Dira ya UKAWA ni daraja la machafuko ya kisiasa

Dira ya UKAWA ni daraja la machafuko ya kisiasa

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Awali ya yote niweke sawa tafsiri; Machafuko hapa simaanishi mapigano au vurugu zozote zile, nazungumzia hali ya mambo kwenda mrama, kwamba siasa za nchi hii zitakwenda kombo, vyama vinavyounda UKAWA vinacheza pata potea, kuna watakaofaidika na wapo watakaonyonywa. Nitaeleza!

Umoja ni nguvu, hii ni kauli isiyopingika kuwa palipo na mshikamano matokeo huwa mazuri. Migawanyiko haina tija, ndiyo maana zama ambazo Ujamaa uliheshimiwa sana nchini, yalikaririshwa maneno kwa Watanzania kuwa "Kidole kimoja hakivunji chawa."

Vyama vya siasa nchini kwa sasa vipo 22. Vile vinavyoitwa vya upinzani idadi yake ni 21. Hivyo vyote chawa yao ni Chama Cha Mapinduzi (Chama Tawala). Tangu ruhusa ya mfumo wa vingi vya siasa mwaka 1992, imeshindikana kwa chawa hiyo kuvunjwa.

Tupo njia moja kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 ambao una kila dalili ya kuleta mapinduzi makubwa katika historia ya siasa ya nchi yetu.

Mwamko wa vijana ndani ya CCM kumezea mate nafasi kubwa na ‘kugutuka' kwa vyama vya upinzani japo ni kukumbuka shuka asubuhi, kwa pamoja inaleta ladha tofauti.
Tayari tongotongo za ujima zimeshaona mlango wake wa kutokea, sayansi imekamata utawala wake.

Kinachoonekana katika mbio za sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, ni mwamko wa watu (wagombea) kuendana na mahitaji pamoja na kasi ya ulimwengu huu wa ‘dotkom'.

Inavutia mno kuona vijana wanajitathmini na kuona wanatosha kuvaa viatu vya Urais. Mkono wangu wa baraka kwa January Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Zitto Kabwe (Mbunge Kigoma Kaskazini, Mwenyekiti PAC), Dk. Hamis Kigwangala (Mbunge Nzega). Anayesema muda wao anakosea.

Kipindi ambacho mtu anaona anaweza ndiyo wakati wake, miaka ijayo hawawezi kuwa na ufanisi walionao leo.


Augustino Lyatonga Mrema wa leo, siyo yule wa miaka ya 1990 ambaye alitikisa akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu, vilevile akiwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mgombea Urais wa upinzani aliyeichachafya CCM katika Uchaguzi Mkuu 1995.

Cheche za Mchungaji Christopher Mtikila wa miaka ya 1990 ni usiku na mchana kama utamfananisha na wa leo. John Cheyo aliyeitwa Bwana Mapesa, hafanani kabisa na huyu wa sasa. Hata Dk. Willibroad Slaa aliyeingia bungeni tangu 1995 na kutikisa zaidi kati ya mwaka 2005 na 2010 kisha kumpa changamoto pevu Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, halingani hata kidogo na huyu wa sasa.

Basi tutarajie mapinduzi makubwa japo wengine kama Zitto tayari Katiba imewagaya na imeshawamwaga, umri hauruhusu. Ni mapinduzi CCM wakimpitisha Lowassa, kwani ataweka rekodi ya kuwa mgombea Urais aliyewahi kuandamwa na skendo nzito za ufisadi kuwahi kutokea.

Stephen Wasira atakuwa mbunge wa upinzani aliyerejea CCM na kuaminika kupewa nafasi nyeti ya kukiwakilisha chama kuwania Urais. Ukawa wakisimamisha mgombea mmoja pia ni mapinduzi, yaani kila upande utazaa mapinduzi. Siku zijazo nitachambua mapinduzi kwa kila jina mmojammoja.

Leo najadili UKAWA; Walichokifanya kuunganisha nguvu ya pamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 siyo kitu kibaya katika sura nyepesi. Si tulishaambiwa umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu? Vilevile tulishaelimishwa kwamba kidole kimoja hakivunji chawa?
Umoja wao ni mtaji mkubwa dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Dhamira ambayo imewafikisha katika kutiliana saini juu ya makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja kila nafasi, kuanzia Urais, Ubunge, Udiwani na Serikali za Mitaa, ni taa ya kijani katika matokeo ya uchaguzi unaokuja.

