Director Muhimbili, fanya haya ili kuboresha huduma ya afya

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
Pamoja majukumu mengi unayopambana nayo naomba nikushauri yafuatayo.

Angalia uwezekano wa kushirikisha sekta binafsi kuwekeza sehemu ya kupumzika kwa watu wanaokuja kuangalia wagonjwa wao. Kwa sasa hali si nzuri hata kidogo. Mmeajili walinzi kuhakikisha sehemu zilizotengwa maalumu kwa mapumziko hazitumiki. Nazungumzi ndani ya geti. Pale main gate ni kero mbaya kabisa.

Naomba mchukulie wingi watu wanaofika Muhimbili kwa sababu uoyote ile kama fursa kwa upande wenu kufanya uwekezaji wenye lengo la kuboresha huduma zenu, iwe kwa wagonjwa au wale wanaowahudumia wagonjwa.

Kuna panya ndiyo panya wa kutosha tu. Jaribuni kuwaondoa kwani wanahemea chakula cha wagonjwa labda hata kuhatarisha afya zao.

Mnapoishiwa mashuka muwe na njia mbadala sio kuwakatalia wagonjwa kukabiliana na changamoto mliosababisha wenyewe.

Muwafundishe walinzi kutoka hayo makampuni ya ulinzi namna ya kutoa huduma kwa wanaofika hapo hospitalini kwenu. Lugha iwe ya staha. Huwezi fukuza watu kama ndege.

Wakatabahu. Naomba niishie hapa. Shukrani sana.
 
Back
Top Bottom