callmeGhost
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 278
- 832
Ndugu yangu, siku hizi mimi na wenzangu wengi tunaangalia soccer kupitia internet. Mfano Halotel Chuo, mia tano, mb 450 naangalia mechi nzima na nabaki na vimb vya kuingia Jf na Instagram.Kwa wanabodi JF na Mkurugenzi Dstv;
Wapendwa kwa hali ya sasa hela ni ngumu sana matumizi yamekuwa juu kiwango kikubwa na hela haionekani. Tukiachana na malalamiko ya wapenzi wengi wa soka hapa nchini juu ya ughali wa malipo ya dstv package lakini victim wa soka bado wanajitahidi kulipa hivyo hivyo kwa kukusanya huku na kule na kupunguza huku na kule,kujinyima baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima mtu alipe dstv aangalie soka. Chaajabu ni hawa wenzetu wa dstv kukosa huruma.
Mfano:
Kuna shida gani mtu anayelipa shs elfu 69,000/= almost 70,000/= kuruhusiwa kuangalia mechi za uefa champions league? mechi zenyewe sio kilasiku ni jumanne na jumatano mara moja au mara mbili kwa mwezi, wakati mwingine ratiba inaonyesha kabisa mechi itaonyeshwa SS10, ama SS3,SS7 lakini dstv wanabadili ratiba na kuzihamisha SS6,SS5,SS2 ilimradi mtu wa compact asizione.
Kumbuka mngeweza kuwa na wateja wengi wa compact kwa hiyo elfu 70 wakalipa pesa nyingi japo mnaona ni kidogo lakini wakawa wengi sana kwakuwa wanauhakika na UCL na EPL kuliko mkangangania premier mpate hela nyingi kukawa na wateja kidogo, jaribuni huo ubunifu kwa miezi miwili muone mtakavyopata wateja .
Inasikitisha kwa usawa huu pesa ilivyongumu mtu anajibana ale maharage na matembele wiki tatu mfulizo alipe shs elfu sabini 70,000/=ama sitini na tisa 69,000/=DSTV na bado aache familia yake usiku aende bar au pub akalipe buku ama buku mbili kila mechi akaangalie PSG na Buyern.
Mechi zenyewe zinachezwa usiku mwingi kurudi nyumbani ni saa sita au saba, ugomvi na familia, kisa compact hawaonyeshi ucl,mtavunja ndoa za watu, jamani watanzania wengi wanapenda soka CEO,MD DSTV wapeni raha watanzania, compact, compact+ na premier ni level kubwa ya malipo wote wapeni UCL.
Kisa cha kweli:
Kuna rafiki yangu nimesoma nae hapo UD undergraduate jina namhifadhi...nimeongea naye juzi kwa whatsup call, amenipa habari za kusikitisha sana juu ya ugomvi uliopelekea yeye kuondokewa na mkewe kaachwa na watoto wa3 mmoja mdogo kaondoka na mama yake kisa alikuwa anaangalia mechi sebuleni akisubiria ucl PSG VS MUNIC last week
Anadai ratiba ilionyesha mechi itaonyeshwa SS6 & SS10. amesubiri ulipofika muda mpira umeanza na haoni basi akapigiwa simu na mwenzie akamfuata wakaenda kuangalia huko Brajeck savei mlimani, kwaharaka na kuwahi mwanzo wa mpira, hakutoa taarifa mapema,taarifa alikwenda kutolea huko baada ya kufika tena mpira ulipokuwa halftime.
Mkewe hakuamini alijua kaenda kwa mchepuko kamueleza mpaka kamsikilizisha kelele za mpira bado hakumuelewa. Aliporudi nyumbani mkewe alichukizwa sana japo alikaa kimya. Lakini furaha ya kumuangalia Neymar, Cavan, Mbappe na Demaria iliishia kesho yake alipomuacha mkewe nyumbani asubuhi alipoenda kazini na aliporudi majira ya saa moja usiku hakumkutamkewe nyumbani kwani alishafanya maamuzi magumu.
Hata watoto wake wengine wa shule waliporudi walikuta ujumbe kwa"House Admin"-mfanyakazi wa ndani kuwa ameondoka na mdogo wao wa mwisho,hawezi kurudi amechoshwa na tabia za baba yao kutoka usiku na kurudi usiku wa manane kila kukiwa na mechi za ulaya kwa kisingizio hazionyeshwi nyumbani wakati wanalipa dstv compact ili aone mpira.
Alimwambia H.admin waambie wanangu waishi kwa amani, hajasema amekwenda wapi, nimepatwa na uchungu sana japo nipo mbali maana nakumbuka na mimi nimpenz wa soka...na mpaka sasa mke na mtoto hawajarudi kwa mumewe. Tuchangie mawazo na tumshauri mtendaji wa dstv waruhusu ucl kuanzia compact elf.70,000 ni pesa kubwa ni mshahara wa mtu.hali ni ngumu,
Asanteni.
Websites kibao zinaonyesha mechi, wewe tu chagua resolution yako, the higher the resolution the higher the bandwidth. Kama kwa mwezi utatumia 2000 tu. Voda wana bundle nzuri za usiku. Tumia hiyo, tena kama una 4g, duhhhhhh utaacha DSTV ishike vumbi. Kuna apps kama KODI, unaconfigure, unaachana na decorder. Channel zote za dstv utazipata.
-callmeGhost