Chadema, Cuf, NCCR-Mageuzi, NLD, kila kimoja kina nguvu yake kisiasa, sasa kitendo cha kuzifanya nguvu hizo kuwa moja, unaweza kuona ‘msuli' mkubwa ambao wapinzani watakuwa nao kwenye uchaguzi unaokuja.

UKAWA ni mtaji siyo tu kwa sababu nguvu za vyama vyote hivyo itakuwa moja kubwa, bali pia lipo kundi la watu ambao huona utitiri wa wagombea wa vyama vya upinzani kama fujo, kwa hiyo hususia uchaguzi, lakini kwa umoja huo, sasa itawavutia hao wasuasiaji kupiga kura. Huo ni mtaji mwingine.

Kwa mantiki hiyo, lipo kundi la watu ambao walikuwa hawaoneshi ushabiki wa upande wowote (neutral), ila sasa wataamka na kuonesha hisia. Watu wanapoamua kuungana, kwanza huvutia wengi, kwa maana hiyo hata kama vyama hivyo visingekuwa na mtaji mkubwa wa watu, bado umoja wao ungepata mapokeo mazuri.

Hebu sasa tafakari nguvu ya Chadema, angalia nafasi ya Cuf, vilevile NCCR-Mageuzi, kisha oanisha ushawishi ambao viongozi wao wanao kijamii, ni wazi kwamba Ukawa wataibuka na matokeo makubwa hata kama hawatashinda urais. Nguvu yao itachagiza wabunge na madiwani wengi wa upinzani.

Uchaguzi wa mwaka 2015, bila shaka kwa dira hiyo ya Ukawa, hata kama wapinzani hawatashika mhimili namba mbili wa dola, yaani Bunge, hivyo kulazimisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ni imani kuwa umoja wao utasababisha upinzani wenye nguvu kwa sababu wapinzani hawatazidiwa wabunge wengi na CCM, hivyo kuibua mtifuano wakati wa kupitisha miswada.

KAMA SURA IPO HIVYO, KWA NINI SASA MACHAFUKO?

Utaona kwamba maeneo yote ambayo nimeyachambua yanaonesha kwamba Ukawa ni faida kwa vyama vya upinzani ambavyo vimeamua kuungana. Hata hivyo, jicho langu namba tatu linaona machafuko kisiasa baadaye kupitia dira hii ya Ukawa.

Miaka miwili au mitatu ijayo, Chadema hakitakuwa hiki cha sasa, kadhalika Cuf hivyohivyo. Sura hiyo ipo pia kwa NCCR-Mageuzi na NLD. Machafuko yanayokuja ni kwa sababu ya asili ya wanasiasa na matakwa ya vyama vya siasa.

Kosa kubwa ambalo vyama vinavyounda Ukawa vimefanya ni kuunganisha dira, huku vikiacha kila chama kubaki vilevile. Ni matumaini yangu kwamba watafika salama 2015 na kushirikiana vizuri kwenye uchaguzi lakini baada ya hapo, washinde au washindwe hawatakuwa imara tena.

Kama Ukawa wanataka waendelee vizuri, wakiwa imara miaka yote na wasitetereke hata baada ya uchaguzi, basi waunde chama kimoja kipya chenye sera mpya, viongozi wa vyama hivyo wakubali kuachia madaraka yao na wagombee upya kupata viongozi wapya wa chama kipya.

Kadhalika, waheshimu sera ambazo watakuwa wamezitunga, miiko na muongozo wa chama kipya. Wawe na dhamira ya kweli ya kuwa kitu kimoja katika maisha yao yaliyobaki katika siasa. Vinginevyo ni pata potea.
Nitaeleza kwa nini na nitatoa mifano;


Kwanza kabisa, muungano wa vyama kwa ajili ya kuingia kwenye uchaguzi huibua athari kubwa. Kipo chama hunufaika na kingine au vingine hupwaya baada ya uchaguzi. Vivyo hivyo kwa muungano wa kuunda serikali.

Mfano halisi ni hapa nyumbani;

Mwaka 2000, Chadema kilimuunga mkono Mgombea Urais wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba, matokeo yake yakawa mabaya sana kwa Chadema. Kwanza kilipata idadi ndogo sana ya wabunge, pili, kilitafsiriwa na wananchi kwamba chenyewe ni dhaifu ndiyo maana hakijiamini kusimamisha mgombea Urais.

