kwa kifupi sana diwan hana kazi kwa
" kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo ktk eneo la kata ya kyela mjini,
kunapelekea halmashauri ya kyela ikome kuwa na mamlaka ya moja kwa moja kupitia kwa diwan wa kata hiyo"
imesema sehemu ya barua hiyo
imeendelea kueleza kua
<kutokana na kufutika kwa kata vijiji navyo vimefutika na wenyeviti wake pia wamefutika na diwani wa kata husika pia naye amefutika (amekoma kuwa diwani) Hio ndio tafsiri ya sahihi ya sheria>
hiyo ni sehemu tu ya barua hiyo kinachonitatiza ni namna ilivyosisitiza kua ndio tafsiri sahihi ya sheria naomba nielimishwe zaidi ktk hatua zilizostahili na mifano halisi ya sehemu zingine au ndo ule usemi wa
ukimwaga mboga sisi tutamwaga ugali?
Wakuu,
Mbona sijalisikia hili? Wacha nifuatilie nione kuna nini. Yaani Kyela kuwa mji mdogo ina maana hakutakuwa na diwani wa kata ya Kyela?
Mheshimiwa Mahenge hawaelewani kabisa na Mwakyembe. Mwenyekiti wa Halmashauri ni mtu wa mbunge.
Muhimu hapa kabla ya kulaumu ni kuangalia sheria inasemaje. Vinginevyo hawa watu wanataka kuleta matatizo.
Huyo Mwenyekiti wa halmashauri mwenyewe hata udiwani hana nafasi ya kurudi tena.
Hii Kyela yetu wanaiyumbisha sana.
Sasa mnataka kuniambia Mwakyembe ndo kaunda Halmashauri ya Mji mdogo au? siyo TAMISEMI. Kama ni kweli kata yenu imekuwa Mji mdogo hilo ni swala la kufurahia, sasa mnalita vita kwa kulinda kibarua cha diwani wenu! yaani mnataka wananchi wakose heshma yao ya kuwa mji mdogo na kupata Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na wakuu wa idara na watalaam wengine kwasababu ya huyo diwani? kweli nyie mmechoka, au mnaelimu gani wakuu?
....... Kinachoongelewa hapa ni je sheria inafuatwa au inapindishwa kwa ajili ya vita vya kisiasa?
Hivi kweli ni utawala bora kumwandikia barua kama hiyo diwani na kusambaza sehemu zote bila hata kuongea na yeye kwanza? Huu ni uongozi wa aina gani? Hata kama sheria itasema hivyo, ilitakiwa wamwite Mahenge kwanza na ikiwezekana hata kumuaga.
Wasomi wa sheria wanaiharibu Kyela.
.Technically inapindishwa mbaya na ni siasa duni zisizo na fikra kamili. hapo ni kufirisika kifikra 100%
Na kama ni siasa hajui ni siasi fitna na sio siasa uchumi na maendeleo,
Utawalaaaaaaa!!!!!! utawala gani kuhalibu maendeleo ya kata ndio utawala uende ivyo what's wrong with we black africans??? jamani hatumwogopi MUNGU????? au Hamjui kuna KUZALIWA NA KUFA KESHO au wadhani ukifa utaenda na huo utajiri sijui siasa zako kwa MUNGU??????
me nadhani ukiwa ktk siasa na uongozi ukapata ni kuhudumia jamii, fanikisha maendeleo, jenga heshima na mengineyo ya msingi ndio ingawa twajuwa wewe ni binadamu kuna kuteleza ila isiwe makusudi sasa
Kesho kimeitishwa kikao cha kamati ya maadili ya halmashauri na wamempa Mwenyekiti mpaka kesho awe amemwaomba msamaha mheshimiwa Mahenge, vinginevyo yeye ndiye atasimamishwa wakisubiri kikao cha madiwani.
Hizi siasa za fitna za Afrika ndio zinatumaliza na tutaendelea kuwa maskini. Kibaya zaidi zinafanywa na wasomi ambao ndio walitakiwa wawe nuru ya mambo mapya ya maana.
aanayetakiwa kuandika barua hiyo ni mkurugenzi iweje mwenyekiti wa halmashauri kujipa madaraka ya kuandika barua hiyo.kwa sababu hiyo ndio shaka ya kuhusika kwa Dr mwekyembe kunakuja kwani mahenge ni hasimu wa DR na mwenyekiti wa halmashauri ni mfuasi wa DR.Sasa mnataka kuniambia Mwakyembe ndo kaunda Halmashauri ya Mji mdogo au? siyo TAMISEMI. Kama ni kweli kata yenu imekuwa Mji mdogo hilo ni swala la kufurahia, sasa mnalita vita kwa kulinda kibarua cha diwani wenu! yaani mnataka wananchi wakose heshma yao ya kuwa mji mdogo na kupata Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na wakuu wa idara na watalaam wengine kwasababu ya huyo diwani? kweli nyie mmechoka, au mnaelimu gani wakuu?
Hizi siasa za visasi Kyela ni balaa tupu. Nimefuatilia na kuongea na wahusika. Kilichotokea mbunge alikua hapa wiki jana na akamshauri huyo mtu wake kwamba aandike barua ya kumfuta Mahenge udiwani wa kata ya Kyela mjini kwasababu sasa Kyela imekuwa mji mdogo.
Mwenyekiti na yeye bila kuangalia sheria inasemaje na bila kushauriana na madiwani wenzake, akaandika hiyo barua.
Mheshimiwa Mahenge ni mfuasi namba moja wa Mwakalinga na pia anakumbukwa kwa juhudi kubwa alizofanya kusimamia ujenzi wa shule za sekondari Kyela. Yeye kwa madiwani ndiye ana uwezo mkubwa, hivyo anafanya mambo mengi kwa kujitolea. Kwa wanaoijua Kyela, yeye ni mmiliki wa guest houses mbalimbali hapa mjini.
Madiwani wanakusanya signatures ili zifike theluthi mbili na wanataka kuyitisha kikao cha madiwani na kumfukuza kazi huyo Mwenyekiti. Mpaka leo madiwani 11 kati ya 21 wameweka sahihi zao na wanasema kesho namba itatimia.
Katika madiwani 21, mbunge anaungwa mkono na madiwani kama watano tu akiwemo huyo diwani Kisugujila pamoja na mama watatu wa kuteuliwa na diwani mwingine wa kuchaguliwa.
Halmashauri ya CCM wilaya pia inaandaa kikao kushughulikia mzozo huu.
Mimi sijui sheria na tunawaomba wenye kujua sheria za miji midogo mutuelemishe. Ila nimeambiwa mji mdogo kama Tunduma una diwani wake na pia kuna mifano ya miji mingine na kwamba sheria waliyotumia kuandika hiyo barua haina maana hiyo.
Tutawahabarisha zaidi vita hii itafika wapi. Ila nina uhakika uamuzi huu una uhusiano na uchaguzi wa mwakani na mpambano kati ya Mwakalinga na Mwakyembe.
Watu hawataki majimbo yao yaguswe.
Mheshimiwa mahenge ndiye aliongoza juhudi za Kyela kuwa mji mdogo. Kinachoongelewa hapa ni je sheria inafuatwa au inapindishwa kwa ajili ya vita vya kisiasa?
Hivi kweli ni utawala bora kumwandikia barua kama hiyo diwani na kusambaza sehemu zote bila hata kuongea na yeye kwanza? Huu ni uongozi wa aina gani? Hata kama sheria itasema hivyo, ilitakiwa wamwite Mahenge kwanza na ikiwezekana hata kumuaga.
Wasomi wa sheria wanaiharibu Kyela.
Mheshimiwa mahenge ndiye aliongoza juhudi za Kyela kuwa mji mdogo. Kinachoongelewa hapa ni je sheria inafuatwa au inapindishwa kwa ajili ya vita vya kisiasa?
Hivi kweli ni utawala bora kumwandikia barua kama hiyo diwani na kusambaza sehemu zote bila hata kuongea na yeye kwanza? Huu ni uongozi wa aina gani? Hata kama sheria itasema hivyo, ilitakiwa wamwite Mahenge kwanza na ikiwezekana hata kumuaga.
Wasomi wa sheria wanaiharibu Kyela.
Kilitime,
Hapa vurugu tupu na wacha tuone mwisho wake utakuwaje.
Sikuandika jana kwasababu hata mimi yamenikuta, nimechongewa kwenye uongozi wa wilaya kwamba namwandika vibaya mbunge JF.
Eti mbunge amepewa IP ya computer ninayotumia na uongozi wa JF. Hiyo ni JF where we dare to speak openly!
Wote tunaotumia hiyo kompyuta ya kazini tuliwekwa kitimoto ila hawana ushahidi ni nani. Nitawajulisheni zaidi baadaye. Watu wanashindwa kufuatilia maendeleo, kazi ni kufuatilia wale ambao wanapingana nao kimawazo. Engineer hayumbishwi na mtu yeyote.
Kuna vikao vingi bado vinaendelea. Mwenyekiti amekataa kuomba msamaha ingawaje sasa ni kama anakubali tafsiri yake ya hiyo sheria ilikuwa na makosa.
Leo siku ya tatu watu hawafanyi kazi na wanaongelea mgogoro huo tu.
Nikipata maelezo zaidi nitawajulisheni. Wacha nilinde kibarua changu kwanza.