stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
Ukilitazama kwa jicho la tatu utagundua kuwa sakata la mchanga halina tofauti kubwa na chanzo cha yaliyotokea Zimbabwe,Libya,Sudani nk
Hivyo kujikwamua kutoka kwenye unyonyaji huu na wizi wa rasilimali za taifa hususani kwenye madini kama dhahabu,shaba,tanzanite,fedha,chuma na gesi inahitajika mbinu ya kidiplomasia zaidi badala ya papara na mabavu
Hii inatokana na ukweli wezi hawa wa rasilimali ni wasomi na werevu sana ndio maana wanafanikiwa kutuingiza kwenye mikataba kandamizi inayowanufaisha wao badala ya taifa husika kama ilivyotokea katika mchanga wa dhahabu
Dawa ya mwerevu ni kwenda naye kiwerevu vinginevyo ukienda naye kwa pupa na mabavu(mbinu ya kizamani) huwezi kufikia malengo yenye mafanikio kwa taifa badala yake unaweza hata kujikuta kwenye migogoro isiyo ya lazima katika biashara ya kimataifa
Kwa kuanzia ushauri wa Lissu wa Tanzania kujitoa kwenye bodi ya kimataifa ya uwekezaji yenye masharti yenye kuwalinda wawekezaji ambapo Tanzania ni mwanachama.Baada ya hapo ndipo tunaweza kuvunja mikataba ya kiwizi kisha baadae tutakuwa katika nafasi ya kuwabana wawekezaji watulipe fidia ya dhuluma yote waliyoitendea nchi yetu
Mbinu hii itaweza kutuepusha na migigoro mikubwa ya biashara za kimataifa,pia itatusaidia kupata haki yetu bila mikwaruzo na wawekezaji ambao bado tuna wahitaji