Tafsiri hiyo kwamba Chadema ni dhaifu, ilisababisha Cuf kushika uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwa muda mrefu. Mwaka 2005, baada ya Freeman Mbowe kuthubutu kugombea Urais, miaka mitano baadaye, kiliweza kuaminika kisha kuwa chama kikuu cha upinzani.

Hapa niweke angalizo kwamba kwa vile hivi sasa Chadema ndicho chama chenye nguvu, matarajio ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, ama vyama vingine vitakinyonya na kupata nguvu kubwa ya kisiasa au Chadema kitavifunika vingine, kuviua na kuviacha majina tu lakini kwa watu havitakuwepo.

Mfano; Hivi sasa Chama cha Liberal Democrats, kinaugulia uamuzi wake wa kukubali kuungana na Conservatives kuunda serikali ya usharika nchini Uingereza kwa sababu kimepoteza mvuto wake na kiongozi wake, Nick Clegg ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa sasa, umaarufu wake umeshuka mno.

Hii ni kwa sababu majukumu mengi ya kiuongozi yanatekelezwa na Conservatives kama chama tawala, wakati Labour kinabaki kuwa chama kikuu cha upinzani. Hapo unaona jinsi ambavyo Liberal kilivyopotezwa, yaani upinzani hakipo, utawala hakipo kwa sababu kilikaribishwa tu kuunda utawala.

Sababu ya kukaribishwa ni kuwa idadi ya viti vya Conservatives katika Bunge la Uingereza (Westminster) ilikuwa haitoshi kumfanya Malkia Elizabeth II amteue David Cameron kuwa Waziri Mkuu na kuunda serikali, hivyo kuomba kuungwa mkono na Liberal ambacho kinaugulia maumivu.

Liberal kimepoteza kuaminika kwa Waingereza (trust), utambulisho wake (identity) na nguvu ya ushawishi (influence) kwa sababu uelekeo wake haujulikani, zaidi kinaonekana kama mpambe.

Vivyo ndivyo itakavyokuwa, kuna baadhi ya vyama vitaonekana wapambe na kipo kitaimarika na kudhihirisha dhamira yake kwa Watanzania.

Upo muungano uliotikisa sana nchini Kenya wa National Rainbow Coalition (Narc), pale vigogo wa Kanu ambacho kilikuwa chama tawala wakati huo, walipojitenga na kuunda Chama cha Liberal Democratic (LDP), kabla ya kuungana na Chama cha National Alliance of Kenya (NAK) cha Mwai Kibaki kisha kutengeneza Narc.

Vigogo wa Kanu, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, George Saitoti na Joseph Kamotho walipopingana na wazo la aliyekuwa mwenyekiti wao, vilevile Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi kutaka Uhuru Kenyatta ndiye awe mgombea Urais wa chama chao, wao wakiona hafai kwa sababu alikuwa bado ‘bwana mdogo kwenye fani'.

Mwaka 2002 Narc kilishinda uchaguzi na kuunda serikali lakini baada ya hapo kilidumu miaka mitatu tu, kwani mwaka 2005 wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini humo, LDP walikwaruzana na Kibaki ambaye alikuwa Rais wa Kenya wakati huo, mgogoro wa kisiasa ukawa mkubwa.

Sababu ya akina Raila na Kibaki kugombana wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba ni kwa sababu muungano wao haukuwa na misingi, isipokuwa waliamua kuunganisha nguvu kwa ajili ya uchaguzi kama ambavyo Ukawa wameamua kwa sasa.

Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, tutakuja kuona mvutano wa vyama hivyo, kila kimoja kikitaka kujiimarisha. Isisahaulike kuwa uhai wa vyama vya siasa Tanzania ni ruzuku, kile chenye uwakilishi mkubwa ndicho kinachopata zaidi, je, chama kipi hakitaki zaidi?

Ni kwa sababu kila chama hutaka kujiimarisha kivyake ndiyo maana tutashuhudia misuguano ya hapa na pale baada ya Uchaguzi kwa sababu ajenda kuu (uchaguzi) itakua imepita. Kila chama kitaangalia maslahi yake na hata hoja mbalimbali tutaona vikipingana.

Tukumbuke kuwa mwaka 2010, vyama vya NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (Cuf), vilipiga kelele sana kutaka nao waunganishwe katika kambi rasmi ya upinzani lakini Chadema chenye wabunge wanaojitosheleza kuunda kambi, wakadengua kisha wakafunga milango. Hawakutaka ushirikiano.

