe-June9-2014.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe

Kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Ally Mkufya (60), anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi shingoni.

Mkufya ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo, alijipiga risasi jana alfajiri akiwa chumba alichokuwa akiishi kwenye baa yake ya Tete Pub Extra ambayo pia ina sehemu ya nyumba ya kulala wageni, iliyopo pembeni ya barabara ya kwenda Tanga mjini.

Kigogo huyo wa CCM ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki baa kadhaa, anadaiwa kukatisha maisha yake kwa kujipiga risasi shingoni wakati huo akiwa amejifungia chumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe, akizungumzia kifo hicho alisema uchunguzi unafanyika ili kujua chanzo cha kujiua kwa kujipiga risasi ingawa baadhi ya watu wanasema kifo hicho kimetokana na sababu za kifamilia zilizomfanya ahame nyumbani kwake na kuishi baa kwa muda mrefu.

Viongozi wa chama wilayani humo akiwamo Mwenyekiti Peter Jambele, Katibu Mwenezi , Makame Seif na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Muheza, Josephin Mbezi, walielezea kusikitishwa na kifo hicho walichosema ni kibaya.

Awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mlinzi wa baa hiyo, Idd Abdallah, alisema alipoingia kazini juzi jioni hakukutana na mwajiri wake licha ya kwamba alikuwa na kawaida ya kukaa nje hadi usiku baa inapofungwa.

Alieleza kuwa aliingiwa na hofu na kuwauliza wahudumu, lakini alijibiwa kuwa bosi wao amejipumzisha chumbani kwake kwa kuwa anajisikia homa na kwamba hali iliendelea hivyo hadi muda wa kufunga baa ulipofika na wahudumu kuondoka.

Mlinzi huyo alisema kuwa ilipofika asubuhi wahudumu walifungua baa na kufanya usafi, lakini cha kushangaza Mkufya alikuwa hajaamka jambo ambalo halikuwa kawaida yake kulala hadi wakati huo.

Hofu hiyo iliwafanya kugonga mlango, lakini haukufunguliwa hivyo kulazimika kuwapigia simu ndugu zake ili waje kwenye baa hiyo.

Abdallah alisema walipofika chumbani kwake walivunja mlango na kumkuta amekufa kwa kupigwa risasi shingoni na bunduki aina ya Short ikiwa pembeni yake huku damu zikiwa zimetapakaa chumba kizima.

Alisema walipiga simu polisi na askari walifika kuuchukua mwili wa marehemu hadi hospitali Teule wilayani Muheza ambako umehifadhiwa.

KAULI YA MKEWE

NIPASHE ilifika nyumbani kwa marehemu jana na kumkuta mkewe, Anna Mkufya, akiwa katika majonzi makubwa. Hata hivyo, hakuwa tayari kuzungumza lolote juu ya tukio hilo.

Marehemu ameacha watoto watano na anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Semgao wilayani Muheza.

SOURCE: NIPASHE

Vipi au na yeye picha zake za unyama unyamani zishaanza kutembea whatssap nini akidhaambika??!! Anyway,r.I.p gamba mstaafu!!
 
Laana ya ufisadi inawatafuna c.c.m,wamekula ruzuku za chama na mwisho wa siku madeni yamewazidi.
Dah! Basi r.i.p msalimie korimba mwambie ukweli uliomnyamazisha ndio unaotokea sasa,kwani kinana ameanzisha chama kipya ndani ya c.c.m.
Mafisadi oyeee?
 
Diwani huyo mstaafu na kada maarufu mjenga chama wilayani muheza amejipiga risasi alfajiri ya leo;mpaka sasa uchunguzi unaendelea wa kubaini nini kimemsibu hadi kuamua kujipiga risasi mwenyewe;jina lake ni ndugu mkufya

Huyu mzee ni jirani yetu,sababu ya kujiua ni kwamba aliitelekeza familia akahamia kwa mchepuko kwa kipindi kirefu,sasa watoto wake waishio dar wakamchukua mama yao na kumtafutia biashara,mzee aliporudi nyumbani akakuta mkewe amehamia dar nyumba ipo tupu,alipopiama afya akajikuta ameathirika akaamua kujimaliza maana hakyona sababu ya kuishi,hapo ndo umuhimu wa kubaki njia kuu unapoonekana
 
Poleni familia ya diwani
Magamba yashamzulumu maana kwa kuzulimiana ndio wenyewe
 
kwa lugha zenu hizi za kigaidi bora angekufa mbowe au slaa

siku ya kufa kamanda mbowe hadi masojaz tuta peperusha bendera nusu mlingoti.
Maana ni mkombozi wa kweli asiyejivunia utajiri wake bali anautumia kwa maslahi ya umma.
 
Damu za wanyonge zimeanza kuwatafuna wanajiua.rip intarahamwe nenda kwa shetani na Mungu asikupokee.
 
Huyu mzee ni jirani yetu,sababu ya kujiua ni kwamba aliitelekeza familia akahamia kwa mchepuko kwa kipindi kirefu,sasa watoto wake waishio dar wakamchukua mama yao na kumtafutia biashara,mzee aliporudi nyumbani akakuta mkewe amehamia dar nyumba ipo tupu,alipopiama afya akajikuta ameathirika akaamua kujimaliza maana hakyona sababu ya kuishi,hapo ndo umuhimu wa kubaki njia kuu unapoonekana

Kweli miCCM inalaana huku KAPUYA anaambukiza vibinti na upande mwingine mibaba inaambukizwa na vibinti kwa hiyo NGOMA DROO
 
Lazima kuna kitu kimemtatiza. mpaka akachukua maamuzi mazito kama hayo!
Labda aliona sura yake ataiweka wapi Tanzania hii!

RIP
 
kabisa mkuu,majengo near shule ya msingi

Nilikuwepo Muheza miaka 6 ilopita nakumbuka huyu mzee alikuwa ni mmiliki wa bar moja kubwa hapo Muheza na ndiyo sehemu ambayo mm naikumbuka vizuri maana baada ya kazi mda mwingi tuliutumia kukaa pale kwenye bar yake na Rafiki yetu Rama Mzungu, R.I.P Mzee Mkufya
 
Huyu mzee ni jirani yetu,sababu ya kujiua ni kwamba aliitelekeza familia akahamia kwa mchepuko kwa kipindi kirefu,sasa watoto wake waishio dar wakamchukua mama yao na kumtafutia biashara,mzee aliporudi nyumbani akakuta mkewe amehamia dar nyumba ipo tupu,alipopiama afya akajikuta ameathirika akaamua kujimaliza maana hakyona sababu ya kuishi,hapo ndo umuhimu wa kubaki njia kuu unapoonekana

Kwa hiyo alijiua baada ya kuona hawezi kumuambikiza mkewe?Au aliamua kujiua sababu alijikuta amekosa mahali pakulelewa akishaanza kuwa hoi?
 
Back
Top Bottom