Wameshahakikisha wamemuua Gadaffi, sasa wanamsakama El-Bashir. Ingawa sijafuatilia kwa undani naanza kuamini Wamarekani na mataifa mengine makubwa wana mkono Al-Shabaab, historia inatuonyesha ni jinsi gani mataifa haya makubwa yaliwahi kuwatumia hawa hawa akina Osama na Al Zawahir kupambana na wenzao wakati huo kisha wakaja kugeukana na kuanza kutafutana miaka ya karibuni. Nahisi.., nasema tena kwamba nahisi... Al-Shabaab hawajaja ila wameletwa, imepita muda wakiwa hapo Somalia bila ufuatiliaji wowote lakini wakaonekana hawana madhara makubwa. Wakaambiwa wawachokoze Kenya, kisha Kenya wakaambiwa msikubali kuchokonolewa wafuateni kabisa huko kwao kisha muwamalize mkishindwa tutawasaidia msijali. Kenya wakadumbukia Somalia, sasa imeshakuwa taabu maana wamevua nguo kuruka bwawani wamegundua maji ni mengi kuliko walivyokuwa wanafikiri. Hawajakaa vizuri wakaambiwa El Bashir alishawahi kuja hamkumkamata, sasa ili akija muwe na uwezo wa kumkamata toeni warranty kutoka hapo hapo Mahakama Kuu ya Kenya???? Pumbaf, non-sense... Je itakuwaje Kesho Mahakama Kuu ya Tanzania ikitoa warranty ya kumkamata Kibaki??? itakuwaje Uganda wakitoa warranty ya Kumkamata Kikwete??? Waafrika tunagombanishwa na hawa wazungu tukiwa tunaangalia kwa macho yetu wenyewe. Kwanini tunaendekeza sera na kuwasikiliza hawa wazungu kwa kiasi kikubwa hadi tunajiharibia wenyewe? angalia sasa El Bashir na Kenya hawataongea tena, mabalozi wesharudishwa makwao na urafiki kwisha.
Kwa mwendo huu, nakuambieni hatuna muda mrefu tutaanza kudundana wenyewe kwa wenyewe. Kama hizo ni zile njama zao za kuvuruga dunia kisha waweke system wanayoijua wao basi inakuja kwa kasi sana maeneo yetu sasa hivi. Nina hakika hatuna tena Rais wa nchi yeyote Afrika anayeweza kusema lolote kuhusu haya mambo yanayoendelea, wazungu wanazidi kuja kutuvuruga kwa kasi kila wanapoona kuna nafasi ya kufanya hivyo kwa udhaifu wetu. Wao wanatumia muda mwingi kujiimarisha na kuhakiki sisi hatuendi popote, watachukua rasilimali zote mkikataa na msipokuwa makini wanawagombanisha na wakati ninyi mnauana wao wanaongeza mafuta kwenye moto kwa kuwauzia silaha huku wakibadilishana na rasilimali za nchi husika. Wanachukua kila kitu na kujidai wanawapatanisha na kuwajengea nchi.
Sitaki kutabiri kitachotokea wala sitopenda kitokee, ila kama Mungu anaona linalotokea na analiacha litokee basi lina sababu ya kutokea ingawa litatuumiza sana muda si mrefu unaokuja. Wenye kujua kama hili liliandikwa litokee watujuze na wenye data zaidi naomba michango yenu tujue kama ni kusubiri tumezwe ama tujue kama kuna la kufanya kuepuka haya, mimi niko tayari kufia hapa kama Gadaffi.