Ukatokea mvutano mkubwa, nakumbuka hata bungeni walitoleana lugha chafu. NCCR-Mageuzi na Cuf waliwaita Chadema ni wabinafsi na kwamba ni hatari endapo watapewa nchi, kwamba kambi tu ya upinzani hawataki kushirikiana na wenzao, je wakishika dola.

Chadema wakasema hawawezi kushirikiana na Cuf kwa sababu kinaunda serikali Zanzibar, wakawaita CCM B. Tundu Lissu akasema, Chadema hakiwezi kuunganisha nguvu na vyama dhaifu, akakitolea mfano UDP chenye mbunge mmoja ambaye ndiye mwenyekiti, John Momose Cheyo.

Hapa ni kuonesha kuwa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ni muungano wa magirini kwa sababu kama kungekuwa na nia ya dhati ya wapinzani kuunganisha nguvu, wangeshafanya huko nyuma lakini kwa sababu za ubinafsi kama siyo uroho wa madaraka, hawakuungana. Wakatukanana!

Tujiulize, Chadema imekuwaje leo kuungana na Cuf ambacho ni CCM B, tena kikiunda serikali Zanzibar? NCCR kimegeuka jiwe leo kuungana na Chadema ambacho ni wabinafsi, tena hatari endapo kitakabidhiwa dola? Kila upande umelamba matapishi yake. Hakuna muungano wa kweli!

Kuna jambo la kushughulikia ndani ya Ukawa kwanza kabla ya mambo mengine. Mwendo wao wa kutolea macho uchaguzi utaleta machafuko ya kisiasa. Vyama vitajitenga na pengine hali ikawa mbaya kwa sababu inahitajika serikali kuwa makini zaidi kama upinzani utakuwa imara.

Imeandikwa na; Luqman Maloto
 
Hivi wewe chizi na machizi wenzenu mnafikiri hivi vipropaganda vyepesi vinaweza kuwakatisha tamaa hawa jamaa. kwanza mmeanza na ruzuku mmeona cd inaanza kubuma mmeanza tena sijui atakayemuunga mwingine mkono wote wataanguka na mwingine ataanguka. pumbavu zenu good for nothing.

OOH hata waungane chama chetu ni imala LAKINI roho zinawauma kweli. si mkae kimya kama wamefanya makosa kuungana.
 
Nyambafu...yaaani umekesha kwa kuandika upuuzi huu?

Tatizo lenu mnadhani kuwa wapinzani hawa ni Raia wa kigeni, hawa ni watanzania na wana haki zote za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni, Nyambafu wewe.....
 
Nadhani MUUNGANO wa vyama vya upinzani wengi walikuwa wanausema lakini hawakuwa na nia vyama vya upinzani viungane,ili CCM iendelee kutawala.

Leo vyama hivi vimeungana tunaazna kufikiria habari za MACHAFUKO,kwa nia yasitokee bila vyama hivi kuungana?Leo tunawajua waandishi wa habari ambao ndoto zao ni kuendelea kufaidika na mfumo wa rushwa na ufisadi ulioko kwenye TAIFA letu,kweli kabisa waandishi hawa hatufai hata kidogo,hata kwa kupewa bure hawafai.
 
CCM haiwezi kutawala milele, UKAWA ni njia moja wapo ya kukidhoofisha ccm.

Njia nyingine ni makundi ndani ya ccm - hili bado alijashughulikiwa vizuri. CCM ni sawa na umoja wa makundi na itikadi tofaauti za kisiasa, na hili hasa ndo linaleta ugumu. Taswira ya makundi ndani ya ccm inatakiwa ijengewe hoja, iweze kutoa picha kwenye jamii hasa ya wanahabari kwamba makundi ndani ya ccm hayana tofauti na muungano wa vyama vya siasa. Hii itatoa mwanya kwa watu ndani na nje ya ccm kutokuino ccm kama Mungu na badala yake kuangalia uwezekano mwingine zaidi nje ya ccm.
 
Roho ya farao na izidi kutawala mioyo ya wana-ccm ili umauti wao uwanyatie bila wao kufahamu kuwa hatamu yao imefika.
 
Hahaaaa hivi Jubilee ya Kenya na CORD vimeuwa vyama vyao? Hebu Acheni Ulimbukeni, haya mambo hayajaanza kufanyika Tanzania. Muungano wa vyma ukishasinda dola, Muungano wao ndo unaunda serikali vyama vinaendelea kama ilivyo sasa kila mtu anafanya shughuli zake. Ruto Kenya kabakiwa na chama chake, Uhuru kabakia na chama chake. Sasa kwanini mnadhani itakuwa tofauti hapa kwetu Tanzania.
 
