Dish gani zuri na bora!

Madewa

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
467
Reaction score
192
Habari zenu wanaJf
Niko Arusha sasa hivi, nahitaji kununua dish la bei ya kawaida, lenye ubora na lenye vifurushi vya bei nafuu, vipi nawezapata wapi huduma hiyo hapa Arusha?

Vipi ubora wa haya azamtv, picha na sauti vipi kwa wanaoyatumia, hivi wanachanel ngapi za free baada ya kifurushi kuisha muda wake?

Natanguliza shukrani
 
pokea ushauri wangu nunua ZUKU ukiwa na 160000 unapata channel za kutosha na nzuri
 
Ndio kaka typing error ni elfu kumi na sita
 
Zuku inakuwaje monthly subscription?
 
unaacha kwenda azam unataka uende zuku angalia usije ukarudi tena hapa
 
vp zuku wako maeneo gani hapa arusha?
 
Azam tv ndio bora.Salio likikata unaendelea kupata channel za bure kibao za Kenya,Uganda na Bongo zinazopatikana kwenye Azam TV.
Customer care yao ni Supadupa pia.
 
Naomba unitajie channel za bongo zinazopatikana kwenye azamtv
Azam One, Azam two, sinema zetu, TBC1, Ch 10, Clouds, ZBC.

King'amuzi chao ni Tsh 137,000 na kifurushi kwa mwezi ni 12,500. Ufundi ni juu yao.

Ila kama ni mpenzi zaidi wa Channels za Bongo, nakushauri ununue Ting ya dish Channels zote za Bongo unapata. Usinunue ting ya antenna, itakutesa. Haipo stable kabisa
 
kuna channel inaonyesha UEFA champions league zuku?

usidanganyike zuku ovyo kabisa. Mimi nilinunua sasa najuta. Hakuna itv, star tv, wala mlimani tv. Local stations zilizopo Ni clouds tv, Chanel ten, tbccm, na eatv basi!
 
TEKSAT ni king'amuzi chenye vipindi vya burudani mbalimbali kutoka hapa nyumbani kama ITV, EATV, CAPITAL, START TV, TBC1, CHANNEL 10, CLOUDS, MLIMANI TV na nyingine nyingi za nje.

Kipo katika mfumo wa MPEG 4, yenye uwezo wa kuunganisha HDMI-high definition, USB itakayokuwezesha kuona picha za filamu AV,RF na Coaxial digital audio, pamoja na uwezo wa ku pause, record na kurewindi vipindi vilivyorekodiwa kwenye External HDD. Kinatumia aria ya kawaida.

Kinapatikana kwa bei ya shilingi 115,000/= tu na hakina malipo ya mwezi.

Piga simu:

0754 292929
0685 292929
0718 282853
0784 679922

Mawakala wanakaribishwa.
 

kinapatkana mikoa gani?
 
Azam Tv inaweza kamata huku Marasibora Rorya?
Kinapatikana wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…