Diwani Arusha (CHADEMA), azuia wafanyabiashara kulipa ushuru

Diwani Arusha (CHADEMA), azuia wafanyabiashara kulipa ushuru

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2008
Posts
482
Reaction score
131
Wadau,nipo hapa soko la Jumla la Kilombero,diwani wa kata ya Levolosi CHADEMA,Ephata Nanyaro amefika hapa na kuwatangazia wafanyabiashara wote kuwa wasilipe ushuru wowote wa soko,kwa madai kuwa,

1.Dc ameingilia shughuli za halmashauri kwa kuleta vijana wa CCM kukusanya ushuru sokoni,kinyume cha sheria,amedai kuwa DC hana mamlaka ya kuleta watu wake ndani ya soko,hivyo amewataka wafanyabiashara kutolipa hadi muafaka upatikane.

Baada ya tamko ilo wafanyabiashara wamelipuka kwa furaha na kumbeba diwani wao juu juu.

Je kisheria huyu diwani yupo sahihj?
 
Kwani wanaotakiwa kukusanya ushuru ni akina nani? Kama wanaokusanya siyo wanaotakiwa kukusanya kisheria basi diwani yuko sawa, taratibu lazima zifuatwe.
 
Kwa kuangalia sehemu mbalimbali za maeneo yanayotolewa huduma za ukusanyaji wa kodi kama sokoni huwa inatolewa zabuni na mwombaji akishinda anapatiwa kibali cha kufanya hiyo kazi,zaidi ya hapo mpaka itolewe taarifa mbadala na ninadhani madiwani huwa wanafahamishwa,hebu aliye karibu na sakata atujuze zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wadau,nipo hapa soko la Jumla la Kilombero,diwani wa kata ya Levolosi CHADEMA,Ephata Nanyaro amefika hapa na kuwatangazia wafanyabiashara wote kuwa wasilipe ushuru wowote wa soko,kwa madai kuwa,

1.Dc ameingilia shughuli za halmashauri kwa kuleta vijana wa CCM kukusanya ushuru sokoni,kinyume cha sheria,amedai kuwa DC hana mamlaka ya kuleta watu wake ndani ya soko,hivyo amewataka wafanyabiashara kutolipa hadi muafaka upatikane.

Baada ya tamko ilo wafanyabiashara wamelipuka kwa furaha na kumbeba diwani wao juu juu.

Je kisheria huyu diwani yupo sahihj?
kama taarifa yako ni sawasawa kama ulivyotueleza,Diwani yuko sahihi 100% wasilipe mpaka muafaka hupatikane
 
Mwana Mpambanaji...... Diwani yupo sahihi pale taratibu zinaopokiukwa wakati taratibu zikifanyika ni vyema hilo zoezi likasima.kwa ulewa wangu.
Nikupe Homework jaribu kufuatilia pia kama yule Diwani wa Kinondoni ambaye amehusika kwenye lile sakata la Jengo kuanguka kama taratibu zilifuatwa yeye kufanya alichokifanya.
 
Back
Top Bottom