kibananhukhu
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 366
- 166
Ni kweli jana jioni, tumeondokewa na diwani wetu Rudolf Chaula, ambaye amepoteza uhai wake kwa kujinyonga na kamba nyumbani kwake. Polisi toka Ludewa wameenda, Mlangali asubuhi hii ili kubaini tatizo hasa ni kitu gani. Hata hivyo, marehemu ameacha ujumbe kwamba ameamua kujinyonga, kwa kuwa kuna mtu alikuwa anamdai tshs. milioni 81, mali ya saccos ya mlangali, naye alikuwa hataki kumlipa. Ni nani aliyemkopsha hizo pesa, basi wenye taarifa zaidi, wanaweza kutusaidia. Tumwombee marehemu, na pole nyingi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki
Alikopesha watu Binafsi hela ili wasaidie Mtu kupata ubunge, Ni hela za Saccos ya walalahoi, walishindwa vibaya na deo yule Wa Filikunjomb, hawajafanikiwa kuipa. Damu ya marehemu hakika I mabegani mwao na vizazi vyao vyote
ivi iringa ni afghan eee,
Kauli yako haijakaa wazi, jaribu kuifafanua ili ueleweke, na kama tukitaka kuchangia maoni ni vema ueleweke vizuri kwanza.
Diwani na deli la Mil 81 nawezekana ee..kwenye maeneo kama hayo...? nadhani ilikuwa na % yake then ikala kwake..Kudadak unadai unajiua..ungedaiwa ungeua??
mtu aliyejinyonga ana R I P?
tusijepoteza muda kumwombea mtu aliyependa mwenyewe kifo.
[h=6]
[/h][h=6]''Ni kweli jana jioni, tumeondokewa na
diwani wetu Rudolf Chaula (CCM), ambaye amepoteza uhai wake kwa
kujinyonga na kamba nyumbani kwake. Polisi toka Ludewa wameenda,
Mlangali asubuhi hii ili kubaini tatizo hasa ni kitu gani. Hata hivyo,
marehemu ameacha ujumbe kwamba ameamua kujinyonga, kwa kuwa kuna mtu
alikuwa anamdai tshs. milioni 81, mali ya saccos ya mlangali, naye
alikuwa hataki kumlipa. Ni nani aliyemkopsha hizo pesa, basi wenye
taarifa zaidi, wanaweza kutusaidia. Tumwombee marehemu, na pole nyingi
kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.''[/h]Hayo ni
maneno ya Deogratias Haule
Filikunjombe mbunge wa Ludewa mkoani Njombe akielezea kifo cha
diwani huyo wa CCM.
source; Deogratias
Haule Filikunjombe mbunge wa LUEWA.