Jamani mm kila nikisoma conversation za maswala ya vyuo nakuta majigambo, kejeli, matusi na kebehi za wana-udsm wakikashifu vyuo vingine,
Sometimes najiuliza: hivi mtu unaweza kuonekana bora kwasababu umeweza kuonesha udhaifu wa mtu mwingine?
Kila nikisoma hoja za wana-udsm naona wanaeleza historia tu na sio current logic,
Utaskia:
- udsm chuo kikongwe ( hii hatukatai na kimetoa mchango mkubwa sana kwa taifa, but twambie; currently kuna nn?)
- walimu wa vyuo vingi nchini wametoka udsm (hapa utakumbuka kauli ya mwana falsafa; John Dewey aluyesema "the quality of education shall never be raised above the quality of teachers" kama walimu wa vyuo hivi wametoka udsm then vyuo hivi viwe poor,
Unadhani huo u-poor umeanzia wapi?)
-udsm ina-rank the first kitaifa: (hapa tunapaswa tuelewe vigezo vinavyotumika ku-rank vyuo.
Kwa kifupi wanaangalia popularity, number of search engines, number professors n.k.
Academic ina less than 10% ktk ku-rank vyuo kwasababu kila chuo kina mtaala wake.
Kwakuangalia vigezo hivyo,
Udsm ina-rank the first kwasababu imeanzishwa zamani hivyo ime-gain popularity, ina product nyingi n.k.
BUT ukisoma ranking ya vyuo, mwishoni hua wanaeleza kua rank hiyo isitumike ku-jaji academic excellence ya vyuo kwasababu sio academic based ranking.
Kwa ufupi tu udsm mnapaswa kubadilika,
Vyuo vingi kwasasa viko vizuri sana,
Hata hapa nikipitia majadiliano yenu,
Naona DIT wakitoa evidence hadi video za mambo wanayoyafanya lkn UDSM wana historia, matusi, kejeli na vijembe.
Hii ni aibu kubwa sana,
Nime-experience uwezo wa vijana wanaosoma education UDSM na UDOM, nnachoweza kusema ni kua mwanafunzi wa education UDOM anauwezo Mara tatu zaidi ya wa UDSM kuanzia discipline, content (ACK & PCK).
Ningeshauri UDSM mjifunze busara kutoka UDOM, SAUT, SUA na vyuo vingine ambao kwao wakiona mtu anakosea au ana udhaifu wanamrekebisha na kushirikiana nae na sio kumkebehi na kumuona hafai,
Mm ningeomba tu vijana mchape kazi muache majigambo yasiyo na tija,
Ktk ranking ya vyuo,
Undergraduate una mchango wa approximately 0.001%
Ikumbukwe, TCU walifanya uhakiki wa vyuo na wakavifungia vyuo vilivyokosa ubora au program zilizokua na mapungufu ktk vyuo husika,
Kwa maana hiyo vyuo vilivyobaki vyote ni bora.
Kilichobaki ni jitihada za mtu binafsi.
Ikumbukwe pia wanafunzi walio ktk vyuo vikuu wote walikubaliwa na NECTA, wengine na NACTE na sasa approved by TCU kua wasake degree; jitihada hizi si za kubezwa Hata kidogo na hakuna kilaza atakayepitishwa organizations zote hizo.
Wakati huo pia tukumbuke kuna vijana wamesoma shule za kata lkn saiv ni international figures na kuna wengine wamesoma international schools then saivi ni ma-admin wa magroup ya WhatsApp na waanzisha uzi maarufu jf.
Mwanachuo utaonekana bora ikiwa una mchango thabiti kwa familia yako na jamii yako na si vinginevyo.
NAWAPENDENI WANACHUO WOTE LAKINI NTAZIDI KUWAPENDA IKIWA MTAHESHIMIANA,
msomi mzuri hujiheshimu, huwaheshimu wenzake na jamii kwa ujumla