Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,198
Salaam Wakuu.
Bila kububuja maneno,kichwa cha Uzi chajieleza. Nimekuwa mtumiaji wa Instagram kwa muda tu na huwa naitumia Kama mitandao mingine.
Kumekuwepo na tabia zisizopendeza ya presenters wa Clouds FM haswa Diva wa "Ala za roho" pamoja na Soudy Brown katika kipengele cha "U heard" wakati wa XXL.
Watangazaji hawa pamoja na kujua kwamba wao ni sehemu muhimu ya jamii,wamekuwa wakipost picha zisizo na maadili katika kurasa zao za Instagram. Sijajua kama Ofisi yao haina mamlaka ya kuwafatilia nje ya kazi lakini post zao hazipendezi kabisa.
Kwa mfano, Diva leo kaumia (anavyodai) na kupata mchubuko kidogo nyuma ya goti, kapiga picha kanyanyua mguu juu na kuonyesha mahali hapo huku moja kwa moja sehemu kubwa ya paja lake likiwa wazi.
Hii si Mara ya kwanza,amekuwa akipiga picha nyingi tu zisizopendeza na kuzitupia Instagram zingine zikiacha makalio yake wazi kabisa.
Soudy Brown naye kazidi, pamoja na ukweli kwamba habari zake ni za kimbea lakini mitandao Ina exposure kubwa Sana katika kazi.
Majuzi alitupia picha ya Giggy Money huku sehemu kubwa ya binti huyo ikiwa wazi. Amekuwa akitupia picha nyingi tu za aina hiyo.
Ni kweli account ni zao binafsi lakini haipaswi kutupia picha zisizo na maadili katika jamii yetu. Wale ni watangazaji na wanafatiliwa na sehemu kubwa ya wananchi. Najaribu kujiuliza je,Kama ndo akili zao zinavyowatuma,huko kazini wanafanya vema?
Je, Clouds Media haioni haja ya kuwahimiza kufanya mambo yapendezayo kwa jamii? Kama hawawezi kuwaingilia katika maisha yao binafsi,Clouds Media haioni kwamba watangazaji wake wanaichafua? Basi,kama ni hivyo wasitoe post zinahusiana na Clouds kwenye mitandao wanayopost ufuska wao.
Naomba taarifa na ziwafikie wote wanaopost picha zisizopendeza. Pia Clouds Media wawaeleze kwamba, tabia irekebishwe.
Nawasilisha..