leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,583
- 3,181
Katika kipindi cha mkasi kilichoruka jana 21/12/2015 usiku Nilipigwa na mshangao wa kufa mtu pale muongoza kipindi Salama alipomuuliza Diva kama anaufahamu wimbo wa taifa akajibu kwa kifupi "siujui". Salama hakuamini jibu hilo akamuanzishia wimbo huo ili kumsaidia hata kama alikuwa ameusahau akasema kwa msisitizo "kwanza huwa siupendi kabisa wimbo huo". Kwanza nilijisikia ovyo na kuhisi kumchukia ghafla mtangazaji huyo wa Clouds Fm.
Naamini kuwa Diva ni mwandishi wa habari haijaLishi habari za aina gani kwa hiyo naamini anajua maadili yanayohusu taaluma hiyo ya habari kwa nini aliruhusu kitu cha namna hiyo (maneno yake ya chuki dhidi ya wimbo wa taifa) kitokee mbele ya watazamaji na kama kipindi hicho hakikuwa live kwa nini EATV hawakuhalili sehemu hiyo?