Nimeiskliza Ngoma ya Rapcha, actually ni nzuri kwa sababu rahisi lakini pia ina sound good, na hicho ndio watu hupenda, watu hawapendi vitu vinavyofikirisha Akili
Dogo ana machaguzi mazuri ya beat pamoja na rap style ila anakosa content tu, ndomana hapo juu jamaa kasema wengine wamesema amechana utoto utoto
Kwa Dizasta vina huko panakosekana Beat nzuri na rap style ila ndio kuna content, ukiskiliza "Best friend" utagundua kuwa haukuwa wimbo mahsusi kwa ajili ya Rapcha japokuwa aliguswa kidogo sana
Best friend ilikuwa inaongelea aina za marafiki na ndugu ambao tunaishi nao kila siku pamoja na kwamba wana tusnich ila tunaongea nao kama kawaida kitu ambacho kina ukweli kwa [emoji817]%
Aliongelea washkaji ambao hawapendi kuona unapiga hela, japokuwa mnashinda pamoja ila ikija mishe ya pesa wanakwepesha na hawataki kuona unapata
Anaongelea washkaji ambao wao ni uvivu tu na kupenda vya kitonga ila kazi hawataki, wao wanachojali ni kudhadharirisha wanawake utadhani wao hawatakuja kuwa na watoto wa kike
Anaongelea kuhusu yeye kuwa ni binadamu na kama ilivo kwa wanadamu wengine kuwa ni dhaifu kwahiyo ata yeye anakosea, ata yeye sio mkamilifu
Kama tujuavyo kuhusu tambo za hip hop, pia jamaa anamwambia Rapcha kwamba yeye sio level zake, hayupo katika ushindani wake,Dizasta vina huwenda wasanii ambao yeye anaona wanakaa chungu kimoja LABDA ni the likes of The incredible,Mbishi,Songa,Sterio,Young killer nk
Kiufupi jamaa ameandika Mambo mengi sana ambayo yanaongelea tabia za wanadamu tulivo akiwemo yeye mwenyewe na hakujikita katika kumchana Rapcha, Ukiskliza Best friend hutoishia kuburudika bali utajifunza kitu/vitu
kinachomponza Dizasta vina ni kutaka kupeleka ujumbe/mafundisho kwa Hadhira kwenye kila anachokiandika kwa sababu ni wazi jamaa anatumia Akili nyingi sana katika uandishi wake
Kwakuwa kwenye best friend alisema hii sio Diss bali ni Clarification na kama dogo ataamua kuchagua vita basi ndio itakuja diss, since Rapcha ameamua kuchagua vita basi Acha tusubiri Diss rasmi sasa
Hii imeturudisha nyuma kidogo wakati Motra kawachana KIKOSI KAZI, palichangamka sana maana alikuja Mexcana na balaa la Amkia wakubwa kama haitoshi akatoka na P mawenge na Future wife na akafunga biashara