Director DSTV; Compact, Compact + na Premier wote wapewe UCL

Director DSTV; Compact, Compact + na Premier wote wapewe UCL

Joined
Feb 27, 2016
Posts
109
Reaction score
138
Kwa wanabodi JF na Mkurugenzi Dstv;

Wapendwa kwa hali ya sasa hela ni ngumu sana matumizi yamekuwa juu kiwango kikubwa na hela haionekani. Tukiachana na malalamiko ya wapenzi wengi wa soka hapa nchini juu ya ughali wa malipo ya dstv package lakini victim wa soka bado wanajitahidi kulipa hivyo hivyo kwa kukusanya huku na kule na kupunguza huku na kule,kujinyima baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima mtu alipe dstv aangalie soka. Chaajabu ni hawa wenzetu wa dstv kukosa huruma.

Mfano:
Kuna shida gani mtu anayelipa shs elfu 69,000/= almost 70,000/= kuruhusiwa kuangalia mechi za uefa champions league? mechi zenyewe sio kilasiku ni jumanne na jumatano mara moja au mara mbili kwa mwezi, wakati mwingine ratiba inaonyesha kabisa mechi itaonyeshwa SS10, ama SS3,SS7 lakini dstv wanabadili ratiba na kuzihamisha SS6,SS5,SS2 ilimradi mtu wa compact asizione.

Kumbuka mngeweza kuwa na wateja wengi wa compact kwa hiyo elfu 70 wakalipa pesa nyingi japo mnaona ni kidogo lakini wakawa wengi sana kwakuwa wanauhakika na UCL na EPL kuliko mkangangania premier mpate hela nyingi kukawa na wateja kidogo, jaribuni huo ubunifu kwa miezi miwili muone mtakavyopata wateja .

Inasikitisha kwa usawa huu pesa ilivyongumu mtu anajibana ale maharage na matembele wiki tatu mfulizo alipe shs elfu sabini 70,000/=ama sitini na tisa 69,000/=DSTV na bado aache familia yake usiku aende bar au pub akalipe buku ama buku mbili kila mechi akaangalie PSG na Buyern.
Mechi zenyewe zinachezwa usiku mwingi kurudi nyumbani ni saa sita au saba, ugomvi na familia, kisa compact hawaonyeshi ucl,mtavunja ndoa za watu, jamani watanzania wengi wanapenda soka CEO,MD DSTV wapeni raha watanzania, compact, compact+ na premier ni level kubwa ya malipo wote wapeni UCL.

Kisa cha kweli:
Kuna rafiki yangu nimesoma nae hapo UD undergraduate jina namhifadhi...nimeongea naye juzi kwa whatsup call, amenipa habari za kusikitisha sana juu ya ugomvi uliopelekea yeye kuondokewa na mkewe kaachwa na watoto wa3 mmoja mdogo kaondoka na mama yake kisa alikuwa anaangalia mechi sebuleni akisubiria ucl PSG VS MUNIC last week

Anadai ratiba ilionyesha mechi itaonyeshwa SS6 & SS10. amesubiri ulipofika muda mpira umeanza na haoni basi akapigiwa simu na mwenzie akamfuata wakaenda kuangalia huko Brajeck savei mlimani, kwaharaka na kuwahi mwanzo wa mpira, hakutoa taarifa mapema,taarifa alikwenda kutolea huko baada ya kufika tena mpira ulipokuwa halftime.

Mkewe hakuamini alijua kaenda kwa mchepuko kamueleza mpaka kamsikilizisha kelele za mpira bado hakumuelewa. Aliporudi nyumbani mkewe alichukizwa sana japo alikaa kimya. Lakini furaha ya kumuangalia Neymar, Cavan, Mbappe na Demaria iliishia kesho yake alipomuacha mkewe nyumbani asubuhi alipoenda kazini na aliporudi majira ya saa moja usiku hakumkutamkewe nyumbani kwani alishafanya maamuzi magumu.

Hata watoto wake wengine wa shule waliporudi walikuta ujumbe kwa"House Admin"-mfanyakazi wa ndani kuwa ameondoka na mdogo wao wa mwisho,hawezi kurudi amechoshwa na tabia za baba yao kutoka usiku na kurudi usiku wa manane kila kukiwa na mechi za ulaya kwa kisingizio hazionyeshwi nyumbani wakati wanalipa dstv compact ili aone mpira.

Alimwambia H.admin waambie wanangu waishi kwa amani, hajasema amekwenda wapi, nimepatwa na uchungu sana japo nipo mbali maana nakumbuka na mimi nimpenz wa soka...na mpaka sasa mke na mtoto hawajarudi kwa mumewe. Tuchangie mawazo na tumshauri mtendaji wa dstv waruhusu ucl kuanzia compact elf.70,000 ni pesa kubwa ni mshahara wa mtu.hali ni ngumu,
Asanteni.
 
Mkuu, Compact huwa wanaonesha ECL ila ni zile mechi za kiwango cha chini....zile timu zetu pendwa inabidi uwe na Compact Plus au Premium. Hata mimi natamani sana Compact iwe na full ECL games.
 
Kwa wanabodi JF na Mkurugenzi Dstv;

Wapendwa kwa hali ya sasa hela ni ngumu sana matumizi yamekuwa juu kiwango kikubwa na hela haionekani. Tukiachana na malalamiko ya wapenzi wengi wa soka hapa nchini juu ya ughali wa malipo ya dstv package lakini victim wa soka bado wanajitahidi kulipa hivyo hivyo kwa kukusanya huku na kule na kupunguza huku na kule,kujinyima baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima mtu alipe dstv aangalie soka. Chaajabu ni hawa wenzetu wa dstv kukosa huruma.
.
Nadhani cha kupigania na kuombea kwa Tanzania ya sasa ni Internet ya kasi na uhakika i.e. fiber ili tuweze kuondokana na hawa makupe! Mtu ukiwa na Intenet yenye speed nzuri una uwezo wa kuangalia mpaka channels 2000 kwa malipo ya sh. elfu kumi za kitanzania kwa mwezi!
 
Mkuu, Compact huwa wanaonesha ECL ila ni zile mechi za kiwango cha chini....zile timu zetu pendwa inabidi uwe na Compact Plus au Premium. Hata mimi natamani sana Compact iwe na full ECL games.
Mkuu laiti tungekuwa na internet ya speed nzuri hawa jamaa wangefunga virago bila hata kufukuzwa! Siku hizi mambo yote yako kwenye IPTV boxes. Kama ukiwa na android IPTV box au MAG etc unakamua channels hata 2000 tena kwa malipo kidogo mno!
 
Hapa ndio panakatisha tamaa! Mtu hata hufaidi functions za SMART TV
 
Huyo rafiki yako au kama ni wewe ugomvi sio mechi ya ucl? Go back to drawing table na my wife wako muone tatizo la msingi.
 
Mkuu laiti tungekuwa na internet ya speed nzuri hawa jamaa wangefunga virago bila hata kufukuzwa! Siku hizi mambo yote yako kwenye IPTV boxes. Kama ukiwa na android IPTV box au MAG etc unakamua channels hata 2000 tena kwa malipo kidogo mno!
Vipi ulaji wa bando, kwa mwezi si unaweza kujikuta unatumia laki kwa internet?????
 
Vipi ulaji wa bando, kwa mwezi si unaweza kujikuta unatumia laki kwa internet?????
Ndio mkuu. Hapo inabidi ujikamue tena kwenye bando. Ndio maana nikasema tatizo ni Internet ya uhakika. Tukiwa na connection za fiber na bei inapungua wakati speed inakuwa kubwa na stable. Kusema ukweli wireless kwenye ku-stream data siku zote sio realible na tatizo la bongo no hayo mabando yao. Angalau wangefanya unlimited na kila mwezi mtu awe analipa anagalau 20,000.
 
Mbona Hata TTCL wanatumia fiber ila bado gharama zipo juu
 
Bora azam tu hao dstv hata ligi ya spain kifurushi cha 19000 hupati chaneli ya HD
 
Bora azam tu hao dstv hata ligi ya spain kifurushi cha 19000 hupati chaneli ya HD
Mkuu unasema kweli? Nilikuwa na mpango wa kufunga home dstv na package yangu kubwa ingekuwa ni 19000/= na kile cha 40000/=

Kama kweli hamna channels za hd kwenye hiyo package basi bora niwe mpole
 
Azam TV ange take advantage ya weakness za DSTV angefaidika sana.
 
BAELEZEE LAKINI WAO WANAJALI MONEY TU MIMI WIKEND NACHEK KTK LAPTOP YANGU NA MOBDRO SOFTWARE IKIKUPATIA CHANNEL ZA BEIN SPORT MURUA NI BUNDLE LAKO TU .
 
Mkuu unasema kweli? Nilikuwa na mpango wa kufunga home dstv na package yangu kubwa ingekuwa ni 19000/= na kile cha 40000/=

Kama kweli hamna channels za hd kwenye hiyo package basi bora niwe mpole
Kweli mkuu hakuna HD kwa kifurushi cha 19000 bora azam utapata kumwona messi na ronaldo kwa picture clear kabisa
 
Back
Top Bottom