Diva: Nyimbo zangu zinabaniwa sana kupigwa Redioni

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
13092350_1017963818284902_1208324435_n.jpg


Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema nyimbo zake pamoja na za mtangazaji mwenzake, Adam Mchomvu zinabaniwa na redio zingine, kitu ambacho anaona si sawa.

Anasema redio za mikoani ndizo zimekuwa zikiwapa support bila kujali kuwa wanatoka Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania nyimbo zao.

Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.

“Mimi naona wako so unprofessional, mbona sisi Clouds FM watu wazuri, mimi Sam Misago kaja, katoa wimbo ataitwa kwenye XXL nyimbo yake itachezwa, sisi mbona nyimbo zetu hamchezi?” amehoji Diva.

“Nilipeleka nyimbo East Africa Radio na ina haki zote za kuchezwa na haikuchezwa kwasababu natoka Clouds Media, kwanini wanatufanyia hivi? Hii ni biashara, wao wafanye kazi zao, na sisi tufanye kazi zetu lakini when it comes to music, sisi tunafanya serious kabisa,” amesisitiza.

Chanzo: Bongo 5
 
wenyewe clouds mbona wanabania nyimbo za wasanii wengine? ndo wakome kwa nyimbo gan haswa kali ad ipigwe yy na adam wabak kuwa watangazaji tu hawajui kuimba
 
Teh Teh inachekesha sana ..wote Diva ,Sam na Adam hawana viwango vya kustahili kuchezewa nyimbo zao kwanza hawajui kuimba!

Si huwa wanasema wimbo ukipigwa radio yao basi umekuwa hit song? Sasa ana walalamikia nini East Africa radio?

Mimi huwa nasikiliza Clouds lakini sijawai kusikia wimbo wa Diva! Kuna watu wana mdanganya kumwambia anajua kuimba ....!
 
Maajabu hayatoisha daima, hivi muziki ni rahisi hiviii !!!!!!....... Huyu attention seeker inabidi apuuzwe ...

Muziki ni zaidi ya kufungwa hogo la pua baada ya kutoka kwenye ala za roho..
 
Hivi kuna mtu amewahi kuusikia wimbo wa diva? Na kwakweli nyimbo za Adam nimesikia moja lakini sidhani kama ni heat
 
Back
Top Bottom