Nadhani MUUNGANO wa vyama vya upinzani wengi walikuwa wanausema lakini hawakuwa na nia vyama vya upinzani viungane,ili CCM iendelee kutawala.

Leo vyama hivi vimeungana tunaazna kufikiria habari za MACHAFUKO,kwa nia yasitokee bila vyama hivi kuungana?Leo tunawajua waandishi wa habari ambao ndoto zao ni kuendelea kufaidika na mfumo wa rushwa na ufisadi ulioko kwenye TAIFA letu,kweli kabisa waandishi hawa hatufai hata kidogo,hata kwa kupewa bure hawafai.

Wanafiki siku zoke wamekuwa wakisema vyama vya upinzani viunganishe nguvu, mara chadema wabinafsi hawataki ushirikiano na wengine, leo sasa chadema imekubali kuungana na vyama vingine na upinzani umeamua kuweka tofauti zao pembeni na kuunganisha maslahi ya nchi, wanatokea waandishi uchwara wanahangaika kukejeli huu Mungano na kuutabiria kifo, watanzania tumejitambua haturudi nyuma.
 
Yani walivyoshupaa utadhani hii nchi ni ya kwao pekee yao.
Naamini ccm wamepanic baada ya kuona the beginning of their end.

Na katika kupanic kwao wanashindwa kuangalia walipojikwaa ni wapi wako busy kuondoa chupa walipoangukia.. Kila mtu amekuwa msemaji kama kambale.. Kama yaliowakuta wale waliokuwa wanatengeneza mnara wa Babeli ndo yanayowakuta ccm.. Kila mtu sasa anaanza kusema lugha yake..
 
Wanafiki siku zoke wamekuwa wakisema vyama vya upinzani viunganishe nguvu, mara chadema wabinafsi hawataki ushirikiano na wengine, leo sasa chadema imekubali kuungana na vyama vingine na upinzani umeamua kuweka tofauti zao pembeni na kuunganisha maslahi ya nchi, wanatokea waandishi uchwara wanahangaika kukejeli huu Mungano na kuutabiria kifo, watanzania tumejitambua haturudi nyuma.

Nadhani ni wale waandishi ambao UKADA huwa hauwatoki kwenye kalamu yao.Wao chema ni kibaya na kibaya ni chema.Leo Lowassa anakumbuka shuka asubuhi,hivi alikuwa wapi kuomba radhi akiwa ndani ya Bunge lao la Mipasho na Matusi kuomba radhi?Wameona kengele imeanza kugonga wanashtuka.

Wanatakiwa wajifunze kutoka Burkinafaso,japo IKULU ni tamu lakini kuna wakati TAMU hugeuka shubiri.
 
Hahaaaa hivi Jubilee ya Kenya na CORD vimeuwa vyama vyao? Hebu Acheni Ulimbukeni, haya mambo hayajaanza kufanyika Tanzania. Muungano wa vyma ukishasinda dola, Muungano wao ndo unaunda serikali vyama vinaendelea kama ilivyo sasa kila mtu anafanya shughuli zake. Ruto Kenya kabakiwa na chama chake, Uhuru kabakia na chama chake. Sasa kwanini mnadhani itakuwa tofauti hapa kwetu Tanzania.


Hizo changamoto ni za kawaida sana ktk siasa. Tunakiwa kuwa na Waandishi wenye upeo na uelewa mpana kuelimisha wasomaji wao. Siyo makala ya kikanjanja kama hii.

Tutafika wakati mmoja Vyama vyote vitakosa wingi wa kura kuunda Serikali. Itabidi chama kilicho ongoza kwa kura kifanye ushirikiano kama huu wa Ukawa kiweze kuunda Serikali.

Kwa hiyo tusishangae kusikia siku zijazo hata CCM(kama kitaendelea kuwepo) kikifanya ushirikiano na vyama vingine. Siyo dhana mpya,majirani zetu Kenya,nchi nyingi za Ulaya,Israel,India,Ujapani,nk imezoeleka sana.
 
UKAWA watakufa tu kwa sababu watanzania wameshatambua hila zao mbaya kwa msatakabali wa amani ya Tanzania ya kesho.
 
hivi vyama vya upinzani kuungana imekuwa dhambi au? huyu mwandishi uchwara badala uanishe changamoto zinazowakabili UKWAWA na namna ya kudeal nazo, yeye anaanza kutisha watu machafuko.. pamba.ff kabisa kanjanja mkubwa!
 
Back
Top Bottom