PreGE2025 Diwani kata ya Chanika atoa milioni 40 ikiwa ahadi yake kwa wakazi wa eneo hilo kwa ushindi wa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa

PreGE2025 Diwani kata ya Chanika atoa milioni 40 ikiwa ahadi yake kwa wakazi wa eneo hilo kwa ushindi wa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Diwani wa Kata ya Chanika na Naibu Meya wa Ilala Masaburi Deoglas Masaburi, amesema kutokana na kufanya vizuri kwenye Uandikishaji wa Daftari la Kudumu lililopita na kupelekea Ushindi wa kishindo wa Serikali za Mitaa, ambapo aliahidi kutoa Sh. Milioni 10 kwa Kata yake na leo ametimiza ahadi hiyo na nyongeza ya Sh. Milioni 20 ili kwenda kuongeza bidii kwenye zoezi kama hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu.
1742214358374.png

Naibu Meya Massaburi pia ameanza kwa kutoa Sh. Milioni 10 kwenye Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kata ya Chanika Kwani Ukumbi Uliopo umekuwa ukiwanyima wana CCM faragha na hivyo kwenda kukodi Ukumbi kwa ajili ya Mikutano.

Fedha hizo Jumla Sh. Milioni 30 alikabidhi mbele ya Katibu wa CCM Wilaya na Wajumbe wote 1,000 wa Mkutano Mkuu wa Kata hiyo.

Aidha amesema ni Mkakati wa Chanika kuandikisha watu wengi zaidi ili Uchaguzi Mkuu CCM ipate Kura nyingi zaidi Kwa Dkt. Samia na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi ambapo ametoa wito kwa Viongozi wote hasa Madiwani kuwa na mkakati kwenye kipindi hiki ili kumpa zawadi ya ushindi wa kishindo Rais Dkt. Samia.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
 
hapo kashapiga million 800+ karibia bilion halafu anatoa million 40
 
Back
Top